WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, November 23, 2012

Ratiba Ya Kumuaga Jesca Emmanuel







RATIBA YA  KUMUAGA MAREHEMU  JESCA EMMANUEL

Mhe. Tuvako Manongi, Balozi  wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, anawataarifu   watanzania wanaoishi  Jijini New York na Vitongoji vyake kwamba, Marehemu  Jesca Emmanuel (12) aliyefariki ghafla  Jumapili iliyopita ataagwa rasmi siku ya Jumamosi tarehe  24/11/2012.

Mahali ni :Bergen Funeral Service Inc,
114-30 Rockaway BLVD,
So, Ozone Park, NY 11420
Simu: 718-738-8383
        www. Bergenfuneral.com
Muda: Kuanzia saa  Tatu Asubuhi (9.00am) hadi  saa 
Sita Mchana ( 12.00 noon)
Tafadhali  tunaombwa sana kuzingatia muda, baada ya  ratiba ya kumuuga Mpendwa wetu  Jesca Emmanuel kukamilika,  mwili wa marehemu  ukisindikizwa na  wazazi wake utaondoka usiku wa  siku  hiyo ya Jumamosi  kwa safari ya Bumbombi- Shirati Tanzania kwa mazishi.


“Jesca,  wazazi wako, mdogo wako, shangazi yako, rafiki zako wanafunzi wenzako  na sisi sote  tuliokufahamu tulikupenda sana. Lakini  Mwenye-Enzi Mungu amekupenda zaidi. Bwana ametoa na  Bwana ametwaa jina lake  lihimidiwe. Amina”


Raha ya Milele Umpe Eee Bwana na Mwanga wa Milele Umuangazie apumzike kwa amani. Amina

UBALOZI WA TANZANIA  UMOJA WA MATAIFA

NEW YORK

No comments:

Post a Comment