WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, October 20, 2012

Vipeperushi vya vitisho kwa Wakristo, Viongozi vyasambazwa Zanzibar


20/10/2012

 Habari hii imenukuliwa kutoka ZanziNews blog

Vipeperushi vinavyotishia uhai wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar vimepeperushwa mjini hapa kufuatia ghasia zinazoendelea kwa siku ya tatu mfululizo.

Kipeperushi kimojawapo kinasema: “CCM kosa letu kuwatia mbwa msikitini. Sasa tunasema kuwa basi tena litakalokuwa na liwe kwa sisi CCM basi tena umoja na CUF. Nyie CUF/Muamsho Abubakari Khamis Bakar (Waziri wa Katiba), Mussa (Kamishna wa Polisi) na Azizi (Kamanda wa Polisi Mkoa) mmeshazoea fujo na sisi sera yetu CCM sera yetu amani sasa mujiuzulu mumpishe Rais afanye kazi zake, Tumechoka na nyinyi juu ya mauaji ya askari wetu. Ondokeni murudi kwenu.  Wewe Abubakar hukuanza leo na jana ufisadi kazi ya ufisadi umeizoweya hadi ulifungwa jela na mafisadi wenzako, mwishowe huku SMZ kumekuokoa.”

Wakati huo huo kuna waraka umesambazwa ambao umewatisha hofu waumini wa dini ya Kikristo nchini ukisema wote watakatwa vichwa. Waraka huo ambao unasemekana umetolewa na watu wenye kujiita jumuiya ya Uamsho umeandikwa na kusambazwa katika maeneo mbalimbali huku wenyewe wakristo wakipelekewa maofisini kwao.

Akizungumza na masikitiko, Askofu wa Kanisa la Anglikan Mkunazini, Emmanuel Masoud amesema ni wakara ambao umewastusha Wakristo kutokana na maneno mazito yalioandikwa humo ambapo ndani ya wakara huo, “Maneno yaliandikwa humu yametushitua sana sisi waumini wa dini ya Kikristo hapa Zanzibar. Kwa kwa kweli sio jambo la kupuuzia ikiwa wanasema watatukata vichwa ni jambo la hatari kabisa” alisema Masoud.
Wakizungumzia ukweli juu ya suala hilo, Sheikh Azzan amesema Jumuiya yake haihusiki na waraka wa aina hiyo na wao kamaWwaislamu hawana sababu ya kuwatisha watu kwa kuwa wanaamini Uislamu sio dini ya kuwabagua watu wala kuwatisha watu.
Azzan alisema wapo baadhi ya watu ambao wanatumia propaganda mbaya za kutaka kuwagawa Wazanzibari katika kipindi hiki na ndiyo wanatumia kila sababu za kuwagawanya. Aliwatahadharisha wananchi kuepukana na propaganda kama hizo kwani zinaweza kuitia nchi katika pahala pabaya na kutoweka kwa amani.
“Sisi hatuhusiki na waraka huo aliyetoa waraka huo ni watu ambao wanapingana na amani iliyopo lakini pia ni watu wenye kueneza propaganda mbaya za kutaka kuwagawa Wazanzibari, jambo ambalo sisi tunaamini hatuna ugomvi, na Wazanzibari wote sisi ni ndugu, hatubagui awe ni Mkristo au Muislam, awe mweupe au mweusi, hatuwezi kubaguana kwa kuwa misingi ya dini yetu imekataza kubaguana” alisema Azzan.


Source: http://www.wavuti.

No comments:

Post a Comment