WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, October 13, 2012

PICHA ZA MSIBANI KWA MAREHEMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA RPC LIBERATUS BALLOW , PAMOJA NA SEHEMU WALIYO MUULIA



 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Everest Ndikillo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na tukio la kifo cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Liberetus Ballow usiku wa Kuamakia leo maeneo ya Kitangiri.                                     
 Nyumba ya Dorcas Moses mwalimu wa shule ya Msingi ya Nyamagana ambye alikuwa kwenye gari aina ya Rav 4 aliyepewa lifti na kamanda Ballow usiku kumrudisha kwake. Hapa Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Fredrick Katulanda akitoka kufanya mahojiano.
 Mtoto wa kaka yake Mwalimu Dorcas akiongea kuhusiana na tukio la Kifo cha kamanda Ballow ambapo yeye ndie alikwenda kufungua geti kwa ajili ya Mama yake Dorcas aweze kuingia ndani ila kabla ya kufungua ndipo aliposikia risasi ikipigwa.
                                     Hapa ni nyumbani kwa marehemu kamanda Ballow.
 Hili ndilo geti ambalo kifo cha kamanda Ballow kilipotokea usiku wa kuamkia leo wakati mwalimu Dorcas Mosese alipokuwa akirudi nyumbani kwa lifti ya gari la Kamanda Ballow.
                     Baadhi ya jamaa yake marehemu nyumbani kama walivyokutwa na kamera yetu.
Kwa picha zaidi bofya read more
                                                     Jamaa zake marehemu Ballow.
                   Waombolezaji wa kike wakilia kwa uchungu nyumbani kwa kamand Ballow leo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza RPC Liberatus Ballow ameuwa usiku wa kuamkia leo na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi katika eneo la Kitangiri karibu na Hotel ya Tai Five majira ya kati ya saa saba hadi nane.
Haya  yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa Mwanza Injinia Everest Ndikillo wakati akitoa taarifa za tukio la kuuawa kwa Kamanda Ballow.
Tukio hilo ambalo limeacha simanzi kubwa kwa wakazi wa jiji la Mwanza pamoja na familia yake huku watu wa kijiuliza kuhusiana aliyehusika na mauuaji hayo ya kikatili.
Taarifa ya Mkuu wa Mkoa zinasema kuwa Kamanda Ballow alikiuwa anatoka katika kikao cha harusi na ndugu yake aitwaye Sembeli Maleto kilichokuwa kinafanyika katika Hotel y a Florida na kish akumpelek amwanamke aitwaye Dorcas Moses Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Nyamagana maeneo ya barabara ya Kona ya Bwiru kwenda Kitangiri.
Walipofika getini kwa Mama Dorcas mara waliwaona watu wawili wakiwa wamevaa makoti ya PolisiJamii, Mama Dorcas alimuuliza Kamanda Ballow kama anawafahamu Kamanda akasema kuwa hawa na watu wa ulinzi wa Jamii wako doria.
Mara wale watu waliongezeka na kuwa sita wakaanza kama kuzozana wao kwa wao na  ndipo Kamanda alipowauuliza kuna nini, Mmoja wao akajibu hakuna kitu na ikapelekea Kamanda kutaka kutoka nje ila wale watu watatu wakaizingira gari ya Kamanda Ballow aina ya Rav 4.
Kamanda Ballow alipoona kama hali hewa inabadilika alichukua redio call ili aweze kuwa taarifu askari na ndipo wale jamaa walipompiga risasi kichwani nakupelekea kifo chake.
Taratibu za mazishi ya Kijeshi bado zinaendelea na nyumbani kwa marehemu ambapo mwandishi wa blogu hii amefika na kukuta watu mbalimbali wakiwa katika hali ya majonzi sana. Mke wa Kamanda Ballow yuko Dar es Salaam na anatarajia kufika Mwanza.
Mpaka sasa Polisi wanamshikilia mtu mmoja aitwaye Dorcas kwa ajili ya Mahojiano huku uchunguzi mkali ukiendelea kuhusiana na kifo cha kamanda Liberetus Ballow.

PICHA NA B PLUS BLOG

1 comment:

  1. Hey I know &X74;his is of&X66; &X74;opic but I ω&X61;s wοnderіng iif yοu knew
    of any widgetѕ I co&X75;lԁ add to my blog
    that аutomatically twee&X74; my newestt twіttеr updatеs.
    I've been lоoking for a plug-in like this for quite
    some time аnd was hoρing maybe уоu would have some eхperience
    wіth something lіke this. Please let me know if you гun into
    a&X6e;ything. I tr&X75;lу enjoy гeaԁing your blog and I &X6c;ook fοrωard to your new u&X70;dates.


    Revieω my weblog - green coffee &X62;ean (www.youtube.com)

    ReplyDelete