Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki akiongea na waandishi wa habari leo Ofisini kwake kuhusu kupinga maandamano wa Waislam yaliyopangwa kufanyika siku ya Ijumaa ya tarehe 02/11/2012 mara baada ya swala
. MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM SAID MECK SADIKI ATOA TAMKO KALI KUHUSU MAANDAMANO YA WAISLAM YALIYOPANGWA KUFANYIKA SIKU YA IJUMAA MARA BAADA YA SWALA.
Na Adrophina Ndyeikiza-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam 31/11/2012.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki ametoa tamko kali la kuwataka Waislam kuacha mara moja kufanya maandamano yao yaliyopangwa kufanyika siku ya Ijuamaa ya tarehe 02/11/2012 mara baada ya swala ya Ijumaa. Kwa mujibu wa vipeperushi vilivyoandikwa na kusambazwa na Jumuiya na Taasisi za Kiislam (Tz),vimewataka waislam kufanya maandamano makubwa kuelekea katika Ofisi ya Mhe.Waziri Mkuu kwa upande wa Dar es Salaam na Mikoani maandamano hayo yataelekea kwa wakuu wa Mikoa aidha kwa upande wa Zanzibar yataelekea Ofisi ya Makamu wa Rais. Aidha,Sababu ya kuandamana kwao wameelezea kuwa ni kushinikiza Serikali kutenda haki kwa wananchi wote bila ubaguzi kwani waislam wanabaguliwa kwa mambo mengi kama vile;- -Kudhalilishwa Masheikh wao kwa kukamatwa hovyo bila sababu za msingi mfano,Sheikh Ponda na Sheikh Farid wakati wakristo hawafanyiwi hivyo. Akijibu hoja hiyo mbele ya waandishi wa habari Mhe.Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Sheikh Ponda hakukamatwa kama Sheikh Ponda bali amekamatwa kama mtu yeyote yule ambaye anaweza kutuhumiwa kwa kosa fulani.Ameongeza kuwa Serikali haikumkamata Sheikh Ponda kutokana usheikh wake/dini yake au uislamu wake bali kutokana na kutuhumiwa kwake.Hivyo tuache vyombo vya sheria vifanye kazi yake na haki itazingatiwa tu. “Alisisitiza Mkuu wa Mkoa”. -Sababu nyingine ni pamoja na Kudhalilishwa matukufu ya Waislam huku Serikali ikikaa kimya.Akijibu hoja hiyo pia Mhe.Mkuu wa Mkoa amesema kuwa jambo hili si kweli kabisa kwani Serikali ilikwishachukua hatua stahiki kwa kumkamata kijana huyo aliyeyekojolea Koran na kumfikisha katika vyombo vya sheria,hivyo kijana huyo alikwishakamatwa,hata hivyo wale wote waliokwenda kuchoma makanisa,kupiga vioo vya magari ya watu na kuiba vitu mbalimbali katika makanisa na ndani ya magari ya watu nao pia wapo katika mikono ya sheria kwani uislam pia hauagizi hivyo. -Sababu ya tatu ni kuundiwa chombo cha kusimamia Waislam kwa nia ya kuwadhibiti na kulazimishwa Waislam kukitii pamoja na ukweli kwamba kinafisidi Uislam na Wislam.Akijibu hoja hiyo Mhe.Mkuu wa Mkoa amesema kuwa kamwe Serikali haiwezi kufanya hivyo,kwani kila chombo kinaundwa na wanajamii husika na wala Serikali haina dini hivyo haiwezi kuunda chombo chochote kile cha kidini.Hata hivyo zipo taratibu maalumu za namna ya kusajili taasisi yoyote ile kwani lazima kueleza mbele ya msajili ya kuwa taasisi yenu ni ipi na ina malengo gani kwa jamii husika na msajili akilizika na maelezo yenu basi huna budi kuisajili taasisi hiyo.Taasisi yoyote ile lazima isajiliwe na ifuate taratibu za sheria,na Serikali inazisikiliza taasisi zote kama zinafuata sheria na taratibu “Alisisitiza Mkuu wa Mkoa”. Hivyo basi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki amesema kuwa Waislam wote wapenda amani wasifanye maandamano yoyote siku hiyo ya Ijumaa mara baada ya swala kwani kwa kufanya hivyo HATUA KALI ZA KISHERIA DHIDI YA WATAKAOHUSIKA KATIKA KUYAANDAA NA KUSHIRIKI ZITACHUKULIWA kwani maandamano hayo ni BATILI na hayajaruhusiwa na JESHI LA POLISI. Sheria kali zitachukuliwa katika suala hili “Alisisitiza Mkuu wa Mkoa”.
Chanzo cha habari Mjengwa blog
No comments:
Post a Comment