NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 25/10/2012
TUME YA HAKI ZA BINAADAMU NA UTAWALA BORA IMEISHAURI SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KUWATAFUTA KUWAKAMATA WALE WOTE WALIOSHIRIKI KATIKA VITENDO VYA VURUGU LILILOTOKEA WIKI ILIOPITA NA KUVUNJA VIKUNDI VYOTE VYA KIHALIFU VILIVYOANZA KUSHAMIRI HAPA ZANZIBAR.
AIDHA TUME IMETAKA SERIKALI KUJIPANGA KIKAMILIFU NA KUHAKIKISHA KUTORUDIWA TENA KWA VITENDO KAMA HIVYO KATIKA NCHI YETU.
KWA MUJIBU WA TAARIFA ILIYOTOLEWA NA TUME HIYO NA KUTIWA SAINI NA KAMISHNA WAKE ZAHOR J. KHAMIS IMEELEZA KWAMBA VITENDO HIVYO NI UVUNJAJI WA HAKI ZA BIANAADAMU NA ZINAPINGANA NA SHERIA ZA NCHI NA KINYUME NA MASHARTI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
HIVYO INALAANI KITENDO CHA KUUWAWA KWA ASKARI SAID ABRAHMANI KWANI KITENDO HICHO NI UVUNJAJI WA HAKI ZA BIAADAMU NA KINAPINGANA NA SHERIA ZA NCHI NA KINYUME NA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA IBARA YA 14 INAYOZUNGUMZIA HAKI YA KUISHI NA KATIBA YA ZANZIBAR IBARA YA 13 INAYOZUNGUMZIA HAKI YA KUWA HAI.
KITENDO HICHO PIA KINAPINGANA NA MKATABA WA KIMATAIFA WA HAKI ZA BINNADAMU NAMBA 3 NA ULE WA AFRIKA IBARA YA 4.
HIVYO IMEENDELA KUSAURI KWAMBA SERIKALI PAMOJA NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUFANYA UCHUNGUZI WA KINA KUWATAMBUA NA KUWAKAMATA WAHUSIKA WOTE WA MAUAJI HAYO NA KUWAFIKISHA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.
AIDHA TUME HIYO YA HAKI ZA BINAADAMU NA UTAWALA BORA IMELAANI KITENDO ALICHOFANYIWA DIWANI WA CCM WADI YA CHUMBUNI KWA KUSHAMBULIWA KUJERUHIWA, KITENDO AMBACHO KINAKWENDA KINYUME NA HAKI ZA BINAADAMU NA KATIBA YA TANZANIA IBARA YA 13(6) (C)NA KATIBA YA ZANZIBAR IBARA YA 13(3) INAYOPIGA MARUFUKU MTU KUTESWA, KUADHIBIWA KINYAMA AU ADHABU ZA KUMDHALILISHA. PIA KUPORA MALI YA MTU NI KINYUME CHINI YA IBARA YA 17 YA JAMHURI YA MUUNGANO NA IBARA YA 16 INAYOZUNGUMZIA HAKI YA KUMILIKI.
TUME IMEENDELEA KUELEZA KUWA MATUKIO YOTE HAYO NI MUENDELEZO WA MATUKIO KADHAA YALIOTOKEA HAPO KABLA NA AMBAPO YAKITAMKWA HADHARANI TENA BILA KIFICHO MATOKEO YAKE NDIO YALIOTUFIKISHA LEO HAPA TULIPO. HAYO NI MAPUNGUFU YA UZINGATIAJI WA MISINGI YA UTAWALA BORA IKIWEMO UWAJIBIKAJI NA UTAWALA WA SHERIA.
IKIELEZEA UTATA ULIOJITOKEZA KATIKA KADHIA YA KUTOWEKA KWA SHEIKH FARID, TUME HIYO IMEELEZA KWAMBA KUMEJITOKEZA KWAMBA JUMUIYA YA UAMSHO NI YA KIDINI ( KIISLAM) NA IMEKUWA IKITUMIWA NA MAKUNDI YA WAHUNI AMBAYO YAMEJIPACHIKA MAJINA KAMA MBWAMWITU,SIMBA MKALI, UBAYA UBAYA NA TOTO TUNDU ILI KUFANIKISHA AZMA YAO.
DAI LA KUTEKWA KWA SHEIKH FARID LINA UTATA MKUBWA AMBAO UNAHITAJI UCHUNGUZI NA UFAFANUZI KAMA VILE HUKO ALIKOTEKWA VIPI ALIWEZA KUFIKA MSALANI (CHOONI) AMBAKO ALIKUWA AKINYWA MAJI WAKATIA AKIWA AMEFUNGWA KITAMBAA USONI NA MIKONONI AKIWA NA PINGU NA KATIKA NYUMBA AMBAYO HAIJUI IMEKAAJE NA KUSHINDWA KUITAMBUA MUDA WOTE.
KUNAUHUSIANO GANI WA KUTEKWA KWA KIONGOZI WA MUAMSHO NA HUJUMA ZA MALI ZA WATU NA CCM NA LILE DAI LA KUNYIMWA KULA KWA SIKU TATU BILA KUATHIRIKA KIAFYA.
HIVYO TAARIFA HIYO ILIMTAKA SHEIKH FARID KUTOA MAELEZO YANAYOTHIBITISHA PASIPO NA MASHAKA ILI KUWATHIBITISHIA WAZANZIBARI, WATANZANIA NA ULIMWENGU KWA JUMLA JUU YA KUTOWEKA KWAKE.
SHEIKH FARID ANADAI ALITEKWA NA WATU WASIOJULIKANA TAREHE 16 MWEZI HUU NA KUONEKANA SIKU TATU BAADAE AKIWA KATIKA HALI YA UZIMA NA SALAMA JAMBO AMBALO LILISABABISHA VURUGU KUBWA HAPA ZANZIBAR NA KUSITA KWA SHUGHULI ZOTE ZA KIUCHUMI NA KIJAMII KUTOKANA NA FUJO HIZO ZILIZOTOKEA AMBAPO HADI SASA HAIJAJULIKANA THAMANI AU HASARA ILIOPATIKANA KUTOKANA NA MACHAFUKO HAYO AMBAPO ASKARI MMOJA WA KIKOSI CHA FFU KWA JINA LA SAID ABDULRAHMAN KUUWAWA.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELAZO ZANZIBAR 25/10/2012
No comments:
Post a Comment