WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, November 21, 2012

Simba 'yamnasa' mrithi wa Kaseja


Juma Kaseja akiwa kwenye mazoezi.
MABINGWA wa soka Bara, Simba wamethibitisha kufanya mazunguzo na kipa namba moja Rwanda, Jean Claude Ndoli ili kuchukua nafasi ya kipa mkongwe Juma Kaseja.
Ndoli, anacheza klabu ya APR ya Rwanda na ndiye mlinda mlango wa kutegemewa wa timu ya Taifa Rwanda, maarufu kama Amavubi.
Mazungumzo na kipa huyo Mrwanda yamekuja siku kadhaa kumpita tangu mashabiki wa Simba wamtuhumu Kaseja kushuka kiwango na kufungwa mabao ya kizembe.
Habari za uhakika kutoka Rwanda, zimesema kuwa Simba imefikia hatua hiyo kufuatia kikao kilichofanyika wiki iliyopita na kuongozwa na Mwenyekiti, Aden Rage.
Taarifa zimesema, tayari Simba iliyopoteza mwelekeo kwenye mechi za mwisho mzunguko wa kwanza Ligi Kuu, wameshafanya mazungumzo ya awali na uongozi wa APR.
Kiongozi mmoja wa Simba ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini, aliliambia Mwananchi kuwapo kwa mazungumzo hayo na APR.
"Kweli, kuna mpango huo wa kumsajili Ndoli, lakini kwa sasa ni mapema zaidi kulizungumzia suala hili kwa vile kamati zote ndani ya klabu zimevunjwa," alisema kiongozi huyo.
"Mpango uliokuwapo siyo tu wa kumsajili kipa, bali hata wachezaji wengine. Tunatarajia kwenda Uganda kwenye michuano ya Kombe la Chalenji kuangalia wachezaji," alisema bosi huyo.
Kiongozi huyo alikiri kwamba, Kaseja anahitaji kupumzika baada ya kuichezea Simba mfululizo katika mechi za mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Akikaririwa na chanzo cha habari hizi, Ndoli alithibitisha kuwapo kwa taarifa za kutakiwa na Simba, ingawa alisema bado ni mapema kwa sasa.
"Nimepata taarifa hizi, sina tatizo kama viongozi wangu wataniruhusu kwenda Tanzania kucheza Simba," alisema kipa huyo.
"Mimi kwa sasa bado ni mchezaji wa APR, lakini naweza kuhama kama viongozi wataridhika," alisema zaidi Ndoli.
Mwananchi ilipomtafuta Kaseja ambaye pia ni nahodha wa timu ya Taifa Tanzania kuzungumzia uamuzi wa viongozi wake kufanya mazungumzo na Ndoli alisema hana la kuzungumza.
"Umesikia dada yangu, kwa sasa siwezi kuzungumzia mambo ya klabu kwa vile niko kwenye kambi ya timu ya taifa tunajiandaa na Chelenji," alisema Kaseja.
Aliongeza: "Hata kama kuna ukweli, mimi sina taarifa, huo ni uamuzi wa viongozi mimi siwezi kupinga."
Mwananchi

No comments:

Post a Comment