WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, October 19, 2012

AGIZO LA POLISI: MARUFUKU KUANDAMANA DAR


Agizo limepatikana via blogu ya John  Badi


Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam wamekutana na kutoa tamko la kuzuia Waislamu kuacha kuandamana mara moja.

Katika taarifa ya waliyoitoa mapema leo asubuhi wakuu na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo wa dini wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadick, aliwatoa hofu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwani wamejipanga kulinda hali ya amani.

Akitoa tamko hilo, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa kumekuwapo na taarifa za waumini wa Kiislamu kuandamana na kufanya fujo mara baada ya swala ya Ijumaa na baadala yake amewataka kuacha kufanya hivyo na warejee majumbani kwa amani na suala hilo linashughulikiwa kisheria.

Hata hivyo kwa upande wao viongozi wa dini waliokutana na Mkuu wa mkoa  juu ya kutolea tamko hilo waliwaasa waumini wote kutoingia mitaani na kuandamana kwani wakifanya hivyo ni kukiuka misingi mbalimbali  ya kisheria iliyopo kihalali na watakapofanya hivyo ni kukiuka sheria za nchi.

Kamanda Kova, Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Musa bin Salum amewataka wakuu wa misikiti mkoa wa Dar es Salaam kuwakataza waumini hao kufanya maandamano kwani kufanya hivyo ni kukiuka misingi iliyopo. Aidha, aliwaomba waumini warejee majumbani  kwa amani.

Askofu  Makunda aliwataka watanzania kuendelea kufuata misingi ya kiimani bila chuki wala kufanya fujo.

Kamanda wa Polisi Kanda maalum mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova alitoa onyo kali kwa waislamu kuacha kufanya hivyo hii leo kwani kwa atakaekiuka atachukuliwa hatua kali. Kova aliwataka waumini kurejea majumbani mwao kwa amani bila kufanya maandamano  na pia aliwataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuendelea na shughuli zao kama kawaida na kupuuza tishio hilo la fujo kutoka kwa waislamu.

“Jeshi limejipanga kuakikisha hali ya amani na usalama 

Source: http://www.wavuti.com


HIVI NDIVYO MAGARI YA JESHI YALIVYOONGOZANA KWENDA KARIAKOO KUTULIZA VURUGU ZA WAISLAM!


Hili ni moja ya Gari lililobeba wanajeshi ambao walikua doria wakati waandamaji waripoleta vurugu na kusababisha vurugu na mabomu ya machozi kulindima kwenye baadhi ya maeneo kama vile Kariakoo na Posta.Tuendeleee kuvuta subira...
Msafara wa magari ya JWTZ kuelekea tuliza Vurugu
Yakiwa yanaelekea eneo la Tukio
Picha hii ya Tamko kwa hisani ya Mo Blog

SOURCE VIJIMAMBO BLOG



No comments:

Post a Comment