Tuesday, October 30, 2012
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif
Sharif Hamad akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na ujumbe wa Umoja wa
Mataifa huko Ofisini Kwake Migombani Zanzibar. Kushoto ni kiongozi wa ujumbe
huo Bw. Akinyemi Adegbola.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif
Hamad akiagana na kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa Bw. Akinyemi
Adegbola baada ya mazungumzo yao huko Ofisini Kwake Migombani Zanzibar. Kushoto
ni Mjumbe wa Umoja huo ofisi ya Zanzibar bibi Njeri Kamau.(Picha, Salmin Said,
OMKR).
Na Hassan Hamad OMKR
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif
Hamad amesema vikosi vya ulinzi vya Tanzania na vile vya Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar vinahitaji kupatiwa mafunzo ya ziada juu ya kukabiliana na vitendo
vya vurugu na kulinda amani ya nchi.
Amesema vikosi hivyo vimekuwa vikitumia nguvu za ziada
katika kukabiliana na vitendo hivyo, hali inayopelekea kuleta madhara kwa raia
wasiokuwa na hatia pamoja na mali zao.
Maalim Seif ametoa kauli hiyo ofisini kwake Migombani Mjini
Zanzibar alipokuwa na mazungumzo na ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliofika kwa
ajili ya kubadilishana mawazo.
No comments:
Post a Comment