WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, October 27, 2012

VPL KUTIMUA VUMBI LEO MECHI ZINAZO VUTA MASIKIO NA MAWAZO YA WATU NI HIZI HAPA VIJIMAMBO ITAWAPATIA MATOKEO YA MECHI ZOTE



Wana Jangwani DAR YANGA  A. S. C watakuwa wanaumana na JKT Oljoro FC ndani ya dimba la kumbukumbu ya Sheikh Amir Abeid Arusha, a.k.a (Arachuga) Mechi hii ni yakukata na shoka Yanga wakiwa na hamu ya kuongoza VPL kwa mala ya kwanza kama watashida mechi hii na Azam na Simba kutoshana nguvu pale chamanzi. Kwani Yanga wana point 17, na wakishinda mechi hii wanaweza kufikisha point 20 . Lakini si kazi rahisi kwao kutokana na timu wanayo cheza nayo kuwa bora na hipo katika top 5 ya VPL na inacheza uwanja wa nyumbani. Yetu masikio kikosi cha Yanga kipo imara kuweza kuhimiri kwata za Mugambo hao wa Oljoro na kuwa kuwageuza Urojo wa maharage ya Mbeya licha ya kucheza nyumbani kwao.
 Simba Mnyama atakae kuwa mgeni wa Azam Fc katika uwanja wa Chamanzi, Timu zote zinataka kurinda heshima yake yakuto poteza mchezo hata mmoja kwaiyo kazi hitakuwa hapo Chamanzi. Simba wakiongoza VPL naAzam wakitaka kuwapoka huongozi huo wa League.
 Azam Fc watakuwa Chamanzi uwanja wa nyumbani wanacheza na Simba mechi hii itavuta hisia za watu wengi wapenda soka la kibongo kwani kila timu imehimarika vilivyo na inataka kujiakikishia inapata point 3. Azam Fc wamecheza mechi 8 na wana point 18 na ni timu ambayo haijapoteza hata mechi moja na imefungwa magoli machache kuliko timu yeyote katika VPL. Simba wao nao kama Azam awajapoteza mechi yeyote na wanaongoza VPL kwa kuwa na point 19 na Azam Fc wakiwa chini ya Simba, hila Simba wamecheza mechi 9 mechi moja zaidi ya Azam. Kwaiyo hapa kutakuwa na patashika jezi chanika kila mmoja akilinda heshima ya uto poteza mechi hata moja. Mambo yote wikend hii tega sikio hapa hapa utapata matokeo ya mechi zote.
 JKT Oljoro wata pambana na Yanga wikend katika uwanja wa shekh Amri Abedi Arusha, hii mechi muhimu kwa timu zote, Aljoro siyo timu ya kubeza kwani wako katika top 5 ikiwa na point 14 na wanacheza uwanja wa nyumbani unajua tena ule usemi usemao mcheza kwao.........

No comments:

Post a Comment