Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe
---
“ Kwa nchi za wenzetu magazeti ya uchunguzi yanafanya kazi hizi. Kwetu magazeti yanasubiri wanasiasa wafanye. Orodha ya Watanzania wenye akaunti Uswiss inakuja. Hoja Binafsi kuhusu suala hili imeruhusiwa na sasa naandaa maelezo ya Hoja. Sio suala la kutaja orodha tu bali pia hatua za kuchukua dhidi ya fedha hizo na wenye fedha haramu zilizofichwa huko.
Zitto Kabwe Kuna baadhi ya Watanzania wenzangu wanabeza kazi hii. Ninachowaambia sitakata tamaa. Ninaifanya kazi hii kwa umakini mkubwa kwa kuwa najua uhatari wake. Sikurupuki tu. Ninafanya kazi hii kwa niaba ya Kambi ya Upinzani nikiwa Waziri kivuli wa fedha. Hii ni kazi ya CHADEMA, sio kazi ya Zitto. Wengine wanasema mbona 'list of shame' tulitaja majina. Ni kweli. Lakini ilituchukua wiki kadhaa kutaja majina. Katika mkutano wa Jangwani wakati napokelewa kutoka Bungeni baada ya kusimamishwa ubunge kufuatia hoja ya Buzwagi, tuliahidi mbele ya umma kutaja orodha ya mafisadi. Tukataja wiki 3 baadaye mnamo Septemba 15, 2007. Tulifanya kazi ile kwa umakini sana. Tutaifanya kazi hii ya Watanzania wenye akaunti huko uswiss kwa umakini zaidi.
Tutaweka wazi majina ya Watanzania wenye akaunti Uswiss kwa utaratibu na umakini. Nitataja orodha hiyo Bungeni na kamwe sitataja nje ya Bunge. Hii ni kazi kubwa inahitaji utulivu. ” ~ Zitto Kabwe

MWANAHARAKATI WA UKWELI HUYO
ReplyDelete