WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, November 21, 2012

VIONGOZI WA UWAMSHO WAPUNGUZIWA MASHARTI YA DHAMANA



Na Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Inspekta Mohammed Mhina.

Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar leo imepunguza masharti ya dhamana kwa Viongozi saba wa Jumuiya mbili za Kiislamu Zanzibar, wanaokabiliwa na mashtaka ya kusababisha vurugu na kupelekea uharibifu wa miundombinu ya barabara mjini Zanzibar, leo tena wameshindwa kupata dhamana.

Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema kuwa uwamuzi huo umetolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo Mh. Ame Pinja, baada ya kukubali maombi ya Mawakili wa Watuhumiwa waliomba kupunguzwa kwa masharti hayo kwa wateja wao.

Watuhumiwa hao ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimam ZanzibarSheike Farid Hadi Ahamed na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Sheikhe Mselem Ali Mselemu na wenzao watano.

Inspekta Mhina amesema kuwa kutokana na uwamuzi huo, kila mshitakiwa sasa atatakiwa kuwa na wadhaminiwa wawili ambao ni watumishi wa Serikali na kwa kila mmoja awe na kiasi cha shilingi 500,000 tofauti na mashrti ya awali ya wadhamini watatu na kwa kila mmoja kwa kiasi cha shilingi milioni moja kwa kila mmoja.

Hata hivyo pamoja na kupunguzwa kwa masharti hayo, hakuna hata mshitakiwa mmoja aliyedhaminiwa kutokana na kukosekana kwa wadhamini ambao ni watumishi wa serikali.

Inspekta Mhina amesema kuwa Watuhumiwa hao ambao wanakabiliwa na kesi tatu tofauti za kuzusha ghasia na kupelekea vurugu katika maeneo mbalimbali ya mji wa Zanzibar, wamerudishwa rumande hadi desemba 4, mwaka huu kesi yao itakapotajwa tena.

Amesema wakati wote mahakama hiyo ikiiendelea, hali ya ulinzi nje na ndani ya Mahamakama uliimarishwa vya kutosha ambapo Makachero wa Jeshi la Polisi pamoja na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia na wale wa vikosi.vya Ulinzi vya Zanzibar

No comments:

Post a Comment