OCTOBAR
22, 2012
Pamoja na mapungufu yake
yote, siasa Marekani ina mambo kadhaa ya kupigiwa mfano. Kinachonivutia zaidi
ni mijadala inyofanyika baina ya wagombea kabla ya uchaguzi. Leo, kwa mfano,
tumeshuhudia pambano la tatu baina ya Obama na Romney
Mijadala ya namna hii
inawapa wapiga kura fursa ya kuwasikiliza wagombea. Vile
vile naiona kama namna ya kuwaheshimu wapiga
kura.
Mfumo wa Marekani
unatambua kuwa wapiga kura wana haki ya kuwasikia wagombea wakiongelea masuala
kadha wa kadha katika kupambanishwa na wapinzani wao.
Ninakerwa ninapokumbuka mambo yalivyo kwetu Tanzania.
Ninakerwa nikikumbuka jinsi CCM ilivyotoroka midahalo mwaka 2010. Ni dharau kwa
wapiga kura. Tatizo ni jinsi wapiga kura wengi walivyo mbumbumbu, wasitambue
kuwa hili lilikuwa dharau. Walipiga kura kama vile hawajadharauliwa.
Hebu fikiria mambo
yangekuwaje ule mwaka 2010 iwapo Kikwete angepambana na Slaa katika midahalo
mitatu hivi, ambayo ingeonekana katika televisheni na kusikika redioni. Lakini
tulinyimwa fursa hii, kutokana na maaumzi muflisi ya CCM.
Hakuna sababu yoyote kwa
nini siku zijazo tusifanye kama wa-Marekani wafanyavyo. Watangazaji makini wa
redio na televisheni tunao, ambao wanaweza wakaendesha mahojiano nasi tukapata
fursa nzuri ya kuwabaini wababaishaji na kuwatupilia mbali
Habari kwa Hisani ya Hapa Kwetu Blog
No comments:
Post a Comment