WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, October 19, 2012

NINI SURUHISHO YA HAYA YANAYOENDELEA TANZANIA YETU, NA NINANI WA KUSHOOSHEWA KIDOLE?. MUNGU IBARIKI TANZANIA


Askari Kanzu akimsindikiza kwa teke mmoja kati ya watuhumiwa waliokamatwa wakati wa operesheni maalum iliyowekwa katika jiji la Dar es Salaam,leo mchana ili kuwadhibiti baadhi ya waliodaiwa kuwa ni waumini wa dini ya kiislam, waliokuwa wamepanga kufanya maandano mchana wa leo baada ya Swala ya Ijumaa kuelekea Ikulu kwa lengo la kushinikiza kiongozi wao, Katibu wa Jumuiya za Taasisi za Kiislam, Sheikh Ponda, aliyekamatwa majuzi,aachiwe. Hata hivyo jitihada za watu hao ziligonga ukuta baada ya wao kujipanga kutokea kila kona na kukutana maeneo ya Ikulu, lakini la Askari pia walijiandaa na kujipanga vyema kila kona ya jiji na kuwadhibiti watu hao. 
Vurugu kubwa ilikuwa katika maeneo ya Kariakoo ambako pia walijitokeza baadhi ya vijana waliojichanganya na makundi hayo na kuanza kuvamia maduka na kupora mali za watu na kuwatishia wenye maduka, jambo ambalo liliwafanya Polisi kuwatawanya kwa kupiga risasi hewani na waliokaidi amri hiyo walianza kushughulikiwa kama picha hizi zinavyoonyesha Pata Mkanda Kamili.
Twende garini.....
Akaaaa sio mimi jamaniiiiiii, Babu (kulia} akijitetea...
Askari wakimdhibiti babu...
Babu akishuhshwa garini kuingizwa kituoni.....
Mgambo wa kike akipambana na kijana kumburuta kumpeleka garini, baadaye mgambo huyu CHALIII
Mgambo chaliii,lakini wapi anaye tuuuu....
Watuhumiwa wakipandishwa garini....
Watuhumiwa wakipandishwa garini....
Watuhumiwa wakipandishwa garini....
Jamaa akijaribu kueskep ambapo alikula bonge la mtama na kutambaa kama hivi na kudakwa na mgambo wa kike....

No comments:

Post a Comment