WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, October 19, 2012

Magari Ya Serikali Yanayotumia Namba Binafsi Kusakwa



 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (waliokaa mbele wapili kushoto) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kusisitiza  utaratibu wa usajili wa magari
 ya Umma unafuatwa na kutafanyika zoezi rasmi la kurejesha usajili wa magari yote.Serikali imetoa muda hadi kufikia Novemba 15,2012 magari ya Umma yaliyo na namba  za kiraia, yarejeshwe namba stahiki za magari ya Umma .  Baada ya hapo Operesheni hiyo iitakamata magari, pikipiki, bajaj na mitambo ya umma,Vilevle kutakuwa na aina ya namba za usajili zitakazotumika kama ST, PT, MT,JW, DFP, CW, SM na ,SU.Hadi sasa serikali imesajili vyombo vya moto,123,431 yakiwemo magari,,pikipiki,bajaj na mitambo ya umma (pichani anaefuatia mwenye sare za polisi) ni Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani katika jeshi la Polisi  nchini Kamanda James Mpinga). (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).



 
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiteta jambo na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani James Mpinga ili magari ya umma yaliyo na namba za kiraia yarejeshwe kwenye namba  stahiki za magari ya Umma kabla ya oparesheni ya kamatakamata kuanza.  (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO)

1 comment:

  1. Serikali hapa imekosa mbinu kidogo tu kulimaliza hili tatizo. Wala haina haya kuanza kusakana saa hizi. Suluhisho rahisi na la kudumu ni; NAGARI YOTE YA SERIKALI YACHORWE ALAMA KUBWA ZA VIELELEZO VYA TAIFA LETU.Mfano: Ubavuni pande zote uchorwe mwenge wa uhuru au Nembo ya taifa vikiambatana na maandishi makubwa "Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hili litakuwa suluhisho la kudumu

    ReplyDelete