Rais Jakaya Mrisho kikwete na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda wakipitia Waraka wa Utumishi Namba 5 wa mwaka 2009 kuhusu matumizi bora na salama ya vifaa na mifumo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA) serikalini wakati wa kikao cha kazi (retreat) cha siku tatu cha Mawaziri, Manaibu Mawaziri na maafisa waandamizi wa serikali kujadili mikakati endelevu na utekelezaji wa sasa na wa baadae katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha kazi (retreat) cha siku tatu cha Mawaziri, Manaibu Mawaziri na maafisa waandamizi wa serikali wanaokutana kujadili mikakati endelevu na utekelezaji wa sasa na wa baadae katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Pamoja naye meza kuu ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali (kulia) na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
Dk. Jabir Kuwe Bakari, Mtendaji Mkuu, Wakala ya Serikali Mtandao, akitoa mada kuhusu wakala huo kwa wajumbe kikao cha kazi (retreat) cha siku tatu cha Mawaziri, Manaibu Mawaziri na maafisa waandamizi wa serikali kujadili mikakati endelevu na utekelezaji wa sasa na wa baadae katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George Yembesi akifafanua juu ya Waraka wa Utumishi Namba 5 wa mwaka 2009 kuhusu matumizi bora na salama ya vifaa na mifumo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA) serikalini kwa wajumbe kikao cha kazi (retreat) cha siku tatu cha Mawaziri, Manaibu Mawaziri na maafisa waandamizi wa serikali kujadili mikakati endelevu na utekelezaji wa sasa na wa baadae katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma
Waziri wa Viwanda na Biashara Dk Abdallaha Kigoda akitoa mada ya wizara yake katika kikao cha kazi (retreat) cha siku tatu cha Mawaziri, Manaibu Mawaziri na maafisa waandamizi wa serikali kujadili mikakati endelevu na utekelezaji wa sasa na wa baadae katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma
Katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu Lyimo akitoa mada ya wizara yake katika kikao cha kazi (retreat) cha siku tatu cha Mawaziri, Manaibu Mawaziri na maafisa waandamizi wa serikali kujadili mikakati endelevu na utekelezaji wa sasa na wa baadae katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma
Naibu Waziri wa Kazi na Vijana Dk Makongoro Mahanga akichangia kwenye kikao cha kazi (retreat) cha siku tatu cha Mawaziri, Manaibu Mawaziri na maafisa waandamizi wa serikali kujadili mikakati endelevu na utekelezaji wa sasa na wa baadae katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma.Picha na IKULU
chanzo cha Haki Ngowi blog
No comments:
Post a Comment