WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, July 31, 2011

KASHESHE WIZARA YA NISHATI NA MADINI

SHERIA AU MAZOEA AMBAYO YANAENDESHA WIZARA ZETU?

“Don't ever take a fence down until you know why it was put up”.

"Kwa jinsi jambo hili lilivyokaa, hakuna jinsi mtu unavyoweza kulitetea hata kidogo, nilitamani sana kwamba nije hapa niseme kwamba uamuzi wangu mimi ni huu, lakini haikuwezekana,"

"Kwa dhati kabisa naomba wabunge tuwe na subira, mara tu mheshimiwa Rais atakapotua South Africa (Afrika Kusini) jioni ya leo  (jana), nitamuarifu na ninaamini tutaelewana kuhusu hatua za kuchukua."

KISHERIA hakuna  mtu aliye juu ya sheria. Iwe kiongozi wa umma, serikali, taasisi yoyote au mwananchi wa kawaida anatakiwa kuheshimu kanuni na misingi ya sheria.Watu wote wanapaswa kutii, 
kuheshimu na kuzifuata kwa mujibu wa Katiba ya nchi husika.

Sheria zinapaswa kufuatwa bila kujali au kubagua mhusika kwa namna yoyote uwe wa rangi, kabila, dini, itikadi au kitu kingine cha namna hiyo; kwa msingi huo Kuvunja sheria yoyote ya nchi ni uhalifu. Bila kujali cheo au hadhi ya mhusika, itikadi yake, utajiri au umaskini kiasi gani, wala haihusiani na rangi hata kabila ni jambo ambalo haliruhusiwi. Kwa msingi huu ukiukwaji ukifanywa kunakuwa na karipio linaloendana na adhabu, kwa msingi huu hata matukio ya watu kujichukulia sheria mikononi kwa kuadhibu wenzao ni kosa kisheria japo kiutamaduni wetu wa kila siku inaonekana ni haki mbadala.

Viongozi wetu wanaposhindwa kufuata sheria na kuvunja sheria hupelekea wananchi kuishi maisha ya wasiwasi kwani hupoteza imani na kuua mfumo mzima wa sheria na uaminifu;

Tukio la hivi karibuni la Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini la kuamurisha idara zote ambazo ziko chini yake kuchangia mchakato wa Bajeti ya Wizara hiyo, kimsingi ni ukiukaji wa sheria ya Matumizi sahii ya fedha za walipa kodi;

Watu wamejiuliza maswali mengi sana hizo pesa zote kwa nini zitumike katika mchakato wa kupitisha bajeti husika? Bajeti hiyo ilikuwa na siri gani kubwa hata wizara itafute pesa zaidi kutoka katika idara zake?

Pesa hizo walikuwa wanapelekewa akina nani? Walikuwa wanalipwa akina nani? Na kwa kiwango na kigezo gani?

Je kunauwezekano mkubwa sana kwamba kuna pesa nyingi sana katika wizara na idara zake ambazo ziko ziko tu (idle) na waataalamu kwa kushirikiana na wanasiasa wanazitafutia njia za kuzitafuna kwa kigeuzo cha uandaaji na upitishaji wa bajeti?
Je katibu Mkuu husika huyo ametolewa kafara safari hii kwani inasomeka kuwa ni mazoea yao kila mwaka utaratibu huu hufanyika?

Sasa kama katibu mkuu ni kinara wa kuashiria rushwa ndani ya utendaji wa kazi zake je kuna haki ambayo itatendeka kwani tunafahamu kuwa makatibu wakuu ndio wataalaum ndani ya wizara ambao wanatumiwa kama wataalamu (professional /professionalism).

Katika hali kama hii je tunaweza kumuhukumu mara moja au inatulazimu tusubiri  na kutoa hukumu mpaka tupate vielelzo vya uhakika kama Katibu Mkuu Kiongozi alivyosema?

Kama ndivyo je utaratibu wa serikali wa kulishughulikia swala hili ni sahihi? Kwa nini aendelee kulipwa (likizo) ya malipo wakati ni mtuhumiwa katika kesi hii?, kwanini stahili zake zote  zisimamishwe na kama hatakuwa na hatia ndipo arudishiwe hizo stahili?

Kwa staili hii Je serikali haioni kuwa unaongeza wasiwasi katika uchunguzi wake na pengine kuwapa wananchi mawsali mengi ya kujiuliza kuwa serikali yetu sio makini?

Si vyema kuhukumu au kuondoa uzio bila kuelewa nini kiko nyuma ya huo uzio? Kwa nini katibu huyo aliytoa agizo hili  kwa kujiamini  kimandishi?

Je ni utaratibu huu ni wa wizara hii tu au ni wizara zote  hutumia utaratibu huu katika uchakachuaji wa bajeti zao?

Sheria daima zinawekwa kama uzio ili kuzuia wavunjaji wa sheria wasipate njia rahisi katika kutekeleza adhima yao; sehemu ikiwekwa uzio tayari inakuwa imejijengea utaratibu wa watu kufuata kana wanataka kuingia ndani wapiti katika mlango ulio salama; endapo mtu ataruka uzio huo huyo ni mharifu na anastahili adhabu; kwa hiyo uzio hujengwa kwa ajili ya kumzuia mtu yeyote kukiuka sheria zilizopo; Je katibu huyu hajekiuka taratibu kwa kuruka uzio alioujenga yeye mwenyewe?

Kama ndio hivyo kwa nini tujenge uzio ambao mwisho wa siku na wajengaji wenyewe ndio wanao vunja?

Tunaiomba serikali iwaadhibu watendaji wote wa juu wa serikali kulingana na matendo yao kitendo cha Katibu Mkuu kuagiza uchangiji wa pesa hizo na kuwa na matumizi ambayo hayajeidhinishwa kisheria ni kosa kubwa la kuhujumu  uchumi wanchi;

Nakumbuka mheshimiwa Rais aliwahi kusema kuwa;
kila mara zingatieni nidhamu ya matumizi ya fedha za serikali ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria, kanuni, taratibu za fehda, na taratibu za manunuzi.

Wabadhirifu na wezi wa fedha za umma wachukuliwe hatua za kisheria.

Je katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini wakati anaandaa utaratibu huu alishauriana na nani? Kuna Kiongozi wa juu pengine alimpa uhakika kuwa achangishe tu atamlinda au utaratibu ambao ameukuta katika wizara hiyo na amekuwa akiuendeleza tu?

Mheshimiwa Rais sasa anatakiwa waonea haya au kuwavumilia viongozi hawawa namna hii wanaotumia nafasi zao katiaka kufanya  ubadhirifu ambao unakoleza ufujaji wa mali ya umma na kudidimiza maendeleo ya nchi. Ni viongozi hawa ambao wanasukuma guruduma la maendeleo nyuma wakati wenzao tunajitahidi kulibingirisha kwenda mbele!

Tunaihimiza serikali kuchukua hatua zinazofaa ambazo zitakuwa ni mfano kwa wengine ambao wanatabia kama ya Katibu Mkuu mhusika.

Friday, July 29, 2011

URAFIKI WETU NA WANASIASA TUNAWEZA UELEZAJE?

Kuna hii nukuu kuhusu aina tatu za marafiki najaribu kuioanisha na viongozi wetu wa siasa Tanzania; Je wanasiasa wetu wanafanana na nukuu hii?

“Kuna aina tatu za marafiki, wale wanaolinganishwa na chakula kwani bila chakula hatuwezi ishi; wale kama dawa ambao tunawahitaji wakati Fulani tu na wale kama ugonjwa ambao hauwahitajia kabisa”.

Maisha katika medali za siasa katika dhama hizi je tunaweza kuwalinganisha au kuwatenga wanasiasa wetu katika makundi matatu kulingana na nukuu ya hapo juu? Kama ni ndio, swali la msingi hapa la kufungulia mjadala wetu wa leo Je tafsiri  ya nukuu hii iweje sasa?.  Na namna gani tunaweza kudurufu ukweli wa msemo huu;

Hebu tuwangalie Wanasiasa ambao tunaweza kuwalinganisha na

chakula”;

 kundi hili ni lile la wanasiasa ambao wana busara, hekima uadilifu, waaminifu, wakweli wastaarabu wacha Mungu na wawajibikaji wa kweli; utendaji wao wa kazi unaongozwa na maadili na woga kulingana na imani zao na zinazoangalia sana matendo mema.  (Hayati Edward M.Sokoine )

Kundi hili wao wanaona kuwa nafasi ambazo wanazo kama wanasiasa au cheo ni dhamana isipotumiwa vizuri kwa manufaa ya wote mtoaji anahaki ya kukichua cheo hicho na kumpa mtu mwingene ambaye ni mwadilifu, na mwaminifu.
Tunajua kuwa chakula ni uhai, na ni muhimu sana kwa maisha ya binadamu, kwani mwili wa binadanu unahitaji chakula, bila chakula mwili utadhoofika na hatimaye kushindwa kufanya kazi na pengine kusababisha umauti kwa kiumbe husika;

Hili ni kundi ambalo kwa sababu ya ukweli wao uwajibikaji wao wakipata nafasi nzuri ya kuwatumikia wananchi wanatekeleza ahadi  kwa matendo, na ikitokea kunatatizo la utekelezaji wa ahadi hizo anakuwa tayari kusema ukweli na wananchi wanakubaliana naye kwa tabia yake ya iliyotukuka.

Hawa ni wale ambao wanaweka masilahi ya taifa mbele kwa faida ya watanzania, ambao wao huridhia muafaka wa sera nzuri za maendeleo ya nchi. Hawa ni wale ambao wanajenga daraja la uaminifu kati yao na wananchi waliowapa nafasi ya kuwatukimia. Hawa sio wanafiki wachoyo, wezi wala rushwa; ni viongozi ambao wanaridhika na kile kidogo ambacho wanapata; ( Mwalimu Nyerere)

Wanasiasa kama dawa

Hawa ni wanasiasa ambao wana vipaji vya kuweza kujenga hoja nzuri na wanajitahidi katika utekelezaji wa sera nzuri kwa wananchi; lakini wanashindwa kutimiza malengo yao kwani mara nyingi wanakosa nyezo nzuri za utandaji au kukubalika ndani ya serikali kwani. Ni kundi ambalo ni nzuri na tegemeo katika uhai wa siasa na uongozi wan chi, lakini hawahitajiki sana wanatumika tu kwa sababu Fulani kwa muda mfupi hataji likikamilika husaauliwa mara mpaka kuwe na hitaji tene; hawa ni madorate  wazuri wajenga hoja nzuri hata wakati mwingine wapatanishi wazuri; tatizo hawahitajiki wakati wote kwani wanaonekana kama vikwazo na wakati mwingine wanakuwa hawana nguvu sana na wakiweza kufanya kazi pamoja na wanasiasa wa kundi la kwanza kuna kuwa na msukumo mzuri sana wa maendeleo ya nchi;
Hawa ni wafichuaji wa uozo wa serikali


Wanansiasa kama ugonjwa

Kundi hilli la wanasiasa hatuwahitaji kabisa kwani ndio wale mangunguli wa kula rushwa ambao wanaishia kuliingiza taifa katika hasara kubwa sana;

Kundi hili linatawaliwa na ubinafsi zaidi; kundi la umimi ni watu
wasiojali maendeleo ya wananchi kwa jumla wao hukumbuka tu raha zao hawakumbuki wengine. Hawa ni wanasiasa ambao wanazungumza mno kuhusu siasa na sio sera. Kwao siasa ni kila kitu; Wanasiasa wabaya daima huweka matumaini yao mbele na kuua matumaini ya maendeleo ya taifa; kwa kuwalagai wananchi kwa siasa uchara zenye faida ya muda mfupi na huwa kama kiini macho kwaJamii.

Kundi hili lina pesa nyingi ambazo upatikanaji wake unatia mashaka; daima ni pesa chafu na zinaendelea kutumika katika mchezo mchafu. Hawa ni wanasiasa ambao ni wala rushwa, rusha wanapata kutokana na kujihusisha na rushwa; ni makini na ni werevu sana na wanafahamiana na watu wengi wapenda rushwa; kwao siasa ni rushwa na bila kujiingiza kwenye siasa hakuna rushwa.

Je tutauondoaje ugonjwa huu Mkubwa?

Tunawahitaji tuwe na wafanyakazi wa serikali ambao ni  waaminifu ambao wataweza kuwazuia wanasiasa walafi katika mipango yao ya ufisadi.

tunahitaji serikal ambayo ni safi; tunahitaji watendaji wasafi ambao ni sehemu kubwa ya serikali. Serikali ambayo haitakuwa tayari kuwakaribisha mafisadi hao katika utendaji wake; serikali ambayo itakuwa tayari kuishi kwa matendo bora na kuamini kuwa “ Ikulu ni Mahali Patakatifu” na sio sehemu ya kuwaruhusu mafisadi kuchafua utakatifu wake.


Ni ukweli kuwa hatuwezi kupata wanasiasa wakamilifu kwa asilimia mia moja; bali tunawihitaji wanasiasa ambao ni watendaji na waadilifu kwa asilikia kubwa  ambao watajitoa mhanga kwa ajili ya maendeleo ya watu wao na sio kurudisha nyuma maendeleo ya taifa.( sakata la Umeme Tanzania nani wa kulaumiwa ni siasa chafu iliyochafua hali ya mwanga na kuleta giza nene)

Tunahitaji viongozi wanaoweza kukemea hali hii ili kuwanyima nafasi mafisadi kuuza nchi kwa faida binafsi. Ni ukweli kuwa  Uongo na maigizo ya ulaghai yakirudiwa sana bila kukemewa yanaweza kuonekana kama ukweli; na wao kuonekana kuwa ni waleta maendeleo kumbe wamevaa ngozi ya kondoo wakati ndani ni chui wabaya sana.

“There are three types of friends: those like food, without which you can't live; those like medicine, which you need occasionally; and those like an illness, which you never want”. - Unknown

Saturday, July 23, 2011

WHERE ARE WE AS A NATION?

Men make history and not the other way around. In periods where there is no leadership, society stands still. Progress occurs when courageous, skillful leaders seize the opportunity to change things for the better. - Harry S. Truman

Tuesday, July 19, 2011

Politicians

There are three types of friends: those like food, without which you can't live; those like medicine, which you need occasionally; and those like an illness, which you never want. - Unknown

Sunday, July 17, 2011

The Reality about Life


Be nice to people on your way up because you'll need them on your way down. ~W. Migner.

This means that we need to treat everyone with internally and externally kindly, professionally and respectfully and if we can show them that they would be as valuable outside as inside;

There are some people who are completely selfless and for whom being nice is a difficult way. They take the advantage of given power and position to build meaningful one -way up and while in power they don’t think that one day they will need help on the way down.


The lesson here is to go out of our way to be nice and helpful to everyone we meet on the way up, as we will surely be on the receiving end on the way back down.

Saturday, July 16, 2011

BUNGE LETU NA MWELEKEKEO WAKE WA UTENDAJI (POSHO)

WAHESHIMIWA WABUNGE TUMIENI POSHO ZENU KATIKA KUPATA USHAURI WA KITAALAMU KWA FAIDA YA MAJIMBO YENU.

Bunge letu la 10 katika mikutano yake iliyofanyika na tangu kuzinduliwa mwishoni mwa mwaka jana, limeonekana mbele ya jumuia ya kitanzania ni bunge ambalo limetawaliwa na mambo mengi ya vituko ambayo pengine kwa wananchi wengi ni kama bunge ambalo halijadili sana matatizo ya wananchi bali linaishia katika mambo ya aibu kwa chombo kikubwa cha kutunga sheria na kusimamia uendeshaji wa mambo ya Serikali.

Wengi wanaona kinachoendelea Dodoma kila wakikutana ni kama uhuru ambao umepita mipaka ya kujadiliana kwa lugha ya kistaarabu, ni uhuru unaofanana na ule wa kijiweni au katika vikao vya moja baridi moja moto; au ni mijaddala ambayo inaendelea katika mazingira ambayo maelewano yanakuwa hayana usimamizi kila mtu anasema, na kama vile hakuna kiongozi wa kusimamia;
Bunge la 10 sio tu linajadili mambo ya manufaa kwa nchi yetu pekee, na kutoa michango yenye tija, bali huwa tunashuhudia vituko vya wabunge na kejeli wanazozitoa,

Pamoja na kuwa Mheshimiwa Spika amewaruhusu kuwa “Wewe kama una shida yako sema hapa… hata Mbunge akienda na vituko vyake bungeni, wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge wanaendelea kuwa wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wakanywe chai pamoja, waendelee na kazi”.  

Je Kauli hii inaashiria nini? Kwamba wabunge wanaruhusiwa kuongea chochote na kufanya chochote bila kujali maadili au Ethics za uongozi? Je Wabunge wanatawaliwa na maadili gani? Na kama ni hivyo kauli kama, “mlango ufungwe tupigane” ni sahihi? Kama ndivyo kwa nini basi mbunge alitolewa kwa kuvaa tofauti na maadili ya Kibunge? Je kauli yeyote iwe nzuri au mbayo ambayo haikizi utendaji wa bunge zinakubaliwa?

Je masilahi ya nchi yatatetewa vipi? Kama hakuna utaratibu wa kuzibiti nini kinasemwa  nafikiri kauli kama hizi zitakuwa ngumu kutekelezwa, mheshimiwa Spika aliendelea kusahuri kuwa:

“Nawaomba tuweke maslahi ya Watanzania na taifa mbele,tudumishe amani na utulivu, tupuuze sera zozote za kudhoofisha utaifa wetu kama Watanzania na kutugawa kwa misingi yoyote ile, iwe ya kikabila, imani za dini, rangi au kwa itikadi za kisiasa”

“Jamani tuendelee kukua, tusiendelee kuwa kero kwa watu. Walikuwa wanapenda sana kuangalia sana kipindi hiki, lakini sasa wengine wanakereka sana kwa tabia zetu. Kwa hiyo tubadilike, muwe watu waheshimiwa kama tunavyoheshimiwa na watu waliotuchagua.”

Nafikiri hakuna demokrasia ambayo haiana mipaka lazima kuna mipaka ya kila kitu: Je faida ya Mwongozo na kanuni za bunge zinafaida gani kwa wabunge na taif a kwa ujumla wake?


Kama Spika alivyodsema “Kuhusu hili la ‘Utaratibu na Mwongozo’, kwa kweli sasa tunatia aibu. Waheshimiwa mnajidharau, yaani imekuwa kelele, huku Mwongozo, mara kuhusu Utaratibu, tumegeuka kama watu wa Kariakoo!..... “Kariakoo ni sokoni kila mtu anazungumza anavyotaka na hakuna wa kuwazuia, lakini hapa ndani kuna utaratibu si sokoni,”

Kwa kweli nafikiri Posho ya Ubunge ya kila mwezi ambayo ni Sh5 milioni ambayo ni kwa ajili ya mafuta, matengenezo ya gari, malipo ya dereva na wasaidizi wa mbunge. Kama waheshimiwa wabunge wataweza kuitumia vizuri kuwaweka karibu na wataalamu kama wana sheria, wanauchumi na wataalamu wa jamii itawasaidia sana hawa waheshimiwa kwani hata wakiwa wanakwenda bungeni watajuu nini wanatakiwa kusema au hata wanapotoa hoja kuhusu mahitaji ya majimbo yao zinakuwa na uzito wa vielelezo; na hata uchangiaji wa hoja utakuwa ni wa uzito zaidi, kama wabunge  wengine wanavyofanya duniani? Hoja nzuri huvuta hisia za wabunge wengine bila kuangalia ni chama gani mbunge yuko; huu ndio mwelekeo ambao wananchi tunahitaji sasa;

Je wabunge wetu wana waataalamu wowote? Kwa vile posho zao kwa hivi sasa ziko kisheria basi watumie posho hizo kwa faida ya wananchi walipa kodi kwa kuwaletea maendeleo sio kugeuza bunge kuwa sehemu ya vituko  maudhi na vichekesho;
Kwa kweli Inatia aibu sana kwa watu kama wabunge kuzozana na kuoneshana umwamba ndani ya bunge, kauli za mwongozo kila wakati ni upevu wa demokrasia au kupevuka kisiasa bali inakuwa ni kero kwa wafuatiliaji makini wa mambo ya bunge kwa maendeleo ya wananchi.

Sio vyema Kulinganisha bunge letu na sehemu kama kariakoo kwani kwa mlinganishoi huu tunalivunjia heshima Bunge na  waheshimiwa wabunge kama moja ya muhimili mkuu wa serikali.
tabia ya kuropoka ovyo bungeni inayofanywa na baadhi ya wabunge mithili ya mkusanyiko ambao hauna nidhamu pasipomsimamizi.

“Hapa bungeni kuna utaratibu wa kuzungumza, mtu akiwa anazungumza wengine mnapaswa kumsikiliza, lakini jana (Juzi) mtu mmoja anachangia na wengine wanazungumza utadhani mko Kariakoo.”

Bunge si sehemu ya kuendeleza tabia za uropokaji, Bunge ni chombo cha kukusanya fikra ambazo zinasaidia serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake. Ni ukweli kuwa bunge litabaki kuwa ni sehemu ya kupambanisha fikra zinazogusa mustakabali wa umma

Waheshimiwa wabunge tumieni posho ambazo mnaendelea kuzipata kwa kuboresha hoja kwa kupata ushauri wa kitaalamu katika utendaji wenu;

Tunaweza kuzichapa kama huko Russia, waheshimiwa wakionyeshana ubabe
India je tatizo hapa lilikuwa nini hapa.

Friday, July 15, 2011

PICHA ZA WIKI HII





Je unaweza kuitafsiri vipi picha hizi?Zinakukumbusha nini? au Zinaashiria nini?

Tuesday, July 12, 2011

NUKUU YA LEO; JULIUS K. NYERERE- AMANI HUZAA MATUMAINI.


Amani ni zao la matumaini, pindi matumaini yatakapotoweka kutakuwa  na vurugu katika jamii. Nitashangaa kama hawa Watanzania watakataa kuasi. Kwanini wasiasi?  Wakati wengi wa wananchi wanapopoteza matumaini unajenga volcano.  Volcano hii italipuka siku moja. Labda kama watu hawa ni wajinga. Wengi katika watu wa nchi zetu ni wajinga ndiyo maana hukubali  kutawaliwa hivyo.  Kukubali kukandamizwa namna hiyo wakati wanayo nguvu inayotokana na wingi wao, ni kwa sababu ni wajinga tu. Hivyo basi Watanzania watakuwa ni wajinga na mataahira (idiots),  kama watakubali kuendelea kukandamizwa na watu wachache (viongozi)  katika nchi yao wenyewe".    Julius Kambarage Nyerere 

Monday, July 11, 2011

IS LEADERSHIP RESULTS OR ATTRIBUTES?



Peter Drucker says,  "Effective leadership is not about making speeches or being liked; leadership is defined by results not attributes". 

Sunday, July 10, 2011

GREAT MAN OF ALL TIME- NELSON MANDELA

"It is better to lead from behind and to put others in front, especially when you celebrate victory when nice things occur. You take the front line when there is danger. Then people will appreciate your leadership". - Nelson Mandela


The truth is that Nelson Mandela was the first Black President of South Africa and he was one of the most instrumental figures that helped to end apartheid in South Africa.

The difference between most of African leaders and Great leaders unlike Mandela is that the their vision in politics means thinking about having a big house, a big car and lots of possessions; while Mandela vision means change for people, even if change is uncomfortable or outright painful as long it makes difference for the benefit of all stood for that.

Let us review the Best Quotes from Nelson Mandela Leadership


“A good head and a good heart are always a formidable combination.”

“After climbing a great hill, one only finds that there are many more hills to climb.”


“I learned that courage was not the absence of fear, but the triumph over it. The brave man is not he who does not feel afraid, but he who conquers that fear.”

“If you talk to a man in a language he understands, that goes to his head. If you talk to him in his language, that goes to his heart.”




“There is no passion to be found playing small - in settling for a life that is less than the one you are capable of living.”

“We must use time wisely and forever realize that the time is always ripe to do right.”


Then What do you admire the most about Nelson Mandela leadership?


The Father

The Father who does good for his children and doesn't spare rod. Understand and practice his principles. The most immaculate leader, every nation has known and benefited from his superior morals. Oh I wish we could have more of Nelson Mandela's leadership characters. World would be a better place... —GuestIsaac Hlakane


A Strong Black Leader

Nelson Mandela is a strong black man and a great leader. I am sharing the history of his life with my children.I truly at admire Mr Mandela's leadership and determination. He has shown the way, not just for Africans but for all people. —GuestVictoria N Pendleton


Unselfish Leader

What a man I didn't think anyone could match what this guy did. We are free because of him. I mean we walk tall now and equality is now immense in our country. —Guestmasoga moses


He is the Greatest

He gave his life for us ... in time, he stopped the brutality the Whites had done to us. Had he not been here we would be as free as we are this day. SIYABULELA TATA. —GuestGogo Molema


The Best President

He was the best president and I thank God for [his presence] our country.  —Guestrobin ndamane


Bravery, Courageous and Devoted

Not everybody can give his life for people they do not know. Papa really is a man. —Guestmokopotsa lehlohonolo


One Of The Strongest Man In South Africa

Nelson Mandela is a very good man who helped his people and country. He went to jail for 27 year for that. People need him and he needs the people too. May he live forever! —Guestlillian


What Do I Admire Most.

His leadership style, his humbleness, his vision and his persistence to hold on irregardless of the challenges he was facing. He has lived his purpose and his soul is in peace. He is truly a blessing to us all. —GuestThabie Ndlovu


Freedom Fighter

[Mandela gave us] Freedom for all Africans not only south Africans blacks but also whites, so I do admire his sense of responsibility. Mandela empowered his peopleand history will give to him the place he deserves. May [God] bless his soul and his days in this world. He is a lover of peace. May his legacy be taught around the world, and I mean by that [allow] the children to learn about peace and how to eradicate injustice. Thanks to Nelson Mandela for showing to the world how to fight for freedom and how to love. —Guestsamba


An Amazing Hero

Nelson Mandela was a great man. If he was not born, none of us would have a happy life. —GuestLikhwa Tsepang Maphosa


One of the Best in the History of Today

We really should admire Nelson Mandela because he stopped the apartheid and he helped the South Africans.... Now let me do my paper on Nelson Mandela before i get in trouble..... —GuestHayvon Brown


Together We Can Do More

Nelson Rolihlahla Mandela was the best president South Africa could ever had. It took a man like him to fight for what he believed was right, it's not everybody who can do that. We are free today because of his passion, love and understanding about his country. He played his part (of being the president of South Africa) in an excellent and appropriate manner. May all the other leaders to follow take note and do more than he did. —Guestmillicent mogoane


He is Great Man

He spent 27 years in prison and he did not lose force. he has help me to believe in real humanity and dignity. He is a great man. —Guesttobiloba


He is a Hero

I admire Madiba for his determination, dream, and perseverance to change so that all have a good life. Not all of us could persevere in jail for 27 years for people you don't know, or die for South Africa. I know that I'm not so capable. —Guestprecious mmatli


Long Live Mandela, you are a great leaders and put the wounds of the past behind, without repressing them, in order for South Africa as a nation and as the entire world to move forward with grace and forgiveness. That is an extremely rare capacity and I think it is almost unknown. I once say again Nelson Mandela you are one of the stunning examples of our time.

Saturday, July 9, 2011

WAMACHINGA VS SERIKALI TANZANIA

Wamachinga na Harakati za Kujikomboa au ni harakati za kuwakomesha wengine?

Maswali haya wameulizwa na waandishi wengi sana wa habari kuhusu wamamchinga zidi ya Serikali

·        Je ni nini chimbuko la wamachinga?
·        kwanini 'wamachinga' wanakuwa ni tatizo ?
·        je huduma wanayoitoa inatakiwa na wananchi au haitakiwi ?
·        Ni njia gani zinazoweza kufanyika ili tatizo ligeuzwe ni fursa ya kiuchumi kwa manufaa ya wote? 
·        Je wa wafanyabiashara hao ni wa rika gani wanafikia wangapi hivi sasa?

Ni ukweli kuwa wamachinga ni wachuuzi waliozagaa katika maeneo tofauti wakifanya shughuli zao kiholela ambao waiibuka kwa wingi miaka ya 1980s wakati wa sera za Ruksa. Ni ajira ambayo inaweza kusemwa sio rasmi kama hawalipi kodi lakini kama wanalipa Kodi ni ajira Rasmi kwani taifa linafaidika na kodi yao na kwa msingi huo, na kwa upande mwingine na wao wnafanikiwa kupata riziki inayowasaidia kuendesha maisha yao

Idadi ya Wamachinga “nifikiri” ni  zadi ya wafanya biashara milioni moja: kwa upande mwingine kama ajira zaidi ya Milioni moja zimetengenezwa hapa, taifa limepunguziwa mzigo wa kuwatafutia ajira vijana hao.

Kwa nini wamamchinga wengi wanazagaa sana?
Nafikiri tuyaangalie maeneo ambayo pengine serikali wamewapangia hawa wamamchinga; je Maeneo  hayo yanajitosheleza?  Je yanavutia kibiashara, je kuna usafiri wa kuweza kuwaunganisha wafanya biashara hawa na wateja?

Je wakifukuzwa na wakakosa kuingiza ridhiki hata ya shilling mia moja nini kitatokea?
 Serikali inatakiw akuwa makini kwani, Nafikiri wamachiga wengi kama watafukuwza bila kupewa msaada woote, na kubaki kuwa hawana kazi,watagueka vibaka na kuliletea taifa  na raia wake.

Je serikali kuwafukuza wamamchinga ni suluhisho la tatizo?
Kuwaondoa wamachinga kabla ya kuwaandalia maeneo mbadala ya kufanyia biashashara zao ni mfumo mbaya wa namna serikali isivyojali maisha ya watu wake. Hakuna ustaarabu ulio bora zaidi duniani zaidi ya ule wa kujali uhai wa mtu kwanza kabal ya kumpokonya rizika yake. Wenzetu walioendelea wana progam kama kuwalipa raia wao ambao kwa namna moja au nyingine wameshindwa kufanya kazi “ unemployment Payments” au msaada wa chakula kwa familia za kipato kidogo “ food stamps” hata nyumba za watu wenye vipato vidogo “ low income Housing” sasa tunapowafukuza wamamchinga tunawapa msaada gani? Zaidi ya askari Mgambo kuwapora Mali zao

Tunaiomba serikali pamoja na kufanya maamuzi ya kuwaondoa wamachinga bila utaratibu makini, bado ina nafasi ya kuhakikisha inaboresha mazingira ya machinga hao kufanya biashara huko walikopelekwa, malalamiko ya machinga yanayoendelea hadi sasa kuwa huko walikopelekwa palikuwa tayari pamenunuliwa na baadhi ya watu ambao si wafanyabiashara ni mfano mbaya wa utekelezaji wa zoezi hili na serikali inapaswa kuwajibika katika hilo mapema iwezekanavyo.

Je mfumo wete wa elimu ya msingi inatusaidia katika kutatua tatizo la wamamchinga kuzagaa zagaa?
Nafikiri tunahitaji (innovative education system) mwanafunzi anayehitimu elimu ya msingi au sekondari asiwe tegemezi na badala yake awe mbunifu kwa maendeleo yake binafsi na kwa  Taifa. Zama hizi  zinahitaji hat kam ni mmachinga  inapaswa kuwa mbunifu. Tusitegemee wachinga bila ubunifu katika hizi zama za sayansi na teknolojia.

Kama taifa tutaweza kuuwezesha mfumo wetu wa elimu ukawafundisha vijana wetu Sayansi na teknolojia hii itakuwa ndiyo njia pekee ya kuokoa nguvu kazi inayoendelea kupotea kwa kujiunga na mfumo maisha wa machinga nchini Tanzania.

Je yanayotokea sasa sehemu mbali mbali za wamachinga kupigana na polisi na kuharibu mali za watu wengine hata kuiba ni sahii?
Katika jamii ambayo mambo yake mengi yako shaghalabadhala saa zingine inaonekana ni uonevu na dhuluma kuanza kukamata wavunja sheria wadogo wadogo wanaokidhi haja zao kila siku za. Tatizo hakuna  hakuna mipango madhubuti na mibadala ya kusaidia na kuwafanya wamachinga wajisikie kuwa wanatakiwa kubadilika na kufanya biashara zao kwa taratibu zinazoeleweka; kinachotokea kila tatizo likijitokeza na mapigano kuumizwa na mali kuharibiwa;


Serikali inatakiwa ifanye nini?
Ni ukweli ambao haukwepeki kuwa nchi imeshindwa kutoa ajira kwa vijana na vijana wameamua kujiajiri wenyewe kwa kuuza chochote kile wakipatacho mitaani.

Nakubali kabisa kwamba kitendo cha wafanyabiashara ndogondogo kuamua kufanya biashara zao sehemu yoyote wanayotaka na kujenga vibanda vyao vya biashara sehemu yoyote bila kuzingatia mipango miji ni ukiukaji wa sheria na taratibu za nchi kuhusiana mipango miji.

Kwa hali hiyo suala la biashara ndogondogo ni suala la maisha.
Kwa mtazamo huo tatizo la Wamachinga ni pana kuliko kuwavunjia vibanda vyao na kuwahamishia sehemu maalumu. Ni suala ambalo linatoa wito wa kurekebisha mfumo mzima wa kiuchumi na kijamii tulionao.

Ni suala ambalo linaitaka Serilaki kusimamia utekelezaji wa sheria na kutumia mbinu zote ili kuepusha hasara kwa raia wake. Ni bora kukinga kwa kutumia busara kuliko kuboboa kwa sababu za siasa;
Kwa nini tusiwe tekeleze sherai ya kuwazuia kujenga vibanda sehemu ambazo sio stahili?, tukiweza kuzuia ujenzi ni utu kuliko kuliko kumbomolea hata kama anastahili kubomolewa kwa kukiuka taratibu.