WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, March 31, 2011

UWAJIBIKAJI WA PAMOJA WA SERIKALI

KAULI ZINAZOTOFAUTIANA MIONGONI MWA WATENDAJI WAKUU WA SERIKALI NI WAJIBIKAJI WA PAMOJA?


Uwajibika wa pamoja kati ya watendaji wakuu wa serikali ni dhana muhimu katika utekelezaji wa majukumu na sera za serikali;
Kila kiongozi anamchango ambao unaweza kusaidia kuleta  mabadiliko katika jamii, la msingi katika kufanikisha hilo kunahitajika kuwepo kwa njia makini, kufuata taratibu na kuwa na mawasiliano ya hali ya juu (effective Communication) miongoni mwao. Ni muhimu kuhakikisha kuwa hoja zao na utekelezaji wao unachambuliwa katka vikao muhimu vya pamoja (in Camera) na kama unafaa  utumike  katika kutekeleza majukumu yao ( ministry Responsibility) katika wizara na idara zao husika katika kuwaleta maendeleo wananchi wake.

SERIKALI yoyote yenye mafanikio ya uwajibikaji wa pamoja ni ile ambayo inaheshimu misingi ya utawala bora, ambayo moja ya nguzo zake kubwa ni nidhamu ya utendaji wa kazi na mahusiano mazuri ya kazi kati ya watumishi, wakiwamo viongozi wa kada mbalimbali.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa JK katika moja ya mikutano yake pamoja na watendaji wake wakuu, amewakumbusha wateule wake kuhusu uwajibikaji wa pamoja (collective responsibility) katika kuongoza nchi, akisisitiza kuwa uwajibikaji huo unaelezwa kwa ufasaha katika Hati Maalum (Instrument) ya Majukumu ya kila Wizara. Katka msisitizo Rais Kikwete alisema kuwa
·        Uzoefu unaonyesha kuwa Mawaziri wengi ni wazito kufanya mawasiliano na wananchi hata pale ambako Wizara imefanya mambo mengi mazuri. Hivyo, Mawaziri muwe mstari wa mbele kuelezea mafanikio ya utendaji wa Serikali katika Wizara zetu,” ameelekeza Rais Kikwete na kuongeza: 
·        Lazima ujengwe utamaduni wa kudumu wa kuwasiliana na wananchi wote ambao ndio waajiri wetu kupitia kura zao. Mawaziri wote tumieni Vitengo vyenu vya Mawasiliano na vyombo vya habari kwa ustadi ipasavyo,
·        Ni rahisi kunyoosha vidole, na kuwabandikia  watu wengine lawama za matatizo haya.


JE KUWEPO KWA TOFAUTI ZA KAULI KATIKA SIKU ZA KARIBUNI MIONGONI MWA WATENDAJI WAKUU WA SERIKALI INAONDOA UWAJIBIKAJI WA PAMOJA AU INAIMARISHA UWAJIBIKAJI;

Katika siku hizi za karibuni kumekuwako sana na kutofautiana kwa kauli miongoni mwa watendaji wakuu wa serikala huhusa mawaziri kuhusu hoja moja ambazo zinaishia kuwa na mielekeo miwili tofauti  na misimamo tofauti;

kuhusu swala la loliondo waziri mwenye dhamana ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Haji Mponda ilimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha kusitisha kwa muda utoaji wa huduma hiyo hadi itakapojiridhisha kwamba dawa inakidhi ubora na inatolewa katika mazingira safi; agizo hilo likiwa mbioni kutekelezwa jana Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisema Serikali haina tena mpango wa kuzuia huduma hiyo kwa kuwa inahusisha imani za watu

kuhusu bomoa bomoa waziri mwenye dhaman  Dr John Pombe Magufuli  alijikuta akipigwa stop na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati akihutubia mkutano wa hadhara alipomuagiza, waziri  John Magufuli kuwa asitishe mara moja ubomoaji wa majengo yaliyo katika hifadhi ya barabara hadi Baraza la Mawaziri litakapoamua vinginevyo. Kama haitoshi Mheshimiwa Rais JK alipotembelea wizara ya Ujenzi alimuagiza Waziri Magufuli kuzingatia kile alichokiita “utu” na “ubinadamu”

kwa nini Rais Kikwete na Waziri Mkuu Pinda waliona vyema kumkaripia Waziri Magufuli hadharani, tena kwa kauli za kumdhalilisha mbele ya wafanyakazi na wapigakura wake ili aonekane kama mtu katili asiye na utu wala ubinadamu? Kwa nini hoja na kauli zao hazikupelekwa kwanza katika Baraza la Mawaziri kama kweli walikuwa na nia ya kufanya hivyo? Na kama wanaona kuwa sheria inayosimamia hifadhi za barabara haifai kwa nini wasizungumzie haja ya kupeleka muswada bungeni ili sheria hiyo iwekewe “utu” na “ubinadamu” badala ya kumsingizia waziri huyo kwamba anatumia ubabe”?


HIVI SERIKALI HAINA MGAWANYO WA MAJUKUMU KWA MAWAZIRI WAKE
 Wakati huo huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Mathias Chikawe, alisema ni kosa kwa mawaziri kupingana hadharani na kuongeza kuwa kama kuna mwenye dukuduku kuna namna ya kuwasilisha maoni yao. Kwa mujibu wa Chikawe, taratibu hizo ni kwa mawaziri husika kuwasiliana na kushauriana na inapotokea anayeshauriwa haelewi, upo utaratibu wa kupeleka maoni hayo kwa Waziri Mkuu.

maswali ya kujiuliza sasa  je na pale ambapo Waziri Mkuu na hatimaye Mheshimiwa Rais hawaoni umuhimu wa kutumia vikao vya Baraza la mawaziri katika kurekebisha jambo lolote na kumkosoa waziri mwenye dhaman mbele ya watu bila waziri kujua nini kinaendelea;
Je kuna umuhimu gani wa wale ambao wako chini yao kutekeleza huo uwajibikaji wa pamoja?  Kama waandishi wengi walivyo hoji, Je Kwa nini hoja na kauli zao  hazikupelekwa kwanza katika Baraza la Mawaziri kama kweli walikuwa na nia ya kufanya hivyo? Na kama wanaona kuwa sheria inayosimamia hifadhi za barabara haifai kwa nini wasizungumzie haja ya kupeleka muswada bungeni ili sheria hiyo iwekewe “utu” na “ubinadamu” badala ya kumsingizia waziri huyo kwamba anatumia ubabe”?  je  kumkaripia Waziri Magufuli hadharani, tena kwa kauli za kumdhalilisha mbele ya wafanyakazi na wapigakura wake ili aonekane kama mtu katili asiye na utu wala ubinadamu inaimarisha uwajibikaji wa pamoja au inabomoa?
Nafikiri viongozi wetu wengi wanatakiwa watumie muda wa kutosha kujifunza faida za” effective communications” na wapi wanastahili kusema hoja gani kwa faida ya nani?

Kama taifa tutuweza sana kusonga mbele pale tutakapo weza kuondoa kabisa hulka za kisiasa katika kutekeleza maendeleo ya wananchi, busara na hekima ni silaha ya uwajibikaji wa pamoja 

Tuesday, March 22, 2011

JE SERIKALI YETU TANZANIA INAYO WASHAURI WAZURI?

JE MATATIZO YANAYOENDELEA KUTOKEA TANZANIA LEO: JE RAIS WETU AMEKOSA WASHAURI WAZURI?


Sehemu ya Pili



katika hizi siku za karibuni kumeanza kujitokeza maandamano yenye “sura ya amani” yakiwa na kibwagizo cha kudai maisha bora kwa watanzania, ambayo yanaendeshwa na CDM yakishinikiza serikali ya CCM kutatua kero za wananchi kwa haraka iwezekanavyo. Ikumbukwe kuwa Tangu 1989, mapambano ya raia yasiyotumia nguvu yamesababisha kuvunjika kwa utawala wa kikomunisti wa chama kimoja cha Urusi, vyama Ulaya ya mashariki, Jamuhuri ya Baltes na Mongolie na muungano kwa amani wa Ujeremani na kukomesha utawala wa ubaguzi wa rangi wa Afrika kusini. Ijapokuwa mapambano hayo, pengine yalikuwa na vifo (Birmanie 1988, Chine 1989), kuna tofauti kabisa na mapinduzi ya kale kama yale ya Amerika ,Ufaransa, Urusi, Uchina yaliyogupikwa na mauaji mengi zaidi. Pembeni ya maandamano makubwa yanayoonekana wazi ya kutafuta mabadiliko ya utawala, kuna vyama vya kisiasa ambavyo vinatumia mwanya wa kuuza sera zao kwa wananchi dhidi ya chama kilicho madarakani kwa msingi wa kuwa kimeshindwa kuatatua kero za wananchi. Je chama ambacho kipo madarakani kinatakiwa kujipanga vipi? Ni ukweli ambao haufichiki kuwa Rais kama kiongozi wa juu kabisa katika nchi anatawala kwa msaada mkubwa wa washauri wake; Je kama washauri wameiona hali hii wanamshauri nini?

Swali nyingine ninalojiuliza ni kitu gani kitapelekea uwepo wa maandamano haya yenye kibwagizo cha amani (sauti ya umma)? je yanakuja kwa sura ya kudai nini? ni uhuru wa watu, usawa , maendeleo mazuri ya kwa wananchi wote?, au ni sehemu tu ya kuanzisha uvunjaji wa amani miongoni mwa watanzania? ama kuna alama gani za ki-historia au za nyakati hizi za siasa, uchumi, jamii, utamanduni, zinazo onyesha kuwa jamii ya kitanzania imefikia mwenendo wa maisha ya kutojali na kutotii serikali yake iliyochaguliwa kihalali? Hapa namnukuu mwanafalsafa Jean Jacques ROUSSEAU (1712 – 1778) alivyoandika kwamba “wanainchi ni lazima waheshimu viongozi wao walio na majukumu ya kutoa amri kwa ajili ya wote. Serikali inayo haki ya kupiga vita watu wote wasiotii amri zake na kuwahukumu kifo. Pia, serikali inayo mamlaka ya kuamru watu wajitoe muhanga kwa ajili yake.”

Pengine tuwaulize washauri wa Mheshimiwa Rais kuwa je mabadiliko gani yametokea ndani ya jamii iliyokuwa imetulia bila msisimko wa kisiasa, na leo hii imekuwa tayari kuungana na vyama vya siasa katika maandamano yanayoendelea sehemu mbalimbali hata wengine wakiwa tayari kuyapoteza maisha yao, kwanini?
·        Kujitokeza kwa wingi katika maandamano haya ya amani ni kielelezo hali halisi kuwa wananchi wamechoshwa na:
·        Ugumu wa maisha na wakati huo huo kundi la watu wachache wanafaidi rasilimali za nchi na watoto wao wakifaidi elimu bora nje ya nchi
·        Wananchi wanasikitika kuona kuwa taifa lenye rasilimali nyingi na za pekee dunia linaendelea kuwa masikini na watoto wa taifa hili wakiendelea kuwa wapumbavu kwa kukosa haki ya msingi ya elimu

 Ni ukweli siopingika kuwa wananchi wanachoshwa na hali hii ndio maana kiongozi mwinigine yeyyote anayejitokeza  na kuwagusa katika kuboresha maisha yao, wanakuwa tayari kumkimbilia na kuamaini kuwa ataleta khali nzuri ya maisha hata kama hali haitabadilika; Inasikitisha miaka 49 ya uhuru Tanzania bado  haina umeme wa uhakika; maji safi na barabara, na kadhalika; wananchi wamechoshwa na umasikini katika nchi yao tajiri; Matatizo yote ambayo yanajitokeza leo wananchi wanona  in kazi ya mikono Serikali na chama kilicho madarakani;

Rai yangu washauri wa Mheshimiwa Rais wetu wawajibike ipasavyo kwa faida ya taifa na sio kwa masilahi ya kikundi kidogo cha watu; na mheshimiwa rais akiona ushauri wao hauna tija kwa wananchi basi awawajibishe kwani taifa hili lina rasilimali kubwa sana ya wataalamu ambao wako tayari kuifikisha nchi mahali pazuri sana kwa manufaa ya wote.


Mungu Ibariki Tanzania na utuepushe na fikra zozote za kuvunyika kwa amani 

Saturday, March 19, 2011

JE SERIKALI YETU TANZANIA INAYO WASHAURI WAZURI?

JE MATATIZO YANAYOENDELEA KUTOKEA TANZANIA LEO: JE RAIS WETU AMEKOSA WASHAURI WAZURI?
                           Sehemu ya Kwanza

Tanzania tumebarikiwa kuwa na uchaguzi mkuu ambao ulifanyika kwa amani bila vurugu zozote za umwagaji wa damu, pamoja na kasoro hapa na pale, ambazo zilijitokeza kabla na baada ya upigaji kura;ambazo zilipelekea Chama cha Maendeleo na Demokrasia kutokuwa na imani na tume ya uchaguzi na hatimaye kususia matokea kwa msingi kuwa uchaguzi hakuwa huru na matokeo ya urais YALICHAKACHULIWA ili kumsaidia mgombea wa CCM kushinda uchaguzi huu  mwezi October 2010;

Maswali ya Msingi hapa Je washauri wa rais wa siasa , uchumi na huduma za jamii, na kadhalika  wanamshauri Rais wetu nini katika kushughulikia kero za wananchi na katika kutimiza ahadi alizozitoa wakati wa kampeni? Au wanakuwa kama bendera wakiogopa kusema ukweli kwa msingi wa kuogopa kupoteza ajira zao na wakijua kuwa kazi zao ni za msimu mfupi?

Baada ya uchaguzi tumeoona vyama vya upinzani vikiongozwa na CUF na CHADEMA wakiwahamasiha wafuasi wao katika madai ya kuandika Katiba upya , kilio hicho cha madai ya katiba mpya kilipata majibu kutoka kwa msheshimiwa Rais JK kuwa serikali yake iko tayari kuridhia mabadiliko hayo.

Tatizo nyingine ambalo bado limeendelea kuliweka taifa mahali pabaya ni pamoja na kukidhiri kwa vitendo vya rushwa (ufisadi uliobebea) ambao bado unaendelea kufanya na viongozi na washirika wao ndani ya serikali; tatizo hilo kwa hivi sasa  linahusishwa na tatizo sugu la kukosekana kwa umeme na wananchi kupinga kwa sauti moja malipo ya kampuni ya kufua umeme wa generator Dowans. Kama kweli huu ni mradi wa wazito ndani chama na serikali basi itafika mahali ambapo wananchi watalazimika kufuata msimamo wa Karl Marx (1818 – 1883) na Friedrich ENGELS (1820 – 1895) wanasema kwamba matajiri na wanaoshikilia vyombo vya utajiri mara nyingi hutumia nguvu kwa kukuza na kulinda mali zao. Ila, ungandamizaji wao unapofikia kilele, masikini wana haki ya kuleta uasi mkubwa kwa mageuzi ya kiuchumi na ya kisiasa. Ndio maana leo tunaona kuwa wananchi wengi wameanza kusimama kiume na kuanza kudai haki zao; wakiitumia kauli mbiu kuwa “hutulipi Dowans” hata kama serikali itaishia kulipa kwa siri lakini kilio cha wananchi kimeshasikika; washauri mpo na umeshauri nini katika utata huu wa zabuni za mitambo hii?

Mauaji wa raia kadhaa huko  Arusha ambayo yalitokea baada ya wafuasi wa CHADEMA kufanya maandamano yaliyokuwa yakipinga matokeo ya ushindi wa Meya wa arusha kwa tiketi ya CCM. Mauaji hayo katika msingi wowote ule yameendelea kuchafua historia nzuri ya nchi yetu na kutukumbusha kile kilichofanyika Zanzibar miaka kadhaa iliyopita; katika hili, je washauri wa rais waliishauri serikali kutumia nguvu kuzima maandamano hayo? Kama ndio je walifuata msimamo wa Mwanafalsafa Machiavel (1462 – 1527) katika maamdishi yake alishauri kwamba viongozi watumie nguvu ili wabaki madarakani na kulinda heshima za nchi zao. Pia anaomba viongozi wawe wenye busara na itakapohitajika, wawe wakali kama simba. Je huu ndio ni msimamo wa serikali yetu? Au ilikuwa bahati mbaya kwa kukosekana kwa mawasiliano mazuri miongoni mwa Taasisi husuka? Je taratibu za gani zifuatwe ili kuepusha hali hii siku za usoni? Hili ni jukumu la washauri wa Mweshimiwa Rais pamoja na busara na uvumilivu wa viongozi wetu;

Kumekuwako pia na uharibifu uliotokana na mabomu yaiyolipuka  Gongo la Mboto ambayo yamesababisha wananchi zaidi ya 20 kupoteza maisha na mali pia, swali la msingi hapa je taasisi zetu zinazoshughulikia usalama zinawajibika vipi katika ukaguzi wa vifaa vyao na wanatumia utaratibu gani wa uhifadhi wa vifaa ambavyo vinaweza kuleta madhara yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa (Joto au baridi);je wanautaratibu wa kukagua vifaa hivyo kutokana na ukaji wa siku nyingi? Je washauri wetu wanamshauri Mheshimiwa Rais nini kuhusu uwajibikaji katika mazingira ya namna hii: Je katika kuhakisha kuwa hali hii haitokei tena je  washauri wa mheshimiwa Rais watamsaidiaje kwa faida ya watanzania wote?