Rais Jakaya Kikwete ameonya kwamba vitendo vya rushwa vinavyojitokeza katika chaguzi za ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) visipodhibitiwa vitakitumbukiza chama hicho kwenye shimo.
Rais Kikwete alitoa angalizo hilo ikiwa ni siku moja tu, baada ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) kumchagua Sophia Simba kuwa Mwenyekiti wake katika uchaguzi unaodaiwa kugubikwa na rushwa, vijembe na tambo.
Kikwete, amesema suala la kuuza na kununua kura lisiposhughulikiwa litakitumbukiza chama kwenye shimo.
Kikwete aliyasema hayo juzi usiku alipokuwa akifunga Mkutano Mkuu Maalum wa uchaguzi wa UWT uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo Chuo cha Mipango mjini hapa.
Rais Kikwete alisema kuwa wakati huu kuna mambo mengi ambayo baadhi yake yanasikitisha na kwamba hata kuyasema yanatia aibu.
“Kuna mambo mengi, mengine yanasikitisha hata kuyasema ni aibu, na wakati wote naendelea kukumbusha. Ndugu zangu haya tukiendelea nayo sura tunayoijenga kwa wananchi ya chama chetu… tunaona sisi tunapata, lakini athari yake kwa wananchi na ndani ya chama ni mbaya sana, tena sana, sina namna ya kutafuta maneno mazuri ya kulieleza hilo ya kununua na kuuza kura ,” alisema Rais Kikwete ambaye alionyesha kukerwa sana na jambo hilo na kuongeza
Source: BongoCelebrity
No comments:
Post a Comment