WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, October 14, 2012

Serikali kutoa uamuzi mgogoro wa ardhi


 Wananchi wanayoizunguuka Kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya Kisaka saka wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akizungumza nao baada ya Tume aliyoiunda kuchunguza mgogoro wa pande hizo mbili kushindwa kuwasilisha kwake Ripoti aliyoiagiza Mwezi Julai 2012.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa ahadi ya Serikali kwa wananchi wa Kisaka saka ya kutoa maamuzi muda si mrefu kuhusiana na mgogoro wa ardhi kati yao na kambi ya Jeshi la Wananchi ya Kisaka saka.
 Mwanafunzi Ibrahim Makame wa Skuli ya Msingi ya Kinduni akifurahia msaada wa Meza 50 na Viti 50 vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi kwa skuli yao ya Msingi ya Kinduni na na Idadi kama hiyo kwa Skuli ya Msingi ya Mgambo.
Mwanafunzi Raya Ali Ali wa Skuli ya Msingi ya Mgambo akivalishwa Mkoba na Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi . Mkoba huo ni miongoni mwa Mikoba mengine 560 aliyoitoa kwa Wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu wa Skuli za Kinduni, Mgambo, Kirombero na Kiwengwa.
 
Na Othman Khamis Ame OMKR
 
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kutoa uamuzi wa moja kwa moja katika muelekeo wa amani kufuatia mgogoro wa ardhi uliopo kati ya Wananchi wa Vijiji vya Fuoni, Maungani , Kombeni na Dimani pamoja na Kambi ya Jeshi laWananchi wa Tanzania {JWTZ } iliyopo Kisaka saka.
Balozi Seif alitoa Kauli hiyo wakati akizungumza na Wananchi wa Maeneo hayo hapo katika Kituo cha Afya cha Fuoni Kibondeni baada ya Tume aliyoiunda mwezi Julai mwaka huu kumpatia ripoti ya Mgogoro huo kushindwa kuwasilishwa kwakwe tokea mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka Wananchi hao kuendelea kuwa na moyo wa subra wakati Serikali inalitafakari kwa kina suala hilo kwa ajili ya kulipatia ufumbuzi utakaoleta afueni kwa pande zote mbili.
Alisikitishwa na maagizo aliyoyatowa wakati wa Kikao chake na pande hizo mbiliTarehe 7 Julai mwaka huu kwa hatua yakuanzia ya kuuagiza Uongozi wa Kambi ya Kisaka saka kulirejesha Bambo mahali palepale walipokubaliana na Wananchi hao.
“ Hakukuwa na haja ya kutoa maamuzi ya haraka kuhusiana na Mgogoro huo ndio maana nikaunda Tume hiyo lakini chakusikitisha hadi sasa sijaletewa ripoti hiyo kama nilivyoagiza kuletewa mwishoni mwa Mwezi wa Agosti mwaka huu.” Alisisitiza Balozi Seif.
Balozi Seif alieleza kwamba Serikali isingependa kuona Jeshi lililoundwa kwa ajili ya kutumikia Jamii linaendelea kuwa na mifarakano na Wananchi katika utekelezaji wa majukumu yake.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaahidi Wananachi hao kwamba yale yote waliyokubaliana na Uongozi wa Jeshi hilo la Wananchi wa Tanzania {JWTZ}yatekelezwa ipasavyo.
Nipeni muda kutokana na hivi sasa kutingwa na shughulki za Baraza la Wawakilishi. Nadhani mnaelewa kwamba mimi ndie Mkuu wa shughuli za Serikali. Lakini nikimaliza tu jibu la suala hili nitajuka kulitoa hapa hapa bila ya kuchukuwa muda mrefu”. Alifafanua Balozi Seif.
Mapema Mwenyekiti wa Kamati ya Wananchi hao wa Vijiji vya Maungani, Kombeni, Fuoni ,kisaka saka na Dimani Ndugu Khamis Vuai Makame kwa niaba ya Wananachi wenzake wameiomba Serikali kuyachukulia hatua za haraka yale mambo waliyokubaliana na uongozi wa Jeshi hilo.
Ndugu Khamis alisema bado wataendelea kulalamikia kutokuwepo kwa uhalali wa ramani ya Kambi hiyo wakati wananchi hao ndio wenye hati ya umiliki wa ardhi hiyo kwa mujibu wa sheria na taratibu za Mamlaka inayohusika na Ardhi hapa Nchini.
Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Wananchi hao alimuelezea Balozi Seif kwamba Jeshi hilo limeingia katika Mgogoro huo wa ardhi kwa utashi wa baadhi ya watu kwa maslahi mengine.
Ndugu Khamis alisisitiza kwamba wanaamini chanzo cha mgogoro huo kitamalizika kwa kutumiwa vikao jambo ambalo wamempongeza Balozi Seif kwa hatua anazoendelea kuchukuwa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliunda Tume ya kuufuatilia Mgogoro huo wa ardhi kati ya Kambi ya Jeshi la Wananahci wa Tanzania { JWTZ } na Wananchi wanayoizunguuka kambi hiyo tarehe 7 julai mwaka huu.
Hata hivyo Tume hiyo imeshindwa kuwasilisha ripoti iliyoagizwa baada ya wananchi hao kuhitilafiana baadhi ya masuala na Mwenyekiti wa Tume hiyo ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Magharibi.
Wakati huo huo Balozi Seif Ali Iddi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kitope amekabidhi Meza 50 na Viti 50 kwa Skuli ya Msingi ya Kinduni na idadi kama hiyo kwa Skuli ya Msingi ya Mgambo zilizomo ndani ya jimbo lake.
Ugawaji wa meza na viti hivyo ulikwenda sambamba na utoaji wa mikoba 560 kwa ajili ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu wa Skuli za Kinduni, Mgambo,Kiwengwa pamoja na Kirombero.
Msaada huo wote wa Meza, Viti pamoja na Mikoba unakisiwa kugharimu jumla ya Shilingi za Kitanzania Milioni Kumi na Sita { 16,000,000/- }.
Akizungumza na Wanafunzi ,Walimu pamoja na baadhi ya Wazazi wa Skuli hizo mbili za Kinduni na Mgambo Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi alisema Uongozi wa Jimbo hilo utaendelea kujitahidi katika kutafutambinu za kupata Vikalio vitakavyokidhi mahitaji ya Wanafunzi wa Jimbo hilo katika zile Skuli zenye Madarasa mapya.
Balozi Seif aliwataka wanafunzi hao kuhakikisha kwamba wanavitunza vyema Vikalio hivyo kwa lengo la kumudu kwa kipindi kirefu kijacho.
Wakitoa shukrani kwa niaba ya Walimu, Wazazi na Wanafunzi wa Skuli hizo Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Msingi ya Kinduni Ndugu Rashid Khamis Kombo na Mwenzake Msaidizi Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Mgambo Ndugu Salum Seif Salum wameelezea faraja yao kutokana na msaada huo muhimu kwao.
Hata hivyo Walimu hao wameuomba Uongozi wa Jimbo hilo kuendelea kusaidia kutatua baadhi ya kero zinazowakabili katika mazingira yao ya katika dhana nzima ya kuwajengea mazingira bora ya kitaaluma Wanafunzi wao.
Katika hafla hiyo Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope aliahidi kutoa Shilingi milioni Tatu { 3,000,000/- } kwa ajili ya kulipa fidia kwa Mwananchi Mmoja ambaye jengo la Nyumba yake ya Kuishi limo ndani ya Ramani ya eneo la Skuli ya Msingi ya Mgambo.

No comments:

Post a Comment