WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, October 31, 2012

YANGA YASHIKA USUKANI WA LIGI.


YANGA 3 - 0 MGAMBO JKT, SIMBA 1 - 1 POLISI MORO

Kwa matokeo haya Young Africans imeshika usukani wa ligi kwa tofauti ya magoli ya kufunga magoli ya Yanga yamefungwa na 
Cannavaro dkk 2
Didier dkk 39
Tegete dkk 80


Onyo Kali Kwa Watakao Andamana



  
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki akiongea na waandishi wa habari leo Ofisini kwake kuhusu kupinga maandamano wa Waislam yaliyopangwa kufanyika siku ya Ijumaa ya tarehe 02/11/2012 mara baada ya swala

. MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM SAID MECK SADIKI ATOA TAMKO KALI KUHUSU MAANDAMANO YA WAISLAM YALIYOPANGWA KUFANYIKA SIKU YA IJUMAA MARA BAADA YA SWALA.
 Na Adrophina Ndyeikiza-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam 31/11/2012. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki ametoa tamko kali la kuwataka Waislam kuacha mara moja kufanya maandamano yao yaliyopangwa kufanyika siku ya Ijuamaa ya tarehe 02/11/2012 mara baada ya swala ya Ijumaa. Kwa mujibu wa vipeperushi vilivyoandikwa na kusambazwa na Jumuiya na Taasisi za Kiislam (Tz),vimewataka waislam kufanya maandamano makubwa kuelekea katika Ofisi ya Mhe.Waziri Mkuu kwa upande wa Dar es Salaam na Mikoani maandamano hayo yataelekea kwa wakuu wa Mikoa aidha kwa upande wa Zanzibar yataelekea Ofisi ya Makamu wa Rais. Aidha,Sababu ya kuandamana kwao wameelezea kuwa ni kushinikiza Serikali kutenda haki kwa wananchi wote bila ubaguzi kwani waislam wanabaguliwa kwa mambo mengi kama vile;- -Kudhalilishwa Masheikh wao kwa kukamatwa hovyo bila sababu za msingi mfano,Sheikh Ponda na Sheikh Farid wakati wakristo hawafanyiwi hivyo. Akijibu hoja hiyo mbele ya waandishi wa habari Mhe.Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Sheikh Ponda hakukamatwa kama Sheikh Ponda bali amekamatwa kama mtu yeyote yule ambaye anaweza kutuhumiwa kwa kosa fulani.Ameongeza kuwa Serikali haikumkamata Sheikh Ponda kutokana usheikh wake/dini yake au uislamu wake bali kutokana na kutuhumiwa kwake.Hivyo tuache vyombo vya sheria vifanye kazi yake na haki itazingatiwa tu. “Alisisitiza Mkuu wa Mkoa”. -Sababu nyingine ni pamoja na Kudhalilishwa matukufu ya Waislam huku Serikali ikikaa kimya.Akijibu hoja hiyo pia Mhe.Mkuu wa Mkoa amesema kuwa jambo hili si kweli kabisa kwani Serikali ilikwishachukua hatua stahiki kwa kumkamata kijana huyo aliyeyekojolea Koran na kumfikisha katika vyombo vya sheria,hivyo kijana huyo alikwishakamatwa,hata hivyo wale wote waliokwenda kuchoma makanisa,kupiga vioo vya magari ya watu na kuiba vitu mbalimbali katika makanisa na ndani ya magari ya watu nao pia wapo katika mikono ya sheria kwani uislam pia hauagizi hivyo. -Sababu ya tatu ni kuundiwa chombo cha kusimamia Waislam kwa nia ya kuwadhibiti na kulazimishwa Waislam kukitii pamoja na ukweli kwamba kinafisidi Uislam na Wislam.Akijibu hoja hiyo Mhe.Mkuu wa Mkoa amesema kuwa kamwe Serikali haiwezi kufanya hivyo,kwani kila chombo kinaundwa na wanajamii husika na wala Serikali haina dini hivyo haiwezi kuunda chombo chochote kile cha kidini.Hata hivyo zipo taratibu maalumu za namna ya kusajili taasisi yoyote ile kwani lazima kueleza mbele ya msajili ya kuwa taasisi yenu ni ipi na ina malengo gani kwa jamii husika na msajili akilizika na maelezo yenu basi huna budi kuisajili taasisi hiyo.Taasisi yoyote ile lazima isajiliwe na ifuate taratibu za sheria,na Serikali inazisikiliza taasisi zote kama zinafuata sheria na taratibu “Alisisitiza Mkuu wa Mkoa”. Hivyo basi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki amesema kuwa Waislam wote wapenda amani wasifanye maandamano yoyote siku hiyo ya Ijumaa mara baada ya swala kwani kwa kufanya hivyo HATUA KALI ZA KISHERIA DHIDI YA WATAKAOHUSIKA KATIKA KUYAANDAA NA KUSHIRIKI ZITACHUKULIWA kwani maandamano hayo ni BATILI na hayajaruhusiwa na JESHI LA POLISI. Sheria kali zitachukuliwa katika suala hili “Alisisitiza Mkuu wa Mkoa”.

Chanzo cha habari Mjengwa blog

JK Azindua ujenzi Wa Barabara Hai



 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe Novatus Makunga katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo
 Akihutubia
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaidiwa kuzindua jiwe la msingi na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na kupewa shukurani na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Miundombinu Mhe John Pombe Magufuli Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe L:eonidas Gama na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe wakikata utepe mojawapo ya magreda katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Miundombinu Mhe John Pombe Magufuli Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Leonidas Gama na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Kilimanjaro baada ya uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo
  PICHA NA IKULU

Makinda amfagilia Mwakyembe kwa treni ya Dar



"Alihidi kuwa lazima ikifika Oktoba usafiri wa reli ungekuwa tayari na kweli umetimiza hongera sana Waziri na unastahili pongezi kazana na uzi huo, sasa naomba ujibu swali lako.”

SPIKA wa Bunge, Anne Makinda jana alimpongeza Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Harison Mwakyembe kwa kuanzisha usafiri wa treni jijini Dar es Salaam katika kipindi alichoahidi huku akitoa kauli ya alidhani kuwa ni ‘pwagu na pwaguzi’ zilizoashiria kuwa ni vijembe kwa waliotangulia.

“Kwanza kabla ya kujibu swali hilo, mimi nataka nikupongeze sana Waziri kwa kuanzisha usafiri wa treni jijini Dar es Salaam kama ulivyoahidi, mwanzoni mimi nilijua ni yale yale ya ‘pwagu na pwaguzi’ lakini umetimiza, hongera sana Waziri,” alisema Makinda na kuongeza:
“Uliahidi kuwa lazima ikifika Oktoba usafiri wa reli ungekuwa tayari na kweli umetimiza hongera sana Waziri na unastahili pongezi kazana na uzi huo, sasa naomba ujibu swali lako.”

Kauli ya Makinda ilichukuliwa kama kukosoa utendaji kazi wa mawaziri waliowahi kuongoza Wizara hiyo hususan Omar Nundu ambaye awali alitoa kauli katika swali namba 14 ambalo liliulizwa na Nundu kuhusu ujenzi wa reli mpya ya kupitia Kata ya Mabawa na Tangasisi Jiji Tanga.

Nundu alikuwa Waziri wa Uchukuzi kabla ya mabadiliko ya baraza jipya la Mawaziri ambalo lilifanywa na Rais Jakaya Kikwete Mei mwaka huu na Wizara yake kuchukuliwa na Dk Mwakyembe.
Katika swali la msingi Nundu alitaka kujua Serikali inasema nini kuhusu hatma ya wananchi takribani 650 juu ya makazi yao na ulipwaji wa fidia baada ya kuarifiwa kuwa watahamishwa ili kupisha ujenzi wa reli mpya na kwamba tathimini ya fidia yao ilipangwa kufanyika Aprili mwaka huu.

Akijibu swali hilo Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe alisema katika bajeti ya mwaka wa fedha 2012/13, Wizara kupitia Kampuni hodhi ya reli (Rahco) iliwasilishwa na Manispaa ya Tanga na kukubaliana kutenga ekari 150 katika eneo la Mwambani kwa ajili ya kujenga sehemu ya kupangisha mabehewa.

Alisema katika kutekeleza suala hilo, Rahco ilimweka mshauri mwekezaji M/S Majengo Estates Developer Limited kwa ajili ya kufanya tathimini ya fidia kwa wananchi wa maeneo hayo.

Waziri alisema taarifa iliyowasilishwa na Mshauri mwelekezi inaonyesha kwamba gharama za fidia za wakazi wa Magaoni ni Sh 5.3 bilioni.

Alisema hivi sasa nyaraka za fidia zipo Manispaa ya Tanga kwa ajili ya uhakiki wa umiliki wa ardhi na makazi ya wananchi hao katika ngazi ya kijiji, wilaya na mkoa ambao unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi huu.

Source Vijimambo Blog

Mhando Wa TANESCO Afukuzwa Kazi Rasmi




JK Azindua Barabara Ya Rombo- Tarakea



 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaidiwa na Mbunge wa Rombo Mhe Joseph Selasini kukunjua pazia kama ishara ya kufungua rasmi wa barabara ya KM32 kutoka Mkuu Rombo hadi Tarakea leo Oktoba 30, 2012 kijijini Tarakea, wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro ambako Rais Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Mbunge wa Rombo Mhe Joseph Selasini kukunjua pazia kama ishara ya kufungua rasmi wa barabara ya KM32 kutoka Mkuu Rombo hadi Tarakea leo Oktoba 30, 2012 kijijini Tarakea, wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro ambako Rais Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na washika dau wa miundombinu wakikata utepe ishara ya kufungua rasmi wa barabara ya KM32 kutoka Mkuu Rombo hadi Tarakea leo Oktoba 30, 2012 kijijini Tarakea, wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro ambako Rais Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne


 PICHA NA IKULU

Utoro wa wabunge wakwamisha azimio


Ukumbi wa Bunge ukiwa na wabunge wachache jambo lililosababisha kushindwa kupitishwa kwa azimio la bunge la kuridhia marekebisho ya pili ya mkataba wa ushirikiano kati ya Jumuiya ya nchi za Ulaya pamoja na nchi wanachama wa Umoja wa nchi za afrika, Caribbean na Pasifiki, mjini Dodoma, jana. Picha na Edwin Mjwahuzi

Julius Magodi na Hebel Chidawali, Dodoma

UTORO wa baadhi ya wabunge jana ulikwamisha kupitishwa kwa azimio la Marekebisho ya ya Pili ya Mkataba wa Ushirikiano Kati ya Jumuiya ya Nchi za Ulaya na Nchi za Afrika, Caribean na Pacific (ACP).
Hii ni mara ya pili kwa wabunge kukwamisha shughuli za Bunge katika kipindi cha miezi minne kutokana na utoro. Awali, utoro huo ulikwamisha kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Kukwama kwa bajeti hiyo kulikuja wiki moja tu tangu Spika wa Bunge, Anna kukemea tabia ya utoro akisema tabia hiyo ilikuwa imekithiri.
Jana, hali hiyo ilitokea baada ya Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa kuhitimisha kujibu hoja mbalimbali za wabunge waliochangia azimio la mkataba huo aliloliwasilisha baada ya kipindi cha maswali na majibu.
Mara baada ya Waziri Mgimwa kumaliza kujibu hoja ili kutoa nafasi kwa Bunge kupitisha azimio hilo, ndipo Mbunge wa Mkanyangeni (CUF), Mohammed Mnyaa aliposimama na kuomba mwongozo wa Spika kwa kutumia Kanuni ya Bunge, Kifungu cha 68 akitaka Bunge lisipitishe azimio hilo kutokana na idadi ndogo ya wabunge waliokuwa ndani ya ukumbi.
Aliomba Bunge lipange muda mwingine wa kupitisha azimio hilo ili marekebisho yaliyopo katika mkataba huo yapitishwe kwa mujibu wa kanuni.
Spika wa Bunge, Anne Makinda alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kulipitisha azimio hilo hadi leo asubuhi.
Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Kifungu cha 77 (1), akidi kwa kila kikao cha Bunge wakati wa kufanya uamuzi itakuwa ni nusu ya wabunge wote, kama ilivyofafanuliwa katika Ibara ya 94 ya Katiba, isipokuwa kwamba, idadi hiyo haitahusu hoja kuhusu uamuzi wa kubadilisha masharti yoyote ya Katiba kwa mujibu wa Ibara ya 98 ya Katiba.
Wakati Spika akiahirisha Bunge, baadhi ya wabunge walionekana wakiwa nje ya ukumbi wa Bunge huku wengine wakiwa katika mghahawa uliopo katika viwanja hivyo.
Bunge la Tanzania kikatiba, linapaswa kuwa na wabunge 357.
Akichangia azimio hilo Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika aliishauri Serikali kuwa makini na mikataba ya kimataifa huku akitaka mkataba huo wa ACP usaidie kurejeshwa kwa Sh360 bilioni zilizofichwa nchini Uswisi na baadhi ya Watanzania.
Mnyika alisema kifungu cha 29 cha mkataba huo kinataja ushirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwamo kuzuia biashara haramu na rushwa.
Alitaka Serikali itumie kifungu hicho kuomba mabilioni ya fedha yaliyofichwa na baadhi ya Watanzania katika benki mbalimbali huko Uswisi.
Suala hili limeibuka bungeni wakati, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe mwishoni mwa wiki iliyopita alikaririwa akimtuhumu , Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hosea kuwa ameiandikia barua Serikali ya Uswisi akieleza kuwa Serikali ya Tanzania haina maslahi na fedha hizo madai ambayo Dk Hoseah aliyakanusha. Zitto alidai kuwa fedha hizo zimefichwa na vigogo 10.

Mbunge wa Kisarawe (CCM), Seleman Jaffo akichangia azimio hilo, aliitahadharisha Serikali kuwa makini wakati wa kuingia mikataba ya kimataifa akisema mingine inaweza kuwa na matatizo kwa taifa.
Alisema Watanzania wasipokuwa makini katika kuingia mikataba ya kimataifa, wanaweza kujikuta wanaridhia mambo yasiyofaa kwa taifa kama vile kukubali ndoa za jinsia moja.
Awali, akiwasilisha azimio hilo, Dk Mgimwa alisema madhumuni ya mkataba huo ni kujenga ushirikiano imara utakaowezesha kujenga uchumi endelevu ili kupunguza umasikini katika nchi wanachama.

Mafao ya kujitoa
Hatimaye, Serikali imesalimu amri na kukubali yaishe baada ya kufuta tangazo lake la Agosti mwaka huu la kusitishwa kwa fao la kujitoa.
Hata hivyo, habari zilizopatikana zinaeleza kuwa hatua hiyo ya Serikali inatokana na kelele za wabunge na wanaharakati ambao kwa zaidi ya miezi miwili, wamekuwa wakihoji juu ya sheria hiyo.
Suala hilo la fao la kujitoa liliibuka katika kikao cha wabunge wakati wakipewa taarifa ya shughuli za Bunge katika Mkutano huu unaendelea kilichokaa jana mchana katika Ukumbi wa Pius Msekwa.
Habari zilizopatikana kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa Spika Anne Makinda alilitolea ufafanuzi kwa kueleza kuwa Serikali itawasilisha muswada bungeni kufanya marekebisho ya fao hilo.
Jaffo ambaye alikuwa amewasilisha kwa Spika kusudio la kuwasilisha hoja binafsi kupinga kuondolewa kwa fao hilo, alimwambia mwandishi wetu jana kuwa amepokea barua ya kumpa taarifa kuwa Serikali itawasilisha bungeni muswada wa marekebisho.
Alisema marekebisho hayo yataruhusu mifuko yote ya jamii kuendelea kutoa mafao ya kujitoa kama ilivyokuwa awali.
Mbunge huyo alisema amepokea kwa furaha uamuzi huo wa Serikali ili wafanyakazi waendelee kunufaika na mifuko hiyo ya jamii.
“Nashukuru kilio changu kimesikilizwa na Serikali kwangu mimi huu ni ushindi, kwani wafanyakazi wengi nchini hawana kazi za uhakika,” alisema
Alisema wafanyakazi wengi hususan wa sekta ya madini, hawana uhakika wa ajira hivyo kuondolewa kwa fao la kujitoa kungewapa wakati mgumu.
Mnyika pia alikuwa amewasilisha kusudio la kuwasilisha hoja binafsi ya kupinga fao la kujitoa kuondolewa katika bunge hili.
Katika Mkutano wa Nane wa Bunge, Jaffo alipinga sheria hiyo ya kufuta fao la kujitoa alipoomba mwongozo wa Spika na mara baada ya kuwasilisha hoja zake, aliungwa mkono na wabunge wengi isipokuwa Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola ambaye alisimama na kutetea sheria hiyo.

Mwananchi

WATU WALIOPIGWA NA POLISI


 Salum Bakari Muya alidai aliteswa kwa kukatwa ngozi kwa kisu kichwani na kasha kunyonyolewa nywele

Na Salma Said.
Polisi wadaiwa kumtesa mbeba mizigo Zanzibar.
MTU moja makazi wa Mkele jana alinusurika kuuawa katika msako wa kuwakamata watu wanaotuhumiwa kusababisha vurugu zilizotokea wiki moja iliyopita mjini Zanzibar.

Vurugu hizo ziliibuka Oktoba 17 mwaka huu baada ya kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMUIKI) Sheikh Farid Ahmed Hadi kutoweka katika mazingira ya kutatanisha Oktoba 16, mwaka huu.Akizungumza na waandishi wa bahari mjini hapa jana, kijana aliyenusurika kuuawa, Salum Bakari Muya alidai aliteswa kwa kukatwa ngozi kwa kisu kichwani na kasha kunyonyolewa nywele polisi ambao pia walikuwa na silaha.

Alisema kabla ya kukutwa na tukio hilo alikuwa amekaa na wenzake wakiwa wanasubiri tenda ya mizigo ya kusafirisha kwa kutumia magari ya punda.

“Nilikuwa nabangaya – yaani kubangaiza –wakatokea polisi sita, walipofika nilipokaa wakanifunua kofia na kunikata kipande cha ngozi na nywele kichwani kwa kisu,” alisema Salum.  Alidai polisi waliomfanyia ukatili huo ni wa kikosi cha FFU na kwamba baada ya kitendo hicho waliamua kumpeleka kituo cha afya cha JKU kilichopoa Saateni kwa matibabu ya awali.

Salum alidai kuwa baada ya kupata matibabu katika kituo hicho cha JKU iliamriwa kwamba apelekwe Hospitali Kuu ya Mnazimoja kwa vile alikuwa anavuja damu nyingi. Hata hivyo alisema alishangaa kabla ya kufika Mnazimoja polisi hao waliamua kumtekeleza katika eneo la kwa Abbas Hussein, kilometa chache kutoka walipomtoa hospitali ya JKU.

“Hawakunifikisha Manazimoja, wakaniacha na kuondoka huku wakisema ubaya ubaya mtakoma waambie na wenzio,” alisimulia Salum akiwa na bandeji aliyofungwa wakati anapata huduma ya kwanza. Alisema baada ya kutelekezwa na polisi aliamua kwenda Welesi huko Kikwajini kwa lengo la kuzungumza na waandishi wa habari juu ya mkasa uliompata.

Baada ya kusimulia mkasa huo, Salum ambaye alifuatana na kaka zake walioomba wasiandikwe majina baadae alipelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi. Alipoulizwa juu ya tukio hilo, Kamishana wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema bado hajapopewa taarifa na kwamba iwapo mwathirika atalalamika kituoni polisi watachukua hatua ya kucunguza.

“Tumezoea kulalamikiwa, kama mtu amefanyiwa ukatili kwanini asiripoti kituo cha polisi, hapo ujue kuna jambo anaficha,” alisema Kamishna Mussa. Lakini baada ya kuelezwa na mwamdishi wa habari hizi kwamba kijana huyo amepelekwa hospitali na kaka zake, Mussa alisema aliahidi kufuatilia tukio hilo.

Kitendo cha Salum kufanyiwa ukatili na watu wanaodaiwa kuwa polisi kimetanguliwa na matukio ya vijana wenguine wawili kuuawa wakati wa utekelezaji wa zoezi la msako huo mjini Zanzibar mwezi Oktoba mwaka huu. Imedaiwa kuwa Hamad Ali Kaimu aliuawa Ijumaa iliyopita wakati akiwa mikononi kuwa polisi katika eneo la Magomeni,  na Salum Hassan Mahanju alikufa baada ya kupigwa risasi katika maeneo ya Amani Fresh na watu waliotajwa kuwa maofisa ulinzi na usalama.

Mbali na vijana hao, askari mmoja Koplo Said Abdulrahman aliuawa na watu wasiojulikana huko Bububu baada ya tukio la kutoweka Sheikh Farid

source Vijimambo blog

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO MKUU WA NANE WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM-TAIFA, MJINI DODOMA LEO




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Chuo cha Mipango, mjini Dodoma leo Oktoba 31, 2012 kwa ajili ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa Nane wa Jumuiya ya Wazazi CCM-Taifa. Mkutano huo unafanyika sambamba na uchaguzi wa Viongozi wapya wa Jumuiya hiyo.

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nane wa Jumuiya ya Wazazi CCM-Taifa. Mkutano huo unafanyika sambamba na uchaguzi wa Viongozi wapya wa Jumuiya hiyo, katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Chuo cha Mipango, mjini Dodoma leo Oktoba 31, 2012.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wajumbe wa mkutano huo baada ya ufunguzi uliofanyika leo, mjini Dodoma.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na William Malecela, wakati akiondoka kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Chuo cha Mipango, mjini Dodoma leo Oktoba 31, 2012 baada ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa Nane wa Jumuiya ya Wazazi CCM-Taifa. Mkutano huo unafanyika sambamba na uchaguzi wa Viongozi wapya wa Jumuiya hiyo. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

source Haki Ngowi blog

Tuma Maoni kuhusu Mabadiliko ya Katiba kwa simu ‘SMS’


31/10/2012


Taarifa hii imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya ZanziNews

Tume ya Mabadiliko ya Katiba imetangaza namba nne (04) za simu za mkononi ambazo wananchi kwa sasa wanaweza kuzitumia kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (‘sms’) kutoa maoni yao kuhusu Katiba Mpya.

Kwa mujibu wa taarifa ya Tume hiyo kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo (Jumatano, Oktoba 31, 2012) namba ambazo wananchi wanaweza kutuma maoni yao kwa njia ya ‘sms’ ni 0715 (Tigo) /0767 (Vodacom) / 0787 (Airtel) / 0774 (Zantel) – 08 15 08.

“Kwa kuzingatia kuwa Watanzania wengi waliopo mijini na vijijini wanamiliki simu za mkononi, Tume ya Mabadiliko ya Katiba inaamini kuwa njia hii ni fursa nyingine muhimu kwa Watanzania kuweza kuwasilisha maoni yao kwa Tume,” imesema sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa na Katibu wa Tume hiyo Bw. Assaa Rashid.

Ili kutuma maoni, Bw. Assaa amesema, mwananchi anapaswa kufungua ukurasa wa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (sms) katika simu yake na kuandika maoni yake pamoja na jina lake kamili, jinsia, mahali anapoishi, umri, elimu na kazi na kutuma kwenda kwenye namba yoyote kati ya zilizotolewa.

Kwa mujibu wa Bw. Assaa, baada ya kutumwa, maoni hayo yatakwenda kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambapo yatafanyiwa kazi pamoja na maoni yanayokusanywa kwa njia nyingine.

Uanzishwaji wa njia hii ya ujumbe mfupi wa maandishi unalenga kuwapa fursa nyingine wananchi kutoa maoni yao. Tume ya Mabadiliko ya Katiba pia inapokea maoni ya wananchi kupitia mikutano ya ana kwa ana; barua pepe (maoni@katiba.go.tz); njia za posta (S.L.P. 1681, Dar es Salaam au S.L.P. 2775, Zanzibar); ukurasa wa ‘facebook’ (Tume ya Mabadiliko ya Katiba) na tovuti (katiba.go.tz).

Katika taarifa yake hiyo, Tume imewaomba wananchi kutumia namba hizo kutuma maoni yao binafsi kuhusu Katiba Mpya bila kushawishiwa na watu, makundi, vyama au taasisi yoyote na kufafanua kuwa Tume inatarajia kuanza kupokea maoni ya makundi, vyama na taasisi mara baada ya kumaliza kukusanya maoni binafsi ya wananchi katika awamu ya nne na ya mwisho itakayomalizika mwezi Desemba, 2012.


Source: 
http://www.wavuti.com

Dkt Shein Afanya Uteuzi




NA MAELEZO ZANZIBAR 31/10/2012 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amemteua Amina Juma Zidikheir kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utumishi wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar. Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Dkt Abdulhamid Yahya Mzee imesema kuwa uteuzi huo ameufanya kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 8(1) (a) cha sheria ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar namba 11 ya mwaka 2003. Amina Juma Zidikheri aliwahi kuwa Mhasibu mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kabala ya kustaafu kwake. Uteuzi huo umeanza tarehe 27 Oktoba,2012 

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 31/10/2012

Viongozi Wa Dini Waiunga Mkono Serikali


 

 
Viongozi wa kikristo wakiongoza maombi mbele ya kanisa la KKKT Mbagala siku moja baada ya kushambuliwa na kuharibiwa.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 Viongozi wa dini waiunga mkono Serikali kuhusu udini VIONGOZI wa dini zote katika Mkoa wa Kilimanjaro wameungana kuunga mkono jitihada za Serikali kupambana na wanaharakati wa kidini ambao wanatumia dini kucheza siasa kwa nia ya kuvuruga amani ya utulivu ambao umedumu nchini kwa miaka mingi. Miongoni mwa mambo mengine, viongozi hao wameitaka Serikali kuangalia upya sera ya usajili wa taasisi za kidini nchini kwa nia ya kupunguza na hata kumaliza joto la uvunjivu wa amani kwa kutumia mgongo wa dini. Aidha, viongozi hao wameishauri Serikali kuchukua hatua kali za kupambana na vitendo vya uvunjifu wa amani na utulivu kupitia kisingizio cha dini ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya watu wanaotumia mwanya wa dini kuingiza siasa katika dini na hivyo kuvunja amani. Msimamo huo wa viongozi wa dini umeelezwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa jana, Jumanne, Oktoba 30, 2012, wakati alipokutana na viongozi hao ambao wamewasilisha matamko yao kwake katika shughuli fupi iliyofanyika Ikulu Ndogo ya Mkoa wa Kilimanjaro mjini Moshi. Matamko hayo yanahusu vurugu za karibuni katika Jiji la Dar es Salaam ambazo zilihusisha uvunjifu wa amani. Viongozi hao wakiongozwa na viongozi wao – Mwenyekiti wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Kilimanjaro Sheikh Ramadhan Salim, Sheikh wa Mkoa wa Kilimanjaro Sheikh Shaaban Rashid na maaskofu Glorius Shoo, Martin Shao na Isaac Amani wakiwasilisha madhehebu ya Kikristo ya Wakatoliki, KKKT, Pentecoste na TAG na imani mbali mbali za dini ya Kiislamu walifika Ikulu Ndogo kuwasilisha salamu kwa Rais Kikwete. Ujumbe wa viongozi hao ulifanana kabisa. Wote walilaani kudhalilishwa kwa Kitabu Kitakatifu cha Quran kwa kukojolewa na kijana mmoja, kitendo ambacho kilisababisha kuvamiwa na kuchomwa kwa makanisa ya Kikristo na kuibiwa kwa mali kutoka kwenye makanisa hayo. Baba Askofu Martin Shao amemwambia Rais Kikwete: “Mheshimiwa Rais tumekuja kukusalimia na kutoa tamko letu la kuunga mkono jitihada za Serikali yako katika kukabiliana na uvunjifu wa amani kwa kisingizio cha dini kama ilivyodhihirika katika siku chache zilizopita.” Naye Sheikh Shaaban Rashid amemwambia Rais Kikwete: “Hatukubaliani na mambo mawili, moja ni kunajisiwa kwa Kitabu Kitakatifu cha Mwenyezi Mungu cha Quran na pili ni kuvunjwa na kuharibiwa kwa Nyumba za Ibada kama ilivyoonyeshwa katika matukio ya Mbagala kule Dar es Salaam. Tunaunga msimamo wa Serikali yako katika kukabiliana na mambo haya.” Naye Mwenyekiti wa Bakwata katika Mkoa wa Kilimanjaro, Sheikh Ramadhan Salim amemwambia Rais Kikwete: “Tumefadhaishwa na kitendo cha kunajisiwa Kitabu cha Mungu – imepata kutokea pale Dodoma, imepata kutokea Boma Ng’ombe Mkoa wa Kilimanjaro na sasa Mbagala, Dar es Salaam. Tunalaani pia vitendo vya kuvunja, kuharibu na kuchoma moto nyumba za ibada.” Ameongeza: “Tunaomba Serikali kuchukua hatua tatu. Moja ni kuhakikisha kuwa hukumu ya uadilifu inafikiwa katika kesi zinazowakabili waliohusika na vitendo hivi. Pili Serikali iangalie upya sera za uandikishaji wa taasisi za kidini na tatu Serikali itoe msimamo kamili na sahihi kuhusu jambo hili badala ya taarifa za matukio haya kutolewa na vyombo vya habari.” Naye Askofu Martin Fataely Shao amesema: “Tunasikitishwa na vitendo na matukio ya uvunjifu wa amani, utulivu na mshikamano. Tunasikitishwa na kuibuka kwa vikundi vinavyodhalilisha dini na imani ya watu wengine kwa kutumia vyombo vya habari na hasa redio. Hatukubaliani na vitendo vya kukashifu dini na imani za watu wengine.” Akizungumza katika shughuli hiyo kwenye siku ya tatu ya ziara yake ya siku nne katika Mkoa wa Kilimanjaro, Rais amewashukuru sana viongozi hao wa dini. “Leo nitalala usingizi mzuri kwa kuwa mmetoa maneno ya kuponya nchi yetu. Nawapongezeni kwa uamuzi wa kukutana na kufikia uamuzi huu.” Rais Kikwete amesema kuwa kwa muda sasa amekuwa anaona dalili za Tanzania kupelekwa pabaya siyo kwa tatizo la ukabila bali kwa tatizo la udini kwa sababu ni dhahiri kuna watu hawafurahishwi na utulivu wa Tanzania na wangependa kuiona Tanzania ikikumbwa na matatizo ya ukosefu wa amani na utulivu kama baadhi ya nchi majirani. Amesema kuwa ni dhahiri wako wanarahakati wa dini zote kubwa mbili ambao wanatumia dini kujipenyeza katika ajenda za kisiasa na hivyo kuvuruga amani na utulivu. “kazi ya wanaharakati hawa ni kukashifu dini za wenzao. Uzuri sheria za nchi hii zinatosha kukabiliana na hali hii. Tunatoa uhuru wa watu kuabudu lakini hatutoi uhuru wa watu kudhalilisha dini za watu wengine.” Rais Kikwete amewahakikishia viongozi hao wa dini kuwa Serikali yake haitalala katika kuhakikisha kuwa Tanzania haiingii katika uvunjifu wa amani na utulivu kwa kisingizio cha dini.“Nataka kuwahakikishia kuwa Serikali yenu iko macho. Kamwe, hatutaruhusu uvunjifu wa amani kwa kisingizio cha dini. Nyie mmeonyesha mfano. Na sisi hatuwezi kuiachia nchi kutumbukia katika matatizo.”

source Mjengwa blog

Taarifa ya TFDA ya ufafanuzi wa taarifa mbalimbali kuhusu ARVs bandia


Picture

Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Mr. Hiiti Sillo akionesha waandishi fomu ya kukusanyia madhara ya dawa (picha: Jiachie blog)
1.0        UTANGULIZI

a).    Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ni Wakala wa Serikali chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii yenye jukumu la kudhibiti usalama, ubora na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba ili kulinda afya ya jamii. TFDA imeweka mifumo mbalimbali ya udhibiti chini ya sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sura 219. Mifumo hiyo ni pamoja na usajili wa bidhaa, usajili wa majengo/maeneo ya kuzalisha na kuuza bidhaa, uchunguzi wa kimaabara wa sampuli za bidhaa pamoja na ukaguzi na ufuatiliaji wake kwenye soko.

b).    Kupitia mifumo iliyowekwa, TFDA imekuwa ikihakikisha usalama, ubora na ufanisi wa dawa katika soko. Aidha, mifumo hiyo pia huwezesha kubaini uwepo wa bidhaa bandia na duni kwenye soko na kuchukua hatua mbalimbali kwa mujibu wa Sheria. Hatua hizo ni pamoja na kusitisha matumizi ya bidhaa husika na kuziondoa kwenye soko, kuziteketeza na kuwafikisha watuhumiwa kwenye vyombo vya dola na sheria.

c).  Itakumbukwa kwamba, mnamo tarehe 21 Septemba 2012, tarehe 4 Oktoba, 2012 na tarehe 10 Oktoba 2012,  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii  ilitoa taarifa kwa umma juu ya uwepo wa dawa bandia ya kupunguza makali ya UKIMWI yenye jina la kibiashara ‘TT-VIR 30’ toleo Na. 0C.01.85 ikiwa ni pamoja na hatua zilizochukuliwa. Baada ya taarifa hizi za Wizara kutolewa, kumekuwa na taarifa mbalimbali kupitia vyombo vya habari zinazoleta mkanganyiko kwa wananchi kuhusu suala hili.

d). Baadhi ya mikanganyiko hiyo ni pamoja na jinsi dawa hiyo bandia ilivyobainika, kama barua za TFDA ziliwafikia Tanzania Pharmaceuticals Industries (TPI) Ltd na kama uzalishaji wa dawa bado unaendelea au la.

e).    Ili kuondoa mkanganyiko ambao umeanza kujitokeza, Mamlaka inapenda kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu dawa hizo bandia ambazo matumizi yake yamesitishwa. Vilevile,  TFDA inapenda kutumia fursa hii kutoa ufafanuzi kuhusu mfumo wa udhibiti wa dawa nchini.

2.0     UFAFANUZI KUHUSU DAWA BANDIA YA TT-VIR 30
  • TFDA ndiyo iliyobaini uwepo wa dawa bandia aina ya TT-VIR 30 toleo Na. 0C.01.85 kwenye soko mnamo tarehe 28 Julai, 2012 kupitia mfumo wake wa ukaguzi na ufuatiliaji wa bidhaa katika soko. 
  • Kama ilivyoelezwa katika taarifa zilizotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, TFDA inasisitiza kwamba kampuni ya TPI Ltd iliiuzia MSD dawa bandia aina ya TT-VIR 30 toleo Na. 0C.01.85, kwa mujibu wa nyaraka zilizopo.
  • Nyaraka hizo pamoja na vielelezo mbalimbali zimewasilishwa kwenye vyombo vya usalama kwa hatua zaidi za kisheria.
  • TFDA imesitisha uzalishaji wa dawa za ARVs za kiwanda cha TPI Ltd kupitia barua Kumb. Na. CA/C.80/222/01A/47 ya tarehe 4 Oktoba, 2012 na vile vile uzalishaji na usambazaji wa dawa zote kupitia barua Kumb. Na. CA/C.80/222/01A/55 ya tarehe 10 Oktoba, 2012.
  • Barua hizo zilipelekwa kwa ‘dispatch’ katika ofisi za Makao Makuu ya Kampuni ya TPI Ltd iliyoko eneo la Mikocheni, Dar es Salaam na kupokelewa tarehe 04 na 10 Oktoba, 2012.
  • Taarifa zilizotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii zilionesha wazi kwamba TFDA ndiyo iliyositisha uzalishaji wa dawa katika kiwanda cha TPI Ltd.
  • Ukaguzi uliofanywa na TFDA kwenye kiwanda cha TPI Ltd, Arusha tarehe 12 na 23 Oktoba 2012, umethibitisha kwamba hakuna uzalishaji wa dawa unaoendelea kwenye kiwanda husika kama ilivyoelekezwa na TFDA.
3.0        MFUMO WA UDHIBITI WA DAWA NCHINI

Aidha, Mamlaka inapenda kutumia fursa hii kufafanua zaidi kuhusu mfumo wa udhibiti wa dawa nchini kama ifuatavyo;

a).    Udhibiti wa dawa unazingatia Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sura 219, kanuni zilizowekwa, miongozo, misingi ya kisayansi (science based) pamoja na miundombinu kama vile maabara na mtandao wa ukaguzi. Mifumo ya udhibiti hujumuisha yafuatayo;-

 i.        Kufanya tathmini ya taarifa za kisayansi kuhusu ubora, usalama na ufanisi wa dawa, kufanya ukaguzi wa viwanda na hatimaye kusajili dawa husika.
ii.        Kusajili maeneo yanayojishughulisha na uzalishaji na biashara ya dawa ikiwepo masharti ya kuwa na wataalam wa kusimamia uzalishaji.
iii.        Kufanya ukaguzi wa maeneo yanayotengeneza dawa, vituo vya forodha pamona na maeneo ya kusambaza na kuuza dawa.
iv.        Kufanya ufuatiliaji wa ubora, usalama na ufanisi wa dawa zilizosajiliwa kwa lengo la kuhakikisha kwamba zinakidhi vigezo na matakwa ya usajili.
v.        Kufanya uchunguzi wa kimaabara ili kuhakiki usalama na ubora wa dawa zinazoombewa usajili na zile zilizoruhusiwa kutumika nchini.


b).    Katika kutekeleza mifumo ya udhibiti na kwa kuzingatia misingi ya udhibiti wa bidhaa duniani, mwenye jukumu la kwanza la kuhakikisha usalama, ubora na ufanisi wa bidhaa ni la aliyeisajili bidhaa (marketing authorization holder) ili kuhakikisha kuwa mtumiaji hapati madhara.

c).    Mifumo hii ndiyo inayoiwezesha TFDA kuhakikisha usalama, ubora na ufanisi wa dawa na pia kubaini dawa bandia na duni katika soko na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria.

4.0        HITIMISHO

a).    Uchunguzi zaidi wa dawa bandia aina ya TT-VIR 30 toleo Na. 0C.01.85 unaendelea kupitia vyombo vya usalama kwa hatua zaidi za kisheria.

b).    TFDA itaendelea kufuatilia usalama, ubora na ufanisi wa dawa kwenye soko kupitia mifumo iliyowekwa ili kulinda na kudumisha afya ya jamii;

c).    Tunapenda kuwakumbusha wote wanaojihusisha na biashara ya dawa, chakula, vipodozi na vifaa tiba kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo iliyowekwa na kwamba yeyote atakayekiuka taratibu hizo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

d).    Tunawahakikishia wananchi kwamba dawa za ARVs zilizoko katika vituo vya kutolea huduma za afya ni salama na hivyo waendelee kuzitumia bila wasiwasi wowote.

e).    Tunatoa rai kwa vyombo vya habari, watoa huduma za afya na wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa pale wanapobaini au kuhisi kuwepo kwa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba vyenye mashaka au uvunjifu wa Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sura 219.

Hiiti B. Sillo
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA
30 OKTOBA, 2012


-----
wavuti.com imenukuu taarifa hii kutoka Jiachie blog
Picture
Waandishi aw habari wakisikiliza Ufafanuzi juu ya dawa ya ARV bandia. (picha: Jiachie blog)


Source: http://www.wavuti.com

Tuesday, October 30, 2012

MAMA PINDA AWAAMBIA VIJANA UJASIRIAMALI NI AJIRA RASMI INAYOTAMBULIKA DUNIANI


Mke wa Waziri Mkuu Mana Tunu Pinda akitoa hotuba ya kufungua Maonyesho ya Wanawake Wajasiriamali (MOWE) katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam ambapo amewahimiza wajasiriamali kujiunga katika ushirika ili iwe rahisi kusaidiwa kupata mikopo, kutafuta masoko, kupanga bei nzuri ya bidhaa zetu, kupata utaalam na teknolojia mpya. Kauli Mbiu ya ya Maonyesho hayo mwaka huu ni “Msichana Amka, Ujasiriamali ni Ajira”.
Mama Tunu Pinda akikata utepe kuzindua Mradi wa Uwezeshaji Kiuchumi wa Maendeleo ya Wanawake Wajasiriamali (WEDEE) Ulio chini ya Shirika la Kazi Duniani (WEDEE) wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Wanawake wajasiriamali ya MOWE yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mama Pinda akipokea vitabu toka kwa Noreen Toroka (wa pili kulia) na Hopolang Phororo wa ILO.
Mama Tunu Pinda akisoma kwa furaha kitini cha mafunzo ya Wajasiriamali baada ya kufungua Maonyesho ya Wanawake Wajasiriamali (MOWE) katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Bi. Hopolang Phororo na Noreen Toroka kutoka ILO.
Pichani Juu na Chini ni Mama Tunu Pinda akikagua baadhi ya mabanda na kujionea bidhaa mbalimbali katika maonyesho hayo.
Mama Tunu Pinda akipokea kipeperushi kutoka kwa Noreen Toroka wa ILO walioandaa maonyesho ya MOWE kwa kushirikiana na Taasisi ya Wanawake na Maendele0 (WAMA) iliyochini ya Mama Salma Kikwete.
Mama Tunu Pinda (katikati) katika picha ya pamoja baada ya kufungua maonyesho ya MOWE 2012.

source; Vijimambo blog

Naridhishwa na Kazi ya Tume ya Katiba - Rais Kikwete




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa anaridhishwa na mwenendo mzima wa kazi ya Tume ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya Wananchi Kuhusu Katiba.

Aidha, Rais Kikwete amewataka wajumbe wa Tume hiyo kuwakumbusha wananchi kutokutoa maoni kwa kutumwa na watu wengine bali watoe maoni yao wenyewe kwa kadri wanavyotaka Katiba yao mpya iwe.

Rais Kikwete ameyasema hayo leo, Jumanne, Oktoba 30, 2012, kwenye Ikulu Ndogo mjini Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro wakati alipokutana na kuzungumza kwa muda mfupi na baadhi ya wajumbe wa Tume hiyo wakiongozwa na Profesa Baregu Mwesiga ambao walikwenda kumjulia hali Rais. Rais Kikwete yuko katika ziara ya siku tatu katika Mkoa wa Kilimanjaro.

Wajumbe hao wanne ambao walikutana na Rais Kikwete ni sehemu ya wajumbe wa Tume ambao wako mkoani Kilimanjaro kukusanya na kuratibu maoni ya wananchi wa mkoa huo kuhusu Katiba. Watakuwa Kilimanjaro hadi tarehe 6 Novemba, 2012.

Rais Kikwete amewaambia wajumbe hao: “ Kwa maoni yangu nadhani kazi ya Tume inakwenda vizuri na mimi nawatakia kila heri katika shughuli hii muhimu kwa mustakabali wa taifa letu. Zitakuwepo changamoto, lakini hizo hazikosi katika shughuli yoyote ya binadamu.”

Aliongeza Rais Kikwete: “Nawaomba tu muendelee kuwaelimisha wananchi kuwa ni vizuri kwao kutoa maoni yao wenyewe siyo kwa kutumwa na watu wengine. Wahasishwe wasiwe kaseti za kucheza maoni ya watu wengine.”

Profesa Baregu amemwambia Rais Kikwete kuwa kazi ya Tume hiyo inakwenda vizuri na wajumbe wa Tume wanayo matumaini makubwa kuwa kazi hiyo itakamilishwa katika kipindi kilichokubaliwa. “Tunaweza kusema kuwa tunakaribia kumaliza robo tatu ya kazi ya kukusanya maoni ya wananchi.”

Profesa pia amemwambia Rais Kikwete kuwa ni kweli wajumbe wa Tume hiyo wanakumbana na watu ambao wanatumika kama kaseti za watu wengine. “Ni kweli wapo. Mwanzoni walikuwa wengi lakini sasa tunaona kuwa wanaanza kupungua.”

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
30 Oktoba, 2012


Source: http://www.wavuti.com

Maalim Seif ashauri kupatiwa taaluma kwa vikosi vya serikali ya mapinduzi kukabiliana na vurugu


Tuesday, October 30, 2012
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Ofisini Kwake Migombani Zanzibar. Kushoto ni kiongozi wa ujumbe huo Bw. Akinyemi Adegbola.


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiagana na kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa Bw. Akinyemi Adegbola baada ya mazungumzo yao huko Ofisini Kwake Migombani Zanzibar. Kushoto ni Mjumbe wa Umoja huo ofisi ya Zanzibar bibi Njeri Kamau.(Picha, Salmin Said, OMKR).
 Na Hassan Hamad OMKR

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema vikosi vya ulinzi vya Tanzania na vile vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar vinahitaji kupatiwa mafunzo ya ziada juu ya kukabiliana na vitendo vya vurugu na kulinda amani ya nchi.

Amesema vikosi hivyo vimekuwa vikitumia nguvu za ziada katika kukabiliana na vitendo hivyo, hali inayopelekea kuleta madhara kwa raia wasiokuwa na hatia pamoja na mali zao.

Maalim Seif ametoa kauli hiyo ofisini kwake Migombani Mjini Zanzibar alipokuwa na mazungumzo na ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliofika kwa ajili ya kubadilishana mawazo.