WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, November 25, 2012

Picha zingine za watanzania New York walivyomuaga Jesca Emmanuel


Mchungaji Perucy Butiku akiongoza Ibada ya  kumuombea Marehemu Jesca Emmnauel na kuwafariji wazazi wake, ambapo pia alitumia fursa hiyo kuwakumbusha waombolezaji kwamba kila mmoja wetu anasiku yake atakayoitwa na  Mwenyenzi Mungu,  kama alivyoitwa Mtoto  Jesca, ni siku ambayo hakuna mtu aijuaye. Na kwa sababu hiyo akasisitiza  umuhimu wa kujiandaa. Ibada ilifanyika siku ya Jumamosi Bergen Funeral Home jijini New York.
 Mama mzazi wa Jesca  Bi. Doto akilia kwa uchungu mara baada ya kuona  mwili wa mtoto wake.
Baba  mzazi wa  Jesca, Bw. Emmanuel akilia kwa  uchungu mara baada ya kumwona mtoto wake, pembeni yake ni Shangazi wa Jesca, Bi. Rose
 Mdogo wake Jesca, Catherine akiwa ameelemewa na majonzi mazito kwa kuondokewa na dadayake, Catherine  aliwatia uchungu waombelezaji pale alipomuaga  Dada yake kwa  kutamka  "  Bye Jesca".
 Naibu Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi  akimuaga Jesca
 Brigedia Jenerali Maganga Mwambata Jeshi  katika  Ubalozi wa Tanzania nchi Marekani, akiaga. Brigedia Jenerali Maganga ni kati ya  Maafisa  wanne waliowakilisha  wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
 Balozi  Tuvako Manongi  akiungana na waombelezaji wengine kumuaga marehemu Jesca. Baada ya  ratiba ya kuaga, Balozi Manongi aliwashukuru watanzania kwa ushirikiano, upendo na mshikamano mkubwa waliouonyesha wakati wote wa kipindi cha maombolezo ya msiba huo na akawasihi kuendeleza umoja huo
  Bw. Emmanuel na Bi.  Doto wakiwa na mtoto wao, muda mfupi kabla ya sanduku kufungwa 
Sanduku lenye mwili wa Jesca tayari kwa Safari ya kwenda Bumbombi- Tarime Tanzania kwa Mazishi.

Watanzania wanaoishi jijini New York na Vitongoji vyake wakiwamo wawakilishi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, jana Jumamosi, waliungana na Familia ya Bw. Emmanuel Alfred Swere na Bi. Doto na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, katika Ibada ya kumuaga Jesca Emmanuel (12) aliyefariki ghafla Jumapili iliyopita.

Ibada ya kumuaga Jesca ilifanyika Bergen Funeral Home na iliongozwa na Mchungaji Perucy Butiku. Mazishi ya Marehemu Jesca yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne katika kijiji cha Bumbombi- Tarime Tanzania.

Raha ya Milele Umpe Eee Bwana na Mwanga wa Milele Umuangazie Apumzike kwa Amani. Amina

source; vijimambo blog

No comments:

Post a Comment