Sunday, October 21, 2012
Na A. K Simai
fujo. Waingereza walipotaka kuwalemaza
wananchi wake wasijihusishe na siasa waliandaa mfumo maalum ambao
uliwashughulisha wananchi wengi wa kawaida na huku wakiwaachia tabaka dogo la
mabepari na walio kwenye matabaka ya juu (upper class) kushiriki siasa.
Walichokifanya ni kuwajengea mazingira ya
kupenda michezo kwa ujumla na hasa mpira wa miguu na kuujengea ushindani mkubwa
mpaka imekuwa ndiyo siasa ya wananchi wa kawaida kuzungumzia mipira kila kona
na kila sehemu. Homa hii siku hizi ipo hata nyumbani ambapo mtoto
mdogo anaweza kukuelezea kuhusu ligi ya Uingereza na wachezaji wake kwa upeo
mkubwa.
Pia baada ya pirika pirika za kwenda mbio
na maisha siku za wikiendi wamewawekea sehemu za kujifurahisha kwa vinywaji na
miziki ya kila aina ili izidi kuwasahaulisha na msongamano wa mawazo wa wiki
nzima na hivyo kuwa na muda mchache kuzungumzia siasa za nchi.
Naam waingereza
walifanikiwa vizuri sana maana sera hii inazidi kuendelezwa na huku
wanaoshiriki katika maamuzi muhimu na nyeti ya nchi ni kundi la wanasiasa
wachache wanaotoka katika matabaka maalum.
Wazanzibari walipotaka kuwalemaza wananchi
wake waliwajengea maskani na mabaraza ya mazungumzo ili wapate muda mwingi wa
kuzungumzia siasa na yanayojiri huku na kule katika mkondo hatari wa siasa.
Wanasiasa wakaichukua siasa na kuitoa
pahala pake inapopaswa iwepo wakaipeleka sehemu isiyopaswa kuwepo na
kumshughulisha kila mmoja wetu na siasa. Siasa ipo majumbani, siasa ipo
barazani, siasa ipo makazini, siasa ipo mitaani, siasa ipo kanisani, siasa ipo
misikitini almuradi siasa wee siasa wee. Ilifika wakati majirani walishindwa
kuzikana kwa sababu ya siasa, ndugu kukhasimiana kwa sababu ya siasa.
Wanasiasa wakajisahau wakiona muradi
umepatikana kila ikizungumzwa siasa kila kona wao huchekelea na kuendelea na
siasa yao bila ya kujali siasa inayoendelea kwengine.
Siasa hii ya mitaani sasa imekuwa. Mitaani
imekuwa hakuwatoshi tena hasa baada ya kukosa sehemu ya kutoa joto lao tokea
vyama viwili vikuu vya siasa kuamua kuacha tofauti zao za kisiasa walipounda
serikali ya umoja wa kitaifa.
Vijana wengi hawana ajira,
serikali imeshindwa kujifunza jinsi Uingereza ilivyoweza kuwadhibiti vijana
wake angalau kwa waliokuwa hawana ajira kuwapatia Misaada ( Benefits) wajikimu
wakati wakitafuta ajira.
Vijana wengi mitaani ambao ndiyo asilimia
kubwa ya wakaazi hawana vivutio vya kuwapumbaza haswa siku za mapumziko kama
ilivyo Uingereza ambapo wamewekeza katika michezo kwa kiasi kikubwa wakiwa na
malengo yao. Vijana hawa huishia vijiweni na mwishowe kujiundia
vikundi vya kihuni kama ubaya ubaya, mbwa mwitu, kimya kimya na kutishia jina
zuri la Zanzibar pamoja na sifa yake kuwa visiwa vya amani. Wengine, Mola
awarehemu, kujiingiza katika madawa ya kulevya.
Athari za kujionea mambo yanayofanyika
katika nchi za nje iwe kwenye televisheni au kwenye mitandao imewaingia vijana
wetu mpaka sasa kukitokea fujo la aina yoyote basi , usalama, amani hupotea
haraka sana, maduka kuvunjwa, mali kuporwa, vifaa kuharibiwa kwa kile ambacho
vijana wamekuwa wakikisubiri tu kitokee na wao kuanza kazi zao. Mambo haya
yalikuwa hayapo Zanzibar, yametokea wapi? Hili ndilo la kujiuliza kama ni
Serikali.
Hivi ni kweli wafuasi wa uamsho ndio
wanaovunja Baa na kisha kuonekana wakigida bia na ulevi hadharani?, Hivi ni
kweli wafuasi wa uamsho ndio waliokwenda kuitia moto maskani mama ya kisonge?,
Hivi ni kweli wafuasi wa uamsho ndio wanaoweka vizuizi katika barabara na kisha
kuwapora watu kwa nguvu? Hivi ni kweli wafuasi wa uamsho ndio waliomkamata na
kumkata mapanga askari wa FFU?
Masuala yote majibu yake yapo kwa suala la
kimsingi la serikali kushindwa kuwa na mfumo wa kuwajengea msingi mzuri kundi
la vijana wanaotegemewa kuwa taifa la kesho. Serikali imevuna ilichokipanda.
Yaliyojiri mwezi wa tano mwaka huu wakati
mmoja wa viongozi wa Uamsho alipokamatwa na Polisi na kuwekwa ndani iliigharimu
sana serikali kwa jina la Zanzibar kutiwa doa, kutumika vyombo vya Dola katika
kuleta utulivu na tuliamini matokeo ya vurugu zile yalikuwa ni fundisho kwa
Serikali, Polisi na Uamsho yenyewe ambayo ilithibitisha kutohusika na vurugu
zile moja kwa moja.
Miezi mitano baadae imeonekana kwamba
vyombo hivi ima vimefeli katika mtihani wake uliopita au kimeingia kidudu mtu
aliyetaka kujaribu kuirejesha ile hali ambayo Wazanzibari wengi wanaopenda amani
na utulivu wa nchi yao wanaiona gharama yake kwa vitendo. Kitendo
cha kutekwa nyara mmoja katika viongozi wa uamsho na kuchukuliwa kusikojulikana
kimeibua yaliyoibuka kama ilivyokuwa mwezi wa tano. Mara hii tu angalau
makanisa hayakuchomwa au kuharibiwa.
Baada ya siku tatu kiongozi kaonekana na
tumesikia kauli yake yaliyojiri wakati alipotekwa nyara na akihojiwa.
Kwa kuwa kauli hizi ni za upande mmoja na zitazokosa ushuhuda wa upande wa pili
zitabakia kwenye miono na maoni tofauti kwa wenye kuzisikia.
Uamsho wanapaswa kujiangalia tena na
kurudi mezani kujitathmini kwa nia zao njema walizonazo na mazingira au halisi
iliyopo na njia zao wanazozitumia hasa ukiangalia matukio yenyewe
yanavyonasibishwa na Uamsho kwa kuwa tu hisia zinatufanya tuamini hivyo.
Hali ya Zanzibar kwa sasa ni tete sana,
tupo katika hatua muhimu ya kukusanya maoni juu ya Katiba mpya. Hali kama hii
itaakisi mawazo, fikra na maoni ya wachangiaji na hivyo kupelekea kupata mawazo
yaliyojaa hisia zaidi kuliko hali halisi
Uamsho ina takriban miaka kumi tokea
kuanzishwa kwake. miaka kumi ni muda mzuri wa kujifanyia tathmini
yakinifu.Alhamdulillah Imekuwa ikifanya harakati nyingi zenye kuleta tija kubwa
kwa Waislamu na nchi kwa ujumla kama kushiriki kikamilifu katika kuunganisha wananchi
wa visiwa hivi waondokane na tofauti za kisiasa na hatimaye kuzaliwa serikali
ya umoja wa kitaifa.
Ila Uislamu ni dini ya amani kama zilivyo
baadhi ya dini nyingine, matendo maovu ya wachache yanaharibu taswira ya Uamsho
yenyewe kwanza na baya zaidi kuharibu taswira ya Uislamu kwa ujumla.
Uislamu ndio unaopigwa vita na si Uamsho
kama inavyoonekana kwasababu ya kupelekea waislamu na uislamu kuingizwa na
kujumuishwa kwenye kapu moja la mambo mabaya.
Mimi binafsi ninakataa katakata kwamba
vurugu zilizotokea zimefanywa na wafuasi wa Uamsho, hawa ni wahuni tu wanatumia
fursa na mwanya wanaopewa na Uamsho katika harakati zake. Mfuasi wa uamsho hana
definition ni nani ni mwanachama (card holder) supporter ( anayewaunga mkono),
sympathiser ni nani hivyo mtu yeyote anaweza kujinasibu na kujilabu kwamba mimi
ni Uamsho.
Kwa kuutendea haki Uislamu, nadhani iko
haja kwa Uamsho kujaribu kukaa chini ni kutafakari pamoja na kujitathmini
katika mwenendo wa matukio yanayotokea hapa nchini na jinsi jamii iliyokosa
maadili sahihi ya malezi na makuzi inavyojidhihirisha wakati wa vurugu na
HABARI IMEWEKWA
NA MAPARA ZanziNews
No comments:
Post a Comment