WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, October 31, 2012

Makinda amfagilia Mwakyembe kwa treni ya Dar



"Alihidi kuwa lazima ikifika Oktoba usafiri wa reli ungekuwa tayari na kweli umetimiza hongera sana Waziri na unastahili pongezi kazana na uzi huo, sasa naomba ujibu swali lako.”

SPIKA wa Bunge, Anne Makinda jana alimpongeza Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Harison Mwakyembe kwa kuanzisha usafiri wa treni jijini Dar es Salaam katika kipindi alichoahidi huku akitoa kauli ya alidhani kuwa ni ‘pwagu na pwaguzi’ zilizoashiria kuwa ni vijembe kwa waliotangulia.

“Kwanza kabla ya kujibu swali hilo, mimi nataka nikupongeze sana Waziri kwa kuanzisha usafiri wa treni jijini Dar es Salaam kama ulivyoahidi, mwanzoni mimi nilijua ni yale yale ya ‘pwagu na pwaguzi’ lakini umetimiza, hongera sana Waziri,” alisema Makinda na kuongeza:
“Uliahidi kuwa lazima ikifika Oktoba usafiri wa reli ungekuwa tayari na kweli umetimiza hongera sana Waziri na unastahili pongezi kazana na uzi huo, sasa naomba ujibu swali lako.”

Kauli ya Makinda ilichukuliwa kama kukosoa utendaji kazi wa mawaziri waliowahi kuongoza Wizara hiyo hususan Omar Nundu ambaye awali alitoa kauli katika swali namba 14 ambalo liliulizwa na Nundu kuhusu ujenzi wa reli mpya ya kupitia Kata ya Mabawa na Tangasisi Jiji Tanga.

Nundu alikuwa Waziri wa Uchukuzi kabla ya mabadiliko ya baraza jipya la Mawaziri ambalo lilifanywa na Rais Jakaya Kikwete Mei mwaka huu na Wizara yake kuchukuliwa na Dk Mwakyembe.
Katika swali la msingi Nundu alitaka kujua Serikali inasema nini kuhusu hatma ya wananchi takribani 650 juu ya makazi yao na ulipwaji wa fidia baada ya kuarifiwa kuwa watahamishwa ili kupisha ujenzi wa reli mpya na kwamba tathimini ya fidia yao ilipangwa kufanyika Aprili mwaka huu.

Akijibu swali hilo Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe alisema katika bajeti ya mwaka wa fedha 2012/13, Wizara kupitia Kampuni hodhi ya reli (Rahco) iliwasilishwa na Manispaa ya Tanga na kukubaliana kutenga ekari 150 katika eneo la Mwambani kwa ajili ya kujenga sehemu ya kupangisha mabehewa.

Alisema katika kutekeleza suala hilo, Rahco ilimweka mshauri mwekezaji M/S Majengo Estates Developer Limited kwa ajili ya kufanya tathimini ya fidia kwa wananchi wa maeneo hayo.

Waziri alisema taarifa iliyowasilishwa na Mshauri mwelekezi inaonyesha kwamba gharama za fidia za wakazi wa Magaoni ni Sh 5.3 bilioni.

Alisema hivi sasa nyaraka za fidia zipo Manispaa ya Tanga kwa ajili ya uhakiki wa umiliki wa ardhi na makazi ya wananchi hao katika ngazi ya kijiji, wilaya na mkoa ambao unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi huu.

Source Vijimambo Blog

No comments:

Post a Comment