WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, October 28, 2011

JE UVUMILIVU NI KARAMA AU MAZOEA


UVUMILIVU HUJENGWA NA MISINGI GANI?



Naanza kwa kujiuliza kuwa “tulichonacho sisi wananchi je ni subira?; na baadhi ya viongozi wetu je wanao uvumilivu?  

Kwa haraka haraka tu Uvumilivu ni uwezo wa, au ni mazoezi ya, kutambua na kuheshimu imani au matendo ya wengine; uvumilivu uko katika kila nyanya ya maisha yetu, kuanzia maisha yetu ya kila siku;TATIZO katika maisha ya kawaida sana, swala la uvumilivu halizungumzwi sana, kwani uvumilivu unahusishwa na familia au kikundi kidogo cha watu; katika level hii uvumilivu huzungumzwa sana katika kuimarisha  maisha ya ndoa;


Uvumilivu huongelewa sana kwa mapana hasa katika maswala ya uongozi, uongozi ni hali ya kuongoza nchi katika mwelekeo wa kuleta maendeleo na ni ukweli kama mwandishi mmoja alipowahi sema kuwa “ KUONGOZA watu na hasa wa watu wazima ni kazi nzito inayohitaji mtu anayepewa jukumu hilo kuwa makini, vinginevyo mambo yanaweza kuwa magumu na hatimaye kuangukia katika mtego wa udikteta.  Hii inatokana na kukosekana mambo makubwa matatu ambayo ni ufahamu au maarifa, hekima na  hasa uvumilivu. Kiongozi asiye mvumilivu anaweza kujikuta anatumia mabavu kutawala ili watu wajue kuwa yupo, ana nguvu na ana mamlaka”.


Ni ukweli ulio wazi kuwa  kiongozi anatakiwa kuwa, mtulivu, mvumilivu na anayetumia zaidi hekima kuliko mabavu”, kiongozi anatakiwa Kuwa na  msimamo wa uvumilivu ni moja ya kazi ngumu zaidi miongoni mwa viongozi dhidi ya wananchi katika jamii. Ni ukweli ambao haufichiki kuwa  viongozi hawakuzaliwa wakiwa wavumilivu, lakini lazima tujifunze kuwa wavumilivu. Katika siasa uvumilivu wa kisiasa unakuza  utamaduni wa utawala bora na ukomavu wa demokrasia; na Kwa demokrasia kufanya kazi vizuri, wananchi lazima kuwa tayari kuvumilia na kuvumiliana.



Dhana ya uvumilivu ni ya msingi sana kwa maendeleo kwani inaruhusu mawazo mapya ndani ya jamii; kupitia dhana hii ya uvumilivu, kiongozi anakuwa  tayari kukubali  na kuheshimu  maoni na mawazo ya watu wengine na haki zao kwa uwazi na uhuru. Katika hali hii,uvumilivu huruhusu kuwepo kwa vyombo  huru vya habari kutumika kama chombo muhimu kuwahabarisha wananchi na kuwasilisha madai yao kwa viongozi wao. Demokrasia inahitaji vyombo vya habari amabvyo hugeuka kuwa daraja la mawazo kati ya viongozi na waongozwa. Vyombo huru vya habari husaidia   wananchi kuelewa taratibu ambazo zinaimarisha demokrasia.uvumilivu wa viongozi huru utasaidia kueneza demokrasia  na uwajibikaji kwani wananchi wataweza kukosoa serikali na ujumbe kufikishwa serikalini bila kuogopa.


ni ukweli kuwa Falsafa ya Uvumilivu hufunza na kuwakumbusha viongozi wanatakiwa kuishi kulingana na fikira njema. Mwenye kuifuata falsafa ya uvumilivu hayuko tayari kuamsha fikra mbaya za udikteta bali daima atajitaidi kuziepusha kwa kuendeleza uamuzi  wa uwazi na kwa kutumia njia  ya utulivu wa hekima kupitia uzoefu makini wa kimantiki: Kiongozi mwenye uvumilivu daima hutafakari, na kuziweka fikira mahali pamoja kabla ya kufanya uamauzi.Msingi wa kimaadili wa falsafa ya uvumilivu  kama mtaalam mmoja alivyo wahi kusema kuwa "zuri liko katika hali ya nafsi, yenyewe, inaonyeshwa katika hekima na kujidhibiti, hivyo kuboresha ustawi wa kiroho: Fadhila inatokana na nia ambayo inawiana na Maumbile. Kanuni inatumika katika uhusiano wa kibinafsi, yaani: kuwa huru kutokana na hasira, na wivu"

kwa ufupi tunaweza kusema kuwa uvumilivu umesheheni nini?
·        Tendo lililojaa subira kubwa,
·        Tendo ambalo kama linafanywa na kiongozi wa nchi basi anatoa uhuru mkubwa kufanya mambo bila kuingiliwa na nguvu za Ikulu,
·        Tendo lililojaa utu,
·        Tendo kwa serikali kuwa tayari kukosolewa na watu binafsi au vyombo vya habari.
·        Tendo ambalo linaashiria uwajibikaji wa serikali na utumishi wenye tija katika kwa taifa na wananchi wake katika kukuza demokrasia

Ni ukweli ambao haufichiki kuwa viongozi wetu wakiwa wavumulivu katika uwajibikaji wao mara moja  hurudisha imani ya wananchi dhidi ya serikali yake, upendo na matumaini katik ya viongozi na wananchi huongezeka pia: Tukumbukwe kuwa Ingawa watu wengi kufikiria uvumilivu ni upole  na kuto wajibika la hasha uvumilivu ni uwajibikaji ulio jaa busara na subira;


Swali lakujiuliza tunavyoelekea kusherekea miaka 50 ya uhuru wa Taifa letu je viongozi wetu katika awamu zote katika serikali yetu ya Muungano waliutumiaje uvumilivu katika kutekeleza majukumu yao?

Je uvumilivu wa kipindi cha mapambano ya uhuru wa taifa letu Bara  na visiwani katika miaka hiyo ni sawa na uvumilivu wa leo?

Je uvumilivu baiana ya vyama vya kisiasa ukoje? Ni kweli kuwa wanavumiliana katika kuchangia hoja katika mambo mbali mbali yanayohusu maendeleo ya Taifa letu?


Je hali ya viongozi wetu na vyama vyao wakati wa chaguzi mbalimbali uvumilivu hutawala kampeni zao?

Kuna maswali mengi sana ya kujiuliza hasa katika kipindi hiki cha kuelekea miaka 50 ya uhuru wa taifa letu na nini kifanyike baadaya ya sherehe hizo kwa manufaa ya taifa letu la Tanzania

MUNGU IBARIKI TANZANIA KUELEKEA MIAKA 50 YA UHURU

Sunday, October 23, 2011

HONGERA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA KUTUNUKIWA SHAHADA ZA HESHIMA


“HONORIS CAUSA”



Kama ilivyoelezwa na wataalum wa vyuo vikuu ambavyo ndio watoaji wa Shahada ya Heshima “ Honoris Causa” kuwa;

shahada ya heshima ni ile itolewayo kwa mtu mwenye vigezo stahiki na aliyetoa mchango mkubwa wa maarifa, elimu au ujuzi katika eneo fulani la kitaaluma.

Kwa kawaida shahada hizi hutolewa kama njia ya kuheshimu na kutambua michango ya watu hao katika maarifa, ujuzi au eneo la kitaaluma kwa mfano, afya, uchumi, mazingira, sayansi au fasihi,
mtunukiwa wa shahada hiyo hapasi kuwa na uhusiano wa awali na taasisi inayompa heshima hiyo.

Mtu anayependekezwa kupewa shahada katika chuo chetu ni yule aliyetoa mchango mkubwa kwa umma au kwa taifa na sio lazima mchango katika taaluma bali ni kazi ya ziada yenye manufaa kwa umma nje ya wajibu wake wa kazi.

Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete toka alipochagualiwa kuwa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania amekuwa kiongozi ambaye amepata shahada zaidi ya moja nje ya nchi na ndani ya nchi;

Kwa maneno mengine ni kuwa Dr. Kikwete amekuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya jamii katika mfumo wa moja kwa moja (direct) na kwa kupitia viongozi wengine ( in direct) katika kuonyesha njia na kutekeleza majukumu amabayo amekabidhiwa kwa kulingana na katiba yetu;

Shahada hizi zote ambazo amepata zinahusiana na utendaji wa kazi ambao unampa sifa yeye kufikia kilele hiki na utekelezaji wa majukumu.  Kwa wale wote ambao wanakaa darasani na kufanaya utafiti na hatimaye kufanikiwa kutunikiwa shahada mbalimbali lengo kubwa na la msingi wake ni kuwawezesha  kuelewa na mambo mbali mbali kupita uchambuzi wa vitabu na utafiti na kutumia elimu hiyo katika kutatua matatizo ya jamii inayowazunguka;

Lakini kwa upande mwingine viongozi mbali mbali ambao hawana shahada ya juu wanaweza kwa namna moja au nyingine wakawa ni wasomi wakubwa sana ambao wanaweza kutatua matatizo ya jamii kuliko hata kama wengekuwa wamesomea kozi husika. Tuchukue utambuzi ambao Kenya waliona na kuamua kumtunukia Mheshimiwa Kikwete shahada ya heshima kupitia  chuo kikuu cha kenyatta,” kwa ujasiri wake wa kusuluhisha ugonvi wa kibaki na oginga 2008; suluhu hii ya ugomvi ilikuwa na maana kubwa sana katika nchi ya Kenya baada ya vifo vya wenyewe kwa wenyewe;

Je unafikiri kuwa “baadhi ya maelezo” ya hapo chini  yana mpa sifa  
Dr. Kikwete kutunukiwa shahada hizo zote za heshima?

Dr. Kikwete kama kiongozi wa chama na serikali ametumia muda wake mwingi kukemea Ufisadi unaofanywa ndani ya chama twawala na , serikali yake

Dr. Kikwete amekuwa mbele katika  kuimarisha utawala bora miongoni mwa  jamii;

Dr.Kikwete ariruhusu kuundwa kwa  tume huru ya kuchunguza mikataba mibovu katka sekta mbalimbali  zenye kulalamikiwa na wananchi

Kuhusu demokrasia, Kikwete amepiga hatua kwa kuruhusu kwa wazi mijadala mbalimbali. Vyombo vya habari na wananchi wamekuwa huru kuibua hoja mbalimbali zikiwamo hata zile zinazodhalilisha serikali pamoja na  kuagizi kuandikwa upya kwa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania iweze kuendana na miaka hamsini ya uhuru

Rais Kikwete ameendelea kuwa msikivu na kupokea hoja zilizotolewa na makundi mbalimbali ya Watanzania na kuzitafutia majibu kulingana na mipaka yake na bila kuingilia chombo kingine cha maamuzi.

Dr. Kikwete ameweza kuiagiza chombo kinachuhusika kutenda haki kwa watuhumiwa wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA)  na wale wote waliotumia madaraka yao vibaya; uamuzi huu wa busara unatoa  matumaini kwamba rais kweli amedhamiria kupambana na ufisadi ambao unatishia uhai wa uchumi wa nchi yetu,

Kikwete kwa kiasi kikubwa kaonyesha kutoingilia Bunge wala Mahakama katika utendaji, ndiyo maana baadhi ya mambo yamefanikiwa.

Dr. Kikwete amesaidia kuleta suluhu Kenya na Zimbabwe na kuuweka uongozi wa umma Comoro, baada ya kutuma vikosi vyetu huko.

Amesimamia muafaka kati ya CCM na CUF  mpaka serikali ya umoja wa kitaifa imepatika na inafanya kazi kwa kushirikiana vizuri sana.

Lakini ikumbukwe kuwa hata wasomi ambao wanakaa darasani katiki kusomea shahada kama aliyopewa mheshimiwa Kikwete wanakabilia na “ challenges”; na kwa msingi huu Si rahisi kwa binadamu akawa na mazuri matupu; hakuna aliye mkamilifu kwani sisi si malaika na Mheshimiwa Kikwete kadhalika,kama binadamu anayomapungufu yake;

Rais Kikwete kwa mazuri aliyofanya anastahili heshima hiyo kwa  pamoja na mapungufu yake na kama kiongozi bado ana muda wa kurekebisha kasoro zilizojitokeza katika uongozi wake kwa kuendelea kuwabana watendaji wake walio chini yake; lakini tusisahau kuwa nasi tunamchango wa kufanikisha maendeleo yetu tukishirikiana na Mheshimiwa Rais wetu.

HONGERA SANA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA KUTUNIKIWA SHAHADA ZA JUU ZA  HESHIMA  NJE NA NDANI YA NCHI

Karibu tujadili kwa maendeleo ya Taifa letu

Friday, October 21, 2011

LEADERSHIP ACCOUNTABILITY VS 50 YEARS OF INDEPENDENCE


WHEN I GET THE BUS FARE

A SONG BY MRISHO MPOTO  
    

ANALYSIS BY       ROSE EMMANUEL TURUKA
KALAMAZOO CHRISTIAN HIGH SCHOOL     OCTOBER     2011

This song is about a man in the village who desperately wants to visit his uncle in the city. He wants to remind his uncle what he is left behind, but he doesn’t have the bus fare.

The author Mrisho Mpoto shows rather irony and metaphor in singing this song. He starts off with “if I receive a bus fare I will come and visit you uncle” he continues by saying “it is better to build a bridge than a wall” literally we would say that Mwisho is longing to see his uncle, he has sort to put that into his first priority that he doesn’t have money to visit him but if he had he would;  instead Mwisho is still converting the message through  song to the President to whom he calls “uncle” advising him on the ways to control the government , because the government is not doing enough to help the people of  are indeed

Mwisho says “it is better to build a bridge than a wall” he is trying to make him understand that a wall separates individuals, the wall he builds between the people and himself call for no communication rather separation. It is an obstacle that blinds you from the reality from another side of the wall and fills you with the fantasy to believe that the other side which you don’t see there is no problems. So he says” it is better to build a bridge “for then people will be able to go from one point to another and will be able to communicate for you will be able to see sides, the reality and fantasy. He then goes on in saying “spring water is not forceful. If you want to drink it's  water you must bend down to it”. Here Mwisho is establishing the point that in order to get the water to drink you must follow the rules and everything that comes with it. You have to get close to the spring water. I believe Mwisho is trying to send the message that, for the President to lead this country effectively, he must not sit in his office waiting for the details to come to him, he should go out and search for the details himself, and not to wait until campaign time. It is true that when President is interacting with people in day to day activities President can see what people are needed truly; Mrisho caution leaders not to wait and appeal to citizens it, what can be changed and how it can be improved changes during voting time.

Mwisho uses the line” you just want the world to be like a village; congratulations”. As the irony of how poor the work of leaders have become the emphasis they give, doing the campaigns is not the work they produce after being in the office. Mwisho says” congratulations” as the irony that it is a poor job, thinking about globalization while village people are suffering for poverty and nothing has improved and the country is falling. Why you just want the world to be like a village, why you want  to focus on external policy while the country is poor, no improvement, no direction, no good leaders, because that is what is happening. There is no good leader to take care of the nation that we are deteriorating slowly.

In the second verse Mwisho asks” uncle do you know your team? Do you know who is loyal and who is not? Character is like skin of the body difficulty to change, remember that the child of snake is not being taught how to bite if you laugh with the monkey you will get the flu”. Mwisho is raising the awareness to the President on the people he takes advice from and operates with. He says the child of a snake is not taught to bite, the leaders who are corrupt not necessary will teach their children how to, they will grow up with it; perhaps they have grow up with it too. So if he stays and do nothing about and laugh with them instead, he will also be contaminated by their disease of corruption practices. And so it is better to take precautions before your get sick.

In this song Mwisho Mpoto establishes the ideas that president should take his responsibilities and matters and look at the issue closely, work so close with people in order to improve the country and people’s conditions. This song is so powerful, Mwisho sees social oppression and is trying to awaken citizen’s mind through the massage to his “Uncle”. I believe that many social movements and social transformation processes have always use music as a tool for social change.

ROSE EMMANUEL TURUKA

Wednesday, October 19, 2011

VYAMA VYA UPINZANI NA WAJIBU WAKE


MAJUKUMU YA VYAMA VYA SIASA NI NINI BAADA YA UCHAGUZI?

 Je uchochezi na kuleta vurugu dhidi ya chama kilichoshinda kuongoza nchi?

Je  malumbano baina ya vyama vya upinzania vyenjewe?

Je vinabaki vyama vya msimu kwa kusubiri uchaguzi ujao na ruzuku?

Jukumu kubwa la chama chochote cha upinzani ni kuangalia kwa makini sera za chama tawala, na kuzipinga pale ipasapo, na kutoa mikakati na sera mbadala na kuwafahamisha wananchi kuhusu masuala yote ambayo yanahusu uendeshwaji wa serikali.

Kila kimoja kinapokuwa kwenye upinzani kinakuwa na kazi ya kukikosoa chama kilicho madarakani ili kukipa changamoto katika kufanya kazi vizuri. Uwajibikaji wao utawapa fursa wapiga kura kuafanya uamuzi wao kutokana na mafanikio ama kushindwa kwa chama kilichokuwa madarakani kutimiza yale iliyokusudia kuyafanya.

Je kama vyama vya upinzani vinalumbana vyenyewe kwa vyenjewe  matokeo yake nini?

·        Vinapoteza muda na malengo ya vyama vyao kwa kuanza kulumbana na wapinzani wenzao. Kwa kufanya hivyo, vinajidhoofisha vyenyewe.

·        Vinapopambana vyenyewe kwa vyenyewe vinakipa chama tawala kupata upenyo wa kuendelea kutawala na kupata hoja ya kuvisema na hata chama tawala kisipotekeleza sera zake kunakuwa hakuna chama mbadala cha kuwaambia wananchi mapungufu ya chama tawala

Umuhimu wa  Elimu ya uraia na  mikakati ya vyama kushika dola ya kuongoza nchi

Ukosefu wa elimu ya uraia imetufanya wengi wetu kuingia katika malumbano ambayo yanafanya safari ya kuelekea demokrasia bora kuwa sio nyepesi.

Kuna haja ya kuanziasha makakati wa kitaifa wa kutoa elimu ya uraia kwa wananchi. Jambo hili litafanyika kama serikali itakuwa na nia ya kuleta demokrasia ya kweli nchini.

Ulazima wa elimu ya uraia upo sana kwa mwananchi wa kawaida kuelewa dhana ya mfumo wa vyama vingi na umuhimu wake katika uendeshaji wa masuala ya kila siku ya serikali na sio ile maana ambayo ipo kwamba chama cha upinzani ni fujo, kupoteza amani na utulivu wa nchi, hawana sera au ni wapinzani wa kila kitu kumbe maana haswa sio hiyo bali ni waangaliaji wa kile kinachofanywa na serikali na penye mapungufu kukosoa

Ndo maana nasema elimu ya uraia ni muhimu sana katika kuhakikisha kuwa dhana nzima ya chama tawala na chama cha upinzani inaeleweka na nini umuhimu wa kuwepo kw achama cha upinzani katika kuhakikisha kuwa chama tawala kinawajibika kutekeleza sera zake

Kwa nini  vituko kati ya chama Tawala na vyama vya upinzani ni sehemu yapropaganda ya siasa?

Vyama vya upinzani vinatakiwa viendelee kuwajibika, katika mazingira yeyote yale dhidi ya chama tawala lakini kwa busara ili kukubalika miongoni mwa wananchi; chama tawala daima kitakuwa kinajitahidi kuhoofisha upinzani, kufanya uwe dhaifu,  na daima ili kuvipunguza kasi vyama vya upinzani  na kuvifanya kuwa haviwezi kuwa na majadiliano ya kuijenga nchi;

Demokrasia ni demokrasia na daima inataka Pande zote mbili kati ya chama tawala na upinzani kwa  pamoja kuzingatia sheria za mchezo. Demokrasia kama msimamiza wa kandanda ya siasa inapinga vikali wachezaji kucheza “ Rafu” na daima inawategemea wananchi katika kusaidia katika maamuzi ya sahihi na kufanya  kandanda ya siasa kuwa safi; kwa hiyo ni jukumu la wananchi  kuelewa sheria na elimu ya mchezo huu. Tusipofanya jitihada za dhati kabisa katika kulielewa hili  Demokrasia inakuwa fujo.

Ni dhahiri kwamba kama watu wako makini na wanachuikua taadhari , nguvu zote bila kupita katika mikono ya wanasiasa wajanja kitaalamu na waaribifu ambao mara chache hujitashidi kuwarubuni raia ambao hawana elimu ya kutosha na wale ambao wako katika mazingira magumu katika  kutekeleza sera ambazo kuwasaidia kuendeleza utawala wao.

Vyama vya upinzani wakati wote vinatakiwa kuwa na  uwezo wa hoja ili kuweza  kukuza  majadiliano  na mijadala,  na kujitahidi  kuachana na mayowe, hoja za nguvu ili kuviwezesha vyama hivyo  kubaki    katika mijadala ambayo itakuwa na tija kwa wananchi kama mijadala ya afya , ustawi wa jamii na uwajibishaji wa serikali iliyoko madarakani; na bila kusahau kuendeleza aina fulani ya "mazungumzo ya kitaifa" na kushinikiza mjadala wa kidemokrasia kwa kiwango cha juu ya ili kuleta zaidi ukomavu wa demokrasia nchini;

Ili kujiimarisha zaidi miongoni mwa wananchama wao na wananchi kwa ujumla nyama vya upinzani vinatakiwa daima viweze kujisafisha na kuwa na rekodi nzuri ya matumizi ya fedha. Kukumbuke kuwa uwajibikaji uanza ndani ya chama chenyewe; upinzani ili kudumisha uwazi, vinatakiwa wakati wa mikutano yao ya ndani itawaliwe na uwazi; kiwe ni chama cha wote na sio chama cha mtu Fulani au kikundi Fulani cha watu. kuhakikisha matumizi ya fedha za chama kuwajibika ni zaidi ya uwezekano wa kubeba sifa hizi ndani ya utawala wake

Vyama vingi vya upinzani daima vinakabiliwa sana migogoro ya ndani na ukosefu wa Utawala  bora ili kujihakikishia ushindi katika kinyanganyiro cha ushindi wa kuongoza nchi vyama vya upinzani lazima vijenge jitihada  za kichama katika kuimarisha  demokrasia mahiri wa ndani ili iweze kusamabaa baina ya wananchi ambao ndio washika dau wakuu tukumbuke kuwa “ Love starts at home”  kwa kufanya hivyo  vyama vya upinzani vitakuwa vimefanikiwa kutimiza Lengo  la kuimarisha demokrasia ndani ya chama kabla ya kuwa mabingwa wa demokrasia na utawala bora kitaifa. Demokrasia ya kweli  haiwezi kustawi bila upinzani mahiri.




Namaliza kwa kujiuliza je vyama vyetu vya upinzani hapa Tanzania vinafanyaje kazi zake?


vinapingana kwa hoja dhidi ya serikali iliyopo madarakani?


vimeweza kujiimarisha na kutoa elimu ya uraia kwa wananchi waishio vijijini, au vinajikiti katika miji mikuu tu ya wilaya au mikoa?


na wanapotofautia na serikali vinatumia mbinu gani katika kuhakikisha kuwa hoja imefika bila kuvunja amani yetu?


Lakini tusisahau kuwa  "Politics is a dirty game. A good person shouldn't be involved in it."

Monday, October 17, 2011

UTAWALA BORA NA ELIMU YA URAIA VIJIJINI


UONGOZI USIO NA TIJA HUZORETESHA ELIMU BORA YA URAIA MIONGONI MWA WAPIGA KURA WAISHIO VIJIJINI



Kipimo cha uongozi bora ambao hutokana na uongozi uliotukuka  ni  pale tu wapiga kura wanapoufurahia uwajibikaji wa viongozi walioko madarakani kwa  kuwatatulia kero ambazo zinahitaji nguvu ya serikali kama huduma bora za jamii kwa  maendeleo yao.

Lakini katika nchi zinazoendelea, bado zinabaki kuwa wahanga wa migogoro ya kiuchumi na kisiasa. sababu kubwa ya migogoro hii ni uongozi mbaya katika nchi husika.

Tanzania kama nchi nyingine za kiafrika bado tunakabiliwa na hali mbaya inayotokana na ubadhirifu wa fedha na utumiaji mbaya wa madaraka ambayo baada ya kumsaidia Mwananchi kumkwamua kiuchumi na kijamii bado mwananchi wanaendelee kukabiliwa na tatizo la umasikini.

Uchambuzi wa maswala ya kiuchumi unatukumbusha kuwa nchi ikifikia katika hali hii inatuonyesha kuwa kuna tatizo la utawala bora, kuna tatizo la uzalendo  kuna tatizo la balance of power;Je serikali inasimama upande upi? Kumsaidia wananchi wa kawaida au kuwatajirisha mtu mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu wachache kwa masilahi binafsi?
Je ni nani waliowaweka viongozi madarakami ni wananchi wanyonge walio wengi au ni kikundi kidogo cha watu wenye pesa?
Kama ni wananchi ambao ndio waliowachagua viongozi kwa kura zao; kwa maoni yangu  kama wananchi kuendelea kuishi katika lindi la umasikini katika nchi yenye rasilimali  nyingi ambazo nchi inamiliki ni ukiukaji wa haki za binadamu.

Hivi sasa kama Taifa tunahitaji viongozi ambao wataweza kuwatetea na kuwaletea wananchi wao maendeleo;

Tunahitaji viongozi waaminifu na wasafi; hili ni jambo la muhimu sana kwa maendeleo ya taifa tukuangalia sana viongozi wetu wanakosa sana sifa hizi mbili kuu muhimu; viongozi wengi wa Afrika wamechagua kutekeleza sera maovu(ufisadi) badala ya upendo mkubwa kwa taifa( utawala Bora) husika.

Nafikiri itakuwa ni jambo la busara kama viongozi wetu watakubali kusimamia elimu ya uraia kwa wananchi wa vijijini ili kusaidia katika mageuzi ya kuboresha utawala na kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi, na utulivu wa kisiasa ambao ni sehemu ya  utawala bora na utekelezaji wa kidemokrasia wanayohubiri. 
Tatizo la viongozi wetu wanashindwa kuja na vision nzuri ambayo kweli itasaidia maendeleo  na kuondoa kero ambazo wananchi wanakabiliwa nazo kila siku;
Hali hii tata kushindwa kutatua malalamiko ya wananchi kwa miaka mingi  ilimpelekea Robert Wheelen wa Taasisi ya Uchumi. Katika jarida la taasisi ya mwezi Septemba 1996 kuuliza’ kwa nini nchi ya afrika isibinafsishwe kwa nchi tajiri ili kuwasaidia kutatua kero zinazowakabili na kuwasaidia katika kusimamia katika kutoa huduma bora na kuleta ufanisi na nidhamu  wa ukusanyaji  kodi kwa maendeleo ya nchi zao’

Kauli hii wakati mwingine inaingia akilini pengine kuna kweli  kama viongozi wetu wanaelekea kushindwa kutatua kweli za wananchi wao pengine swala hili la ubinafsishaji linaweza kuwa ni suluhisho la maendeleo kwa wote;
Maswali ninayojiuliza kutoka na kauli hii;
·        Je Serikali yetu ya Tanzania imefanikiwa kwa kiasi gani katika ukusanyaji wa kodi hali ambayo imefikiwa sasa tunaweza kujisifu tumepiga hatua au bado juhudi zinahitajika katika kuendelea kufanikisha hili?
·        Je Serikali yetu inasimamiaje shughuli zake za kuendesha serikali kwa faida ya wote, je utawala bora unatekelezwa au bado tuna usugu wa usimamizi mbovu chini na ukosefu wa uwezo wa utawala bora?.
·        Je Serikali yetu imeandaaje miundo na mageuzi ambayo yataimarisha utawala wa sheria, kusaidia kukuza demokrasia na uwajibikaji na uwazi.
·        Je kwa nini wazee wetu kama Mandela, Nkrumah na Nyerere wameendelea kuwa  viongozi bora na wa kuheshimika ndani ya nchi na nje ya nchi zao?
·        Je viongozi bora wanatakiwa wawe na sifa gani?
 kwa matazamo wangu:
  • anayeweza kuwasiliana  na kuwasilisha hoja kwa ufasaha,
  • mwenye uwazi na mawazo mapya,
  • uwezo wa kusikiliza pande zote za mipango endelevu,
  • mwenye hekima na akili ya kawaida,
  • uwezo wa kusimama  na kuongoza wakati political or economic crises ,
  • kujua ukweli kabla ya kufanya maamuzi,
  • Kiongozi bora lazima awe mchapa kazi na mwajibikaji
Tunamkumbuka Mwalimu Nyerere alipoamua kwa hiari yake kuachia madaraka na kutengeneza platform kwa kiongozi wa kuchukua madaraka ya urais kwa kupitia vikao halali ndani ya chama chake na nje ya chama chake.


Kwa msingi huu  Viongozi bora kuandaa watu wao wa kuendeleza safari ya uongozi wa nchi bila woga wa kushitakiwa wakiwa nje ya madaraka; viongozi wetu lazima wajifunze kuwa  mabadiliko ya uongozi ni muhimu kwa ajili ya kuanzisha tawala mpya.  Hapa ndipo tunapoona umuhimu wa elimu bora ya Uraia.


Utawala bora ni utekelezaji wa uwezo na mamlaka na serikali kwa njia ya kuwa watumishi bora wanaoweza kuboresha ubora wa maisha ya wananchi wake. Hii itasaidia kujenga jamii bora na yenye uwezo wa kujikwamua na kupambana na changamoto zinapojitokeza

Na hitimisha kwa kusema kuwa Kuwa kiongozi bora si kazi rahisi wakati mwingine inahitaji mtu kuwa na maono ya mabadiliko, elimu ya utambuzi, mawasiliano ya wazi bila woga, na kuwa tayari kufanya maamuzi  magumu. Tunahitaji viongozi  ambao ni wawajibikaji wa maendeleo yetu; ambao watusaidia sisi kukimbia wakati wenzetu wanatembea katika kuyatafuta maisha bora. Tunawaombea viongozi wetu waweze kuwa charisma na maono ya kujenga upya taifa letu kisiasa na kiuchumi kwa maendeleo ya wananchi wao bila kusahau elimu bora ya uraia.