WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, May 16, 2011

TATIZO LA MHESHIMIWA DR. MAGUFULI NI NINI HASA?


                         Dr. John Pombe Magufuli

Kumekuwa na kilio kutoka kwa watendaji ndani ya Wizara ya Ujenzi ambayo Mheshimiwa Dr.Maguful anaongoza na kwa watendaji wengine nje ya wizara yake kama vile, viongozi wa manispaa zinazounda jiji la dare s salaam na hata pengine kutoka kwa wananchi kuhusu  utendaji wa Waziri Magufuli wakilinganisha utendaji kazi wake na Ubabe;

Swali amabalo mimi najiuliza je kama Waziri Dr. Magufuli utendaji wake unaonekana ni wa ubabe ni kwa nini?  Au watendaji wetu wamejenga mazingira ya kufanya kazi zao bora liende bila umakini wa kuzingatia sheria? Je kama Waziri anatekeleza Majukumu yake kisheria na sheria hiyo ili ifanikiwe inahitaji nguvu za ziada je huu ni ubabe?

Nafikiri umefika wakati ambao kama haturidhiki na utendaji kwa mantiki hii wa Mheshimiwa Dr. Magufuli na tunajua kabisa anakwenda kinyume na maadili ya uongozi, kinyume na sheria inayompa mamlaka ndani ya uwezo wake kama waziri hebu tuwe wakweli na tuyaainishe mapungufu ya ubabe huu ili hoja zetu ziwe za msingi; uropokaji na kusema sema tu bila kuwa na vielelzo nafikiri kama Waziri anatekeleza Majukumu yake kisheria na kuzielewa sheria hautapunguza kasi ya utekelezaji wake hata kama utakuwa wa ubabe; na tukumbuke kuwa binadamu bila kumshikia bango hasa kwetu sisi na nchi zetu hatutafuata sheria katika maisha yetu ya kila siku;

Hata mheshimiwa Rais Jk ameona hili ndio hata sasa ameanza kuwa mkali dhidi yenu ninyi watendaji wa serikali na kuwaeleza wasioweza kufanya kazi kwa kufuata sheria na maadili ya utumishi wa Umma wajiondoe; kauli amabazo zilikuwa hazipo; wakati wa kubebana umepita; tukitaka kuendelea lazima mambo ya kesho tuyaone leo na tusiyafumbie na kuyaonea aibu, hata kama utekelzaji wake sasa utaonekana mbaya lakini kesho kila mtu atafurahia; ebu jikumbushe ujenzi wa sehemu ya barabara ya ubungo –kimara mpaka kibaha; leo tunasema nini bado tunasikitika au tunafurahia hatua hiyo kubwa ya maendeleo?

Tuwe wakweli tuwajibike inavyotakiwa, tusimamie sheria ili kesho sheria isimfanye kiongozi mwingine kuonekana mbabe wakati akitekeleza mapungufu ya jana.

Sunday, May 15, 2011

JE TUWAFANYE NINI WANASIASA?

                            Utajiri wetu ni mkubwa lakini?

Siasa ni sayansi ya utengenezaji wa maneno matamu matamu ambayo yanatumika katika kuibadili akili ya wananchi ili waweze kukubaliana na kikundi Fulani ambacho kimejipanga kisera ili kiweze kupata nafasi ya k utawala, ambacho mara nyingi huwa na mipango  mitamu ya kinadharia zaidi ya maendeleo kwa wananchi.
Kutokana na sera zao wakati mwingine upangaji wa hoja na utamu wa maneno yao hupelekea kuaamini kuwa wanasiasa ni watu wanaojua kila kitu. Na kila mtu anadhani hakuna mtu anayeweza kufanya kitu kwa maslahi ya nchi bila kuhusisha siasa.  Kinachoendele hapa ni dhana tunayoijenga kuwa mwanasiasa umekuwa bingwa wa kujenga hoja, wanataka kuona umekuwa bingwa wa kutatua matatizo na kuwaletea wananchi asali na maziwa.

Siasa ili inafinikwe lazima ijengwe chini ya msingi wa sera, na sera hizo lazima ziwalenge  kwa watu Sera zote zinapotungwa ni kwa ajili ya watu, lakini tatizo ni kubwa wanasiasa wanawarubuni watu, hivyo  kuvurugu mipango ya maendeleo; Ni wazi kwamba mhemko wa kisiasa, umeikumba nchi yetu; Kila kitu tumekifanya ndani ya siasa, hili ni tatizo kubwa. Siasa uchwara tunazipa nafasi na kujikosesha maendeleo.  Kutokana na kushindwa   kuwaelimisha watu kuhusu tabianchi, ufahamu wa maisha, mbinu za kukabiliana na majanga na mengineyo, moja kwa moja vinasaliti jamii 

Tanzania ni nchi maskini ni lazima tuwe na viongozi ambao kweli wanasaidia wananchi. Muda wa kukubali kuendelea kudanganywa umekwisha, ni lazima sasa sisi kama wananchi tuwahukumu wanansiasa kutokana na namna wanavyotufanyia mambo, wanavyotufanya sisi masikini kana kuwa hatujui nini kinaendelea.  Kauli mbiu yetu iwe kama hawatujali kwa maendeleo  na kutuzidishia umasikini, inatunapasa kuachana nao tumechoka kuendelea kudanganywa..

Leo hii kigezo chetu cha maendeleo ni nini?  Tunayaangaliaje maendeleo ya wananchi? Kwa nini kuna tofauti kubwa kati ya mtu na mtu? Je tukisema wananchi hawajitumi kwa maendeleo yao je tumewawezesha?

Kipimo chetu cha maendeleo ni kuangalia maisha ya jumla au  ya mwananchi mmoja mmoja? Je tunayalinganisha maendeleo ya wananchi wetu kwa kuangalia uwezo wao wa kuzalisha mali  na wanatumia vifaa gani, na vinahusiana vipi na kuimarisha afya zao? je thamani ya fedha yetu, kiwango cha elimu na uimara wa sekta za viwanda  tunaviangaliaje katika kumletea maisha bora huyu mwananchi? Au tunaridhika na Msongamano wa magari na watu katika miji yetu mikuu ikianzia darn a miji mingine na tunaridhika kuwa  hii ishara tosha ya maendeleo  na maisha bora?

Je kuna uwiano kati ya uimarishaji wa bidhaa za ndani na zile zinazokuja toka nje ya nchi? Au tunaridhika na kilimo cha duni cha wananchi serikali kupitia wanasiasa hatuoni sababu ya  kuwasaidia wananchi  kuwajengea uwezo wa kupata masoko; Uwezo wetu wa kuwatafuti masoko yenye tija umefia wapi? Bila dhana bora na elimu nzuri ya kilimo tunaelewa kuwa tumepania kuwamaliza kabisa  wananchi kwa kuwaletea ushindani  wa kupambana na biashara kutoka nje  na hivyo kuwanjima uwezo wa ushindani katika midhani sawa.

Je Tanzania ya leo ni chama tawala pekee ndicho kinachoongoza kutoa ahadi ambazo baada ya uchaguzi zinakuwa mzigo ndani ya chama? Je vipi vyama vya upinzani vimefanikiwa kukibana chama tawala katika kuhakikisha kuwa wanatekeleza ahadi zake kwa wananchi? Ni ukweli ambao haufichiki kuwa wanaotawala ndio wenye meno ya kutafuna, basi la msingi wabanwe watekeleze ahadi zao; kwa msingi huu watawala kupitia vyama vyao wasipobanwa kitakachoendelea na tunakiona kikiendelea kutokea ni kuwa taifa letu litaendelea kuzalisha wafanyabiashara feki na bidhaa feki. Elimu na walimu feki, mitihani feki, wahitimu feki, na vyeti feki. Hospitali zitaendelea kutikiswa na dawa feki. Mwisho wa siku wimbo wetu utakuwa kila kitu ni feki  

Hivi sasa tunaona vyama ushindani vikipita sehemu mbali mbali kwa kauli ya kuhamasisha ubovu wa serikali inayotawala; swali la msingi hapa ni kweli wanachokisema ndicho wanachokiamini na kuwa tayari kuwaletea wananchi maendeleo punde wakipata nafasi ya kuongoza?

Au tuendelee kuamini kuwa hii ni siasa kila mtu anatafuta ulaji kwa staili ya kuonyesha mabaya ya mwenzake? Je hakuna jema ambalo serikali inayopingwa sasa hivi imewafanyia wananchi? Nikifikiri haya yote ninaishia kwa kusema kuwa TUWAFANYE NINI WANASIASA KWANI HAWAAMINIKI HATA KIDOGO; wanaendelea kuwafanya wananchi kama watoto wa kuku watanyonya kesho wakati hakuna uwezekano wa kuwatoa katika umasikini uliopindukia;

Utajiri huu wote tulio nao kwa nini tunaendelea kuwa masikini inauma sana wanasiasa mnatutesa jamani;