WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, May 7, 2015

YANGA SC YAPELEKA KILIO SIMBA

AZAM FC imekata tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mabingwa Yanga SC jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
 
Ushindi huo, unaifanya Azam FC ifikishe pointi 48 baada ya kucheza mechi 25, nyuma ya mabingwa, Yanga SC wenye pointi 55 za mechi 25.
 
Simba SC ipo nafasi ya tatu kwa pointi zake 44 na hata ikishinda mechi yake ya mwisho itafikisha 47, hivyo kwa mwaka wa tatu mfululizo Wekundu wa Msimbazi watakosa michuano ya Afrika. 
Azam FC ilitoka nyuma kwa 1-0 baada ya Mbrazil Andrey Coutinho kutangulia kuifungia Yanga SC dakika ya 12 na Bryson Raphael akasawazisha dakika ya 14 kabla ya Aggrey Morris kufunga la ushindi dakika ya 85. 
 
Kikosi cha azam kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Gadiel Michael, Shomary Kapombe, Aggrey Morris, Mudathir Yahya, Brison Raphael, Frank Domayo, Gaudence Mwaikimba, Kipre Tchetche na Brian Majwega. 
 
YangaFC; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Rajab Zahir, Pato Ngonyani, Saum Telela, Danny Mrwanda, Nizar Khalfan, Amissi Tambwe, Mrisho Ngassa na Andrey Coutinho

DT. SHEIN AFANYA ZIARA MAENEO YALIYOKUMBWA NA MAAFA YA MVUA, ZANZIBAR


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na wasaidizi wake alipofika Uwanja wa Farasi na Kwahani Mjini Zanzibar leo wakati alipofanya ziara ya hafla kutembelea wananchi wa sehemu hiyo waliopatwa na maafa ya kuingiliwa na maji ya mvua iliyonyesha juzi na kupelekea maafa yaliyosababisha kukosa makaazi bora.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wananchi wa Uwanja wa Farasi na Kwahani Mjini Zanzibar wakati alipofanya ziara ya hafla leo kutembelea wananchi wa sehemu hiyo waliopatwa na maafa ya kuingiliwa na maji ya mvua iliyonyesha juzi na kupelekea maafa yaliyosababisha kukosa makaazi bora.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Injinia Ramadhan China wa Idara ya Ujenzi wakati alipofanya ziara ya hafla leo kutembelea Maeneo ya Mwanakwerekwe Mjini Unguja kuangalia maafa mbali mbali yaliyowakumba wananchi wa sehemu hiyo kwa kuvunjikiwa na nyumba zao kutokana na mvua kubwa iliyonyesha juzi na kupelekea hasara mabali mbali.(Muro)

source: mjengwa.blog