WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, September 29, 2011

IGUNGA, IGUNGA USIHARIBU USTARABU WETU WA AMANI NA UTULIVU

JE NI MAZINGIRA GANI YANAANDALIWA NA VYAMA KUELEKEA UCHAGUZI MDOGO IGUNGA- TABORA?

Oscar Ameringer aliwahi sema kuwa "Politics is the gentle art of getting votes from the poor and campaign funds from the rich, by promising to protect each from the other" -
Hiki ndicho kinachotokea Igunga kwa sasa vyama kupitia wanasiasa wao wanajitahidi kuvuna kura kutoka kwa wananchi wa kawaida “ wenye kipato cha chini au kwa ufupi masikini; kwa msingi huu wanasiasa huwapumbaza masikini walala hoi kwa kuwanunua ili wawapigie kura bila wao wenyewe kujua kwa kutumia sera na mapenzi yao kwa chama husika na wakati mwingine kuwapatia pesa ambazo wanazipata kwa matajiri wenye malengo binafsi mara ushindi ukipatikana.

Pesa au rushwa ambayo inatolewa na wanasiasa ni mfumo wa utendaji wa kufikisha ujumbe kwa wanachama wao ili wahakikishe kwa naman yeyote ile ushindi unapatikana, kwa kauli mbio tofauti tofauti zinazoashiria maendeleo; kwa msingi huu  wa kampeni ni wakati wa neema au mavuno kwa wafuasi wao na wananchi wanyanja.
Siasa ni ushindani na ni utaalau wa juu kabisa wa kupangilia mikakati hata kama ni ya uwongo, ili mradi lengo la kushika dola litimie. Kutokana na falfasa hii Ifahamike kuwa sio kila mtu au kila chama kinanafasi sawa katika aina hii ya kushiriki katika kuufikisha ujembe; uzoefu hutumika vitisho nya kuwatisha wanyonge hutmika pia; pesa ndo usiseme; Nguvu hii ya pesa huviondoa vyama vidogo ambavyo haviwezi kushindana na kuviacha vyama vyenye nguvu kama inavyotokea Igunga wakati huu wa kampeni ya nafasi ya Ubunge.

Wanasiasa akisimama ulingoni kauli zao ni namana ya kutatua kero za wananchi katika kuondoa kero zao; sikiliza kiini chote cha kampeni huko Igunga kwa sasa ni kutatua kero za wananchi wa Igunga kwa kunadi sera mbalimbali za maendeleo tutafanya hili na lile;
Tatizo kubwa la wanansiasa sio wakweli na hawajali hasa wakisha pata au wakishachaguliwa; wanakuwa na sababu nyingi tu za kujitetea, lakini ukweli hawajali tena kwani walichotaka si wamepata kushika dola.

Kama semi hizi tatu za kiingereza zinavyosema:.
l  When the ruler himself is 'right,' then the people naturally follow him in his right course."
l  “Whatever the best man does, others do that also. The world follows the standard he sets for himself”.
l  "If a ruler himself is upright, all will go well even though he does not give orders. But if he himself is not upright, even though he gives orders, they will not be obeyed."

Semi hizi zinajumuisha tabia za wanasiasa wetu namna wanavyotakiwa wawe ili kujenga imani kwa wananchi na maendeleo ya taifa letu.
 Turudi Igunga; Kilio kikubwa kwa hivi sasa huko Igunga ni matumizi mabaya ya pesa, pengine rushwa na tukumbuke kuwa rushwa ni jiko ambao zambi  zote hupikwa huko; kwani watu hawa  hutaka kuwa viongozi ili wajitengenezee faida binafsi, ni sawa na mwanaume ambaye sio mkweli anavyoweza kumdanganya mwanamke ili aweze kuutumia mwili wa mwanamke huyo katika kutimiza kujifurahisha yeye mwenyewe; baada ya kufanikisha haja yake humdharau na kumwona sio kitu tena hata kama walikubaliana katika kusaidiana ahadi hizo zote huyeyuka na kumwacha mwnamke huyo akisononeka kwa uaminifu wake na kujitoa kwake.

Je fujo zinazoendelea huko igunga je zinatokana na wananchi hasa vijana kuelewa haki zao na nia yao na kutaka kiongozi atayechaguliwa awe kweli mtatuzi wa shida zao? Au ni vurugu tu ambazo zinachochewa na wanasiasa kwa kutumia pesa ili iwe ni sababu ya kuvuruga amani ambayo ilitakiwa itawale uchaguzi huu mdogo? Au vyama vinaandaa sababu mapema ili hata vikishindwa katika uchaguzi viweza kuhalalisha matokea kuwa wameshindwa kwa sababu hii au ile;

Tatizo langu leo hii ni hili, aina hii ya kampeni inaharibu moja ya msingi wetu mkubwa san asana ambao ulijengwa na waasisi wa taifa hili utamaduni wa uvumilivu unavyobomoka hivi sasa. Tukumbuke kuwa taifa hili linafahamika ni miongoni mwa taifa ambalo lilikuwa limetulia na wananchi wake wamekuwa wakivumiliana sana. Je kwani nini leo hii wanasiasa wanatupeleka katika hali ya kuvunja umoja wetu? Wanatutakia nini hawa wanasiasa na vizazi vyetu? Wanatamani nchi hii isitawalike kwa faida yao? Kwa nini wanaingiza  roho ya ukatili kwa vijana wadogo?

Nafikiri bado kuna kila sababu ya wanansiasa kutambua kuwa ni dhambi sana kuchezea amani ya nchi kwa masilahi binafsi na ya muda mfupi na kuliacha taifa katika janga kubwa la uvunjaji wa amani.

Pamoja na ushindani wa siasa huko Igunga lakini uchaguzi huu mdogo usiwe sababu ya kuvunja amani; tunawaomba wasimamizi wa sheria zihusuzo uchaguzi wawe makini kuhakikisha kuwa taratibu zote zinafuatwa bila kumwogopa mtu, au kikundi chochote  au chama chochote kile.

Muhimu ni kwamba tuzike tofauti zetu kwa faida ya taifa letu na vizazi vyake.
MUNGU IBARIKI TANZANIA

Sunday, September 25, 2011

IGUNGA INATUPELEKA WAPI KAMA TAIFA


Igunga imegeuka fitina ugomvi na mbaya zaidi sio ugomvi wa hoja ni ugomvi wa misuri ambao hauna tija kwa Taifa letu.

Tunaendelea kujiuliza kwa nini wakati kampeni za hicho kiti kimoja tu zikiwa zinakaribia kufikia ukingoni  tunaendelea kushuhudia matukio yanayotishia uvunjaji wa amani, yanazidi kuongezeka.
Kama vile, Kudhalilishwa kwa watendaji serikali na vyama na serikali




Kujihami kwa baadhi ya viongozi hadharani, kama ndugu yetu Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM), akiwa na bastola kiunoni akiwa akihutubia katika mkutano wa kampeni. Kama magazeti mengi  yalivyoonyesha kuwa” Bastola ya Rage ilionekana wakati mbunge huyo akijiandaa kupanda jukwaani kwa ajili ya kumnadi mgombea ubunge wa CCM kwenye moja ya mikutano ya kampeni jimboni humo”.





Kama Mwandishi  wa makala hiyo alipouliza”Kwa sababu hiyo, tunajiuliza, Rage alikuwa akikabiliwa na hatari gani hadi kulazimika kupanda jukwaani ni bastola? Hivi kila mwenye silaha ya moto Igunga akisema atembee na silaha yake hali itakuwaje?Na kwa wasio na silaha za moto, wakiamua kutoka na silaha za jadi kama mishale, visu, mapanga na zinginezo, Igunga patakalika? Sisi hatuungi mkono kitendo hicho na tunalitaka jeshi la Polisi kuchukua hatua ili kuhakikisha kampeni za uchaguzi Igunga na hatimaye uchaguzi wake, unafanyika katika mazingira ya utulivu na amani.”


Nakubaliana kabisa na mwandishi wa makala hii kuwa huu ni udhaifu mkubwa kabisa kwa wasimamizi wetu wa maswala ya amani na utulivu; Mheshimiwa Mbunge hakuwa na sababu yeyote ile ya kuja kwenye kampeni na silaha, kama alikuwa na uhakika kuwa usalama wake ulikuwa mashakani kulikuwa hakuna sababu yeyote kwa yeye kujumuika katika kampeni  kwa siku na wakati kama huo.



Tunafahamu kuwa vikosi vyetu vya ulinzi na usalama jamani viko na vinaendelea kuwa makini katika kulinda amani ya wakaazi wa Igunga na taifa kwa ujumla katika wakati huu wote wa kampeni;



Tukio nyingine ambalo nalo limepigiwa sana kelele ni kitendo alichofanyiwa DC; kwa wahusika wote wale katika sakata hili la kumdhalilisha Mama huyu; kumekuwa na matumizi ya nguvu zaidi kuliko busara;hata kama wahusika wanakana na kuona waliyofanya ni sawa, ukweli ni kuwa kosa lilifanyika watake wasitake; Busara busara jamani tunahitaji sasa kuliko wakati mwingine wowote huko nyuma.


Bado ni ukweli ambao haufichiki kuwa Heshima kwa viongozi wetu  na hata kwa mtanzania yeyote na  mtu yeyote ni muhimu. Nafikiri tulitakiwa kuangalia sheria na hatua zake na sio kumdhalisha kama alivyofanyiwa huko igunga katika eneo lake la kazi. Ni busara kujaribu kuepuka kujichukulia sheria mkononi;

Tukikumbuka sana wosia wa  Baba wa Taifa kuwa watanzania wote ni ndugu. Ni vema basi sote kama taifa tukafuata sheria tulizojiwekea bila kujali itikadi za vyama; na wabunge wetu wakawa mstari wa mbele katika kuishi kwa matendo yale wanayoyapitisha bungeni na sio kuwa vinara wa kuongoza fujo na uvunjaji wa sheria hizo. Sisi kama taifa tujitahidi kwa pamoja kudumisha amani! “Inawezekana timiza wajibu wako”

Hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa mawazo, ni umaskini mbaya  sana'  Mwalimu J. K. Nyerere,

Mtu mwenye akili akikuambia neno la kipumbavu -ukalikubali, anakudharau!'  Mwalimu Nyerere


Kama  Taifa tusimame imara katika kupigania "umoja, amani na upendo miongoni mwetu" hii ni kati ya zawadi kubwa sana ambayo  waasisi wa taifa letu Mwalimu Nyeyere na Mzee Abeid Karume walituachia

Tuache kuburuzwa na upepo wa siasa na wanasiasa; ambao wanapigania zaidi masilahi binafsi  na sio masilahi ya taifa, tufunguke sasa.

Nawatakieni Kampeni za mwisho mwisho zenye amani  na nguvu ya Hoja na sio matumizi ya Misuri

Friday, September 23, 2011

KAULI YA WAZIRI MKUU MHESHIMIWA MIZENGO PINDA KUHUSU UTENDAJI WA POLISI NA SAKATA LA SUKARI


POLISI WANAPOSHINDWA  KUSIMAMIA SHERIA NA WAJIBU WAO; FIKRA YAKO NI IPI?

Polisi ni chombo cha serikali chenye nguvu ya kisheria ya kuhakikisha kuwa sheria zinafuatwa, na usalama wa raia na mali zao unakuwepo.

Maswali ambayo sisi raia tunajiuliza leo kama polisi wanalindwa na sheria ya kuhakikisha kuwa nchi inaendelea kubaki salama;
Je Polisi wanaposhindwa kuwajibika kinyume na kiapo cha utii wa sheria zilizowaweka kazini kwa kushindwa kuitumikia nchi na wananchi wake kwa uadilifu nini kifanyike? Kuyahamisha majukumu yao kwa chombo kingine cha ulinzi au kuwawajibisha?
Je tuwafanye nini baadhi ya polisi wanaotumia lugha za ubabe, vitisho na kutumia nguvu hata wakati hakuna sababu ya kutumia nguvu kutatua katika utendaji wake.

Je polisi wetu  wanatumiaje mafunzo yao  katika kuwaelimisha raia kuhusu makosa mbalimbali yanayofanyika, kwa sababu sio makosa yote yanapelekwa mahakamani?

Je askari wetu wanauhusiano wa namna gani  na jamii inayowazunguka? Je polisi wetu wanatumia sheria zaidi au ubabe katika kushughulikia kero za raia wake?

"Je polisi anapomiliki biashara  kama daladala anaweza kusimamia sheria vizuri ambayo inahusiana na biashara yake hiyo ya daladala pale uvunjaji wa sheria ukitokea?"


Je polisi wetu ni msaada kwa raia wenye shida kama inavyofanyika katika nchi nyingine au ndo wanakuwa chanzo cha kero?
je ni jakumu la askari yeyote ambaye anayefanya doria dhidi ya majambazi  ni lipi au anaruhusiwa pia kufukazana na wakosaji wangine kama “daladala” kwa wakati mmoja?

Je ni sahihi kwa polisi kusindikiza magari ambayo yanabeba magendo kama swala la sukari hivi sasa? “ escot ya Mzigo”? Kilio cha waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda katika ziara yake huko Mara jinsi polisi wanavyoshiriki kuhujumu uchumi wa nchi.

Nafikiri itakuwa vyema kama  polisi wetu wataendelea kuwa rafiki wa raia wema ili kuwawezesha kupata ushirikiano katika kubaini wahalifu. Tunazidi kuwaomba  waendelea kufanya kazi zao kwa kufuata sheria na kiapo chao.UWEZO kuchapa kazi vizuri wanao, SABABU wanayo kuendelea kulinda amani; tatizo tu NIA inachechemea pengine kwa sabau ya uduni wa masilahi basi tunaiomba na serikali yetu iliangalie hili la masilahi bora kwa polisi wetu.

Thursday, September 22, 2011

Friday, September 16, 2011

SHERIA ZETU TUNAPOZIPA MUHALI NI UWAJIBIKAJI AU UZEMBE?


KUFUATIA AJALI YA MELI YA “MV SPICE ISALANDER “SISI KAMA TAIFA TUFANYE NINI KUEPUSHA HALI HII ISITOKEE TENA?

Mwishoni mwa wiki kulitokea ajali mbaya ya kupinduka kwa Meli na kuzama, ajali ambayo imesababisha vifo vya watanzania wenzetu zaidi ya 200 wengi wao wakiwa wananwake na watoto, ajali ambayo ilitokea katika bahari ya Hindi katika eneo lenye mkondo mkali wa Nungwi ikiwa inaelekea Pemba;

Msiba huo ni mkubwa kitaifa kwani umekatisha maisha ya watanzania wenzetu ambao ni nguvu kazi yetu kwa maendeleo yetu; wengi wa aliofariki ni wazazi wa familia zetu na watoto ambao walikuwa wanaandaliwa kwa ajili ya maendeleo yetu ya kesho.

Kwa mara nyingine nachukua nafasi hii kutoa pole kwa  kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa wazazi kwa msiba huu mkubwa. Na kwa viongozi wetu wakuu wa taifa letu Raisi wa Serikali ya Mapinduzi Ya Zanzibar pamoja na timu yake yote ya uongozi; Raisi wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania na timu yake vile vile;

Swali ambalo limenigusa sana siku hii ya leo ni hili kwa nini ajali hii ilitokea?

Ni kweli imekuwa ajali kama ajali ambayo imekuja bila hodi na haikuwezekana kabisa kuepukwa?

Je ni ajali ambayo imechangiwa na uzembe wa usimamizi wa wajibu wetu kama watendaji?

Je ni tatizo la uwajibikaji na kuweka rehani ya maisha ya watanzania  kwa kuendekeza “ muhali” na kushindwa kusimamia na kukemea sheria katika atendaji pale panapohitaji kufanya hivyo?

Je ni tatizo la tamaa ya wamiliki wa vyombo na wasimamizi wa miradi hivyo kushindwa kufuata taratibu zinazoongoza biashaya zao?

Mwananchi wa kawaida atajiuliza lakini serikali zetu ziko wapi katika kuwajibika?

Au zinasubiri kuwajibika baada ya tatizo kutokea au hufanya kazi vipi ( management in crisis or management after crisis or crisis management)?

Leo naungana na kauli ya Waziri katika Afisi ya Makamo wa pili wa Rais, Mhe Mohamed Aboud Mohamed

 “amesema,kuwa kamati maalum itaundwa ili kuchunguza juu ya ajali hiyo na ikibainika kuwa uzembe umepatikana sheria itachukua mkondo wake”. ..
”kuwa tatizo kubwa la wazanzibari ni muhali, na amesema ili utendaji mzuri uwepo, lazima suala hili la muhali liwekwe upande ili nchi ipige hatua za maendeleo, na ikibainika kuna watu wanafanya uzembe wa kikazi lazima hatua za sheria zichukuliwe”

Tunaipongeza kauli hii ya awali ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwa itawachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainiika kufanya uzembe uliosababisha kuzama kwa meli ya Spice Islanders huko katika mkondo wa Nungwi na kusababisha vifo vya watu watanzania wenzetu zaidi ya 200.

Wasiwasi wangu ni huu kuwa, pamoja na kusisitiza umuhimu wa kuangalia na kukagua kila mara vyombo vya usafiri ili kunusuru ajali ambazo zinaweza kuepukika. 


Je wakibainika kwa uzembe huu watachukuliwa hatua za kweli ambazo zitakuwa fundisho kwa wamiliki na watendaji wengine?

Tatizo letu kama taifa siku zote tume zinazoundwa zinaishia kuwa ni viini macho tu na hakuna msukumo wa kweli wa adhabu ambazo zinakidhi haja na haki kwa wafiwa;

Kwa nini meli hiyo ilipakia kupita uwezo wake? Kwa nini captain alikubali kuendelea na safari? Kama yuko hai inapasa awajibishwe kulingana na uzito wa madhara ambayo yametokea  tusimwonee muhari;

Je tunaweza kuthubutu kama serikali ya China inavyothubutu kwa raia wake ambao wanasababisha hasara kwa taifa? Wao hawana mchezo;

Kama tukiweza kuthubutu kwa wavunjaji sheria, uwajibishaji huu tutaweza kuzilinda na kuzitekeleza sheria  na kanuni ambazo zimewekwa kwa ajili ya vyombo vya usafiri ili kudhibiti na kuzuia ajali zisitokee, kwa bahati mbaya sana baadhi ya wamiliki wa vyombo hivyo huacha kufuata kanuni hizo ama kwa makusudi na masilahi binafsi.

Ni kweli kuwa ajali haziepukiki, lakini ajali nyingine husababishwa na uzembe wa wamiliki pamoja nawatendaji wake na hili ndilo lilitokea wiki iliyopita huko Nungwi. 

Natoa wito kwa wadau wote kushikamana katika kuhakikisha vifo vinavyosababishwa na ajali vinapungua kama si kumalizika kabisa kama tukisimama pamoja na kukataa kuburuzwa na wenye mali na kuweza kuwakatalia wengine kupanda kwenye ambacho kimejaa kulingana na uwezo wake tutakuwa tumeweza kuthubutu kwa masilahi ya taifa. 

udhaifu wa usimamiaji wa sheria na muhali umetupa wakati mgumu wa kujua meli hiyo ilikuwa na abiria wangapi? Kwa nini kunakuwa na taarifa ya idadi inayotofautiana? Huu ni uzembe ambao kwa kweli hautakiwi kuendelea kuvumiliwa;

Mwisho tunaiomba Serikali  yetu ambayo ndio muhimili wa maisha bora ya raia wake na usalama wao kuhakikisha inasimamia  utekelezaji wa sheria zake; serikali lazima ithubutu katika  kuwawajibisha wote waliohusika na kuwachukulia adhabu kali na kuacha MUHALI 

Monday, September 12, 2011

SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA AJALI YA MELI ZANZIBAR


Kwa niaba ya Blogu ya Ukadirifu na Mungupamojanasi,  tumopokea kwa mshituko mkubwa sana na kwa majonzi makubwa sana taarifa kufuatia ajali ya kuzama kwa Meli “ MV  Spice Islander” ambayo ilitokea huko Nungwi tarehe 10/09/2011;  ambayo imesababisha vifo vingi vya watanzania wenzetu ambao walikuwa wanasafiri kati ya Dar es salaam, Unguja na Pemba.



Tunatoa salamu zetu za rambirambi kwa wahanga wote wa ajali hii, ambao wamepoteza wapendwa wao, ndugu  na marafiki.

Tunatoa salamu zetu kwa viongozi wetu wakuu wan chi Rais wa Serikali ya Mapinduzi Dr Ali M. Shein, Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete;
Tunatoa shukrani na pongezi za dhati kwa wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika harakati za  kuokoa maisha ya waanga wa ajali hii na vile viele katika shughuli za kuopoa maiti;

Mwenyezi Mungu aendelee kuwapa, nguvu na faraja ndugu zetu ambao wameguswa na msiba huu mkubwa  na katika kipindi hiki chote kigumu ambacho kipo mbele yetu;


Friday, September 2, 2011

KUTHUBUTU KWA VIONGOZI WETU KWA FAIDA YA WANANCHI





Kauli ya Baba Wa Taifa Mwalimu Nyerere "TUMUACHE BADO AKUWE KIDOGO"

Inatufundisha nini katika maendeleo ya taifa hili na viongozi ambao wanashindwa kuchukua uamuzi mara moja?

Ili tuweze kuendelea tunahitaji, pamoja na mambo mengine yote  swala la uongozi bora ni muhimu sana;

Je viongozi wetu wako tayari kutoa maamuzi magumu kwa faida ya watanzania bila woga?

Je Viongozi wetu bado wana Utamaduni wa kuogapa kuwajibika katika utoaji maamuzi kwa ajili ya kikundi fulani cha watu?

Je Viongozi wetu wanaweza kuthubutu wakati wanapo takiwa kuwajibika kufanya mambo kwa kuangalia masilahi watanzania walio wengi hata kama yatawauzi na kuwakwera wachache wenye nguvu kama alivyokuwa akifanya Hayati Edward Moringe Sokoine?

Ni ukweli ambao haupingiki tukiangalia maelekezo ya Wanafalsafa kuwa “kukaa kimya bila kutolea msimamo wako katika jambo fulani maana yake ni kwamba unakubali au unapinga ila unao woga wa uwazi”.  Na kama viongozi wetu wana tabia hii ni kasoro kubwa; kama wahenga walivyotuambia kuwa; “ngoja ngoja huumiza matumbo” tukingoja kufanya maamuzi tunaruhusu mawazo mabaya toka kwa wamanchi wenye hasira pale ambapo kuna kuwa na tatizo. 

Mwalimu J.K.Nyerere aliwahi sema  "Hatuwezi tukawa kweli chama cha watu ikiwa hatujishughulishi na shida za   kawaida za watu wetu".Tujiulize,Je viongozi tulionao ambao hawajishughulishi na shida zetu, wapo kwa ajili ya nani?

Ni ukweli kuwa “Hekima na busara huzaa mafanikio ya uongozi bora, lakini machafuko ni udhaifu wa uongozi”

Mkongwe wa siasa Mahatma Ghandi, aliwahi sema,   “tufikirie kesho lakini tutende kwa ajili ya leo.Hivyo mustakbali wa maisha yetu ya kesho yatategemea maamuzi sahihi ya leo”.
Kama taifa nini tunahitaji?
· vyama vya siasa vyenye nguvu na vyenye kuheshimu demokrasia,
·    Bunge lenye nguvu za hoja lisilitawaliwa na itikadi ya chama chochote! 
·        Viongozi wenye kufikiri kwa faida ya wananchi
·        Viongozi wanaweza kusimamia sheria

Rais Mstaafu awa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa aliwahi kutamka hili kuwa sisi watanzania ni wagumu wa kufikiri;

Swali langu hapa Mheshimiwa Mkapa kama Rais mtaafu nini kilimsukuma yeye kutoa kauli hii?

Je ni ugumu wa kuyakabili matatizo ya maisha au kama ndugu yetu Juvenalis Ngowi alivyowahi andika kuwa “Bahati mbaya ni kwamba inawezekana uvivu wetu huu wa kusoma mambo magumu ndio unatuingiza “mkenge” hata kwenye mambo muhimu ya kitaifa kama mikataba. Inafika mahali tunaingia mikataba ya kusikitisha kiasi cha kujiuliza hivi Mwenyezi Mungu aliwapa watu hao ubongo wa nini? Maana uti wa mgongo pekee ungewatosha watu hao”.

Ndipo tunapoukumbuka wosia wa baba wa taifa’ "TUMUACHE BADO AKUWE KIDOGO" 

Kama wananchi ambao ni sehemu ya kuwachagua hawa viongozi nafikiri inatupasa tuondoe uvivu wetu wa kufikiri, tuamke sasa na tuache itikadi za kuwaacha kuwapa madaraka mtu yeyote ambaye inaonekana wazi kuwa bado hajapata utashi wa kuwa kiongozi bora wa kuwatumikia wananchi wake.

Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema - Ukiweka dodoki kwenye maji safi litanyonya maji safi! Ukiliweka kwenye maji taka, kadhalika litanyonya maji taka! Hapo ndipo tulipo! Uvivu wetu wa kufikiri pengine huleta tatizo hili.

Sisi wadau wa kuwaweka madarakani tukisimamam imara tutawafanya viongozi wetu kuweza kuthubutu au kuchukua maamuzi ambayo watawasaidia na kuwaletea maendeleo ya haraka wananchi na kulinda  mali ya umma kwa nguvu zote, bila kujali kitu chochote. 

 Nafikiri viongozi wetu wa sasa  wanatakiwa kufuata busara na umakini ambao marehemu Sokoine alikuwa nao katika uongozi wake Kwanini, wasikubali kujifunza kwake waone matokeo yake? Kama kuna maamuzi magumu inatakiwa wayafanye; mbona Sokoine alifanya na kuwafanya wahujumu uchumi kuiogopa serikali na kusalimu amri?

Viongozi wetu wanaweza kwani tunaimani kuwa kwa sasa wameshakuwa kifikra na utendaji unaozingatia misingi ya haki na kujali maendeleo ya watanzania wanyonge ndio maana tumewakabidhi nchi;