WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, October 22, 2012

Mwakyembe azidi kuuanika uozo wa Bandari Dar


Geofrey Nyang’oro
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amesema Bandari ya Dar es Salaam imeingia katika rekodi za dunia kwa utendaji mbovu barani Afrika kati ya bandari 36 zilizofanyiwa uchunguzi na taasisi za kimatifa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Dk Mwakyembe alisema  bandari hiyo, imengia katika rekodi kufuatia kukithiri kwa vitendo viovu vya wizi, utendaji mbovu, rushwa na ucheleweshaji mizingo unaofanywa na baadhi ya watendaji.
“Nimesikitishwa kuona Bandari ya Dar es Salaam ndiyo inayoongoza kwa utendaji mbovu katika ripoti za Taasisi za Kimataifa. Mizigo inayopakuliwa ndani ya siku moja hadi mbili kwenye bandari za mataifa mengine,  hapa Dar es Salaam inachukuwa siku 10 hadi 20,” alisema.


Alisema pia ni bandari inayoongoza kwa kutoza gharama kubwa ya mizigo kuliko bandari nyingine yoyote duniani  na inayoongoza kwa matukio ya hujuma na wizi wa mizigo ya watumiaji wa bandari.

“Mimi nilidhani Tanzania imeingia  katika historia ya dunia kwa kupakia twiga wazima kwenye ndege licha ya urefu wao ule na  kusafirisha nje, kumbe unapofikiri hilo ndilo kubwa yapo makubwa zaidi yake na yanapatikana (TPA) !, Ni jambo la kushangaza katika bandari ile kontena unaiona pale, lakini  ndani ya muda mfupi inatoweka  mchana kweupe, nitahakikisha ninafanyia kazi na hali hiyo itatoweka kabisa,” alisema Dk Mwakyembe.

Dk Mwakyembe alifafanua kuwa katika bandari hiyo, kumekuwa na matatizo makubwa likiwamo la ucheleweshaji mizigo na wizi ambapo kwa  kipindi cha mwaka juzi hadi mwaka huu, tayari kontena 32 zimeibiwa.

Alisema vitendo hivyo visivyofaa ndivyo vilivyosababisha baadhi ya wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi waliokuwa wakitumia  bandari hiyo, kuhama na kuanza kutumia bandari za nchi jirani ikiwamo ya Mombosa nchini Kenya.

Alisema pamoja na matatizo hayo tayari mabadiliko aliyofanya kwa muda mfupi yameanza kuzaa matunda kufuatia mawaziri kutoka nchi nne za jirani wanaotumia bandari hiyo kutuma ujumbe wa pongezi kwa mabadiliko hayo.
Alitaja nchi ambazo zimetuma ujumbe wa kupongeza kuwa ni Demokrasia ya Watu wa Kongo (DRC), Burundi, Rwanda na Uganda.

Akizungumzia ripoti, Dk Mwakyembe alipongeza tume aliyoiunda kwa kazi nzuri iliyofanywa na kusisitiza kuwa  Serikali itatekeleza mapendekezo yote yaliyotolewa na tume katika ripoti hiyo na kwamba itatenda haki kwa kila mtu.
“Ripoti hii ina kurasa zaidi ya 240, ina mapendekezo mengi na naahidi mbele yenu kuwa nitatekeleza kila kilichomo ndani, nitaisoma na kupitia mstari kwa mstari yote na  nitatenda haki kwa kila mtu atakayehusika kwa yote yatakayojitokeza,” alisema Dk Mwakyembe.

Kuhusu waliosimamishwa kazi, Dk Mwakyembe alisisitiza kuwa  hatima yao ya kurejeshwa kazini, kupoteza kazi na ama kuchukuliwa hatua zaidi itategemea ripoti hiyo.

Agosti 23 mwaka huu, Dk Mwakyembe aliwasimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa (TPA), Ephraem Mgawe  na wasaidizi wake kwa tuhuma za kukwamisha maendeleo ya bandari kukaidi agizo la Ikulu.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi iliyoundwa na Dk Mwakyembe, Wakili  Bernard Mbakileki alisema kamati yake wakati wa kutekeleza majukumu hayo ilikumbwa na changamoto mbalimbali ikiwamo ya baadhi ya watu waliotakiwa kuhojiwa kukwepa hatua hiyo kwa visingizio.

Source: Mwananchi

No comments:

Post a Comment