SWALI LILILOLETA MTAFARUKU:
"Wewe ukiwa
mwenyekiti wa UWT kwa kipindi cha miaka minne iliyopita hatujawahi kukuona
ukisimama jukwaani kutetea Chama."
Jibu la swali
Sofia Simba alijibu "Inaonekana
aliyeuliza swali hajakomaa katika siasa za nchi, ndio maana ameambulia kuzomewa
na wajumbe wa mkutano huu. Habwatuki bungeni au majukwaani kwa vile yeye ni
serikali, na hata mbunge wa CCM hapaswi kukikosoa chama chake. Mimi si mithili
ya upinzania kukaa na kukiosoa chama napaswa kukitetea. Anayesema Sofia Simba
hajafanya kitu anajidanganya kwani wapiga kura wako kwenye matawi, kata, wilaya
na mikoa, hao ndio wapiga kura wa chama na mimi kama mwenyekiti wa UWT
nilijiimarisha katika ngazi za chini."
Je Baada ya jibu hili tunafikiri kulikuwa na sababu yeyote ya wawili hawa ambao wamekabidhiwa dhamana ya uongozi katika nafasi mbalimbali ndani ya serikali kuzozona?
Je mzozano wao ndio ukuaji wa demokrasia au ilikuwa tu ni sehemu ya kuonyeshana ubabe na nani ni nani mbele ya wapambe wao?
Nafikiri kama taifa tunahitaji zaidi viongozi ambao wanaweza kuvumiliana nakukabili challenges katika njia ambayo itadumisha amani na kuepusha ugomvi na uhasama.
Tulijenge Taifa pamoja kwa upendo na kuvumiliana.
No comments:
Post a Comment