WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, October 17, 2012

Vurugu zazuka Zanzibar baada ya ‘kiongozi wa Uamsho kukamatwa’

17/10/2012


Huyu ndiye Kiongozi wa Kundi linaloitwa UAMSHO la Zanzibar Sheikh Farid anayesadikiwa  kukamatwa huko Visiwani Zanzibar. Kundi hilo shughuli zake ni za mihadhara ya Kidini hasa ya Kiislam. Picha zote naakhtarissak
Kwa mujibu wa Katibu wake, Abdallah Said Ally, amesema alikuwa na dereva wake maeneo ya Michenzani akitokea nyumbani kwake Mbuyuni, ndipo akakutana na gari moja ambalo dereva halifahamu na akashuka mwenyewe kwenye gari lake na kuingia katika hilo gari na kuanzia hapo hadi sasa hajulikani alipo.
Katibu huyo wa Uamsho na wenzake wamekuwa katika juhudi za kutuliza jazba za wafuasi wao na sasa wanawasiliana na polisi kujua alipo kiongozi wao.
Habari zaidi baadae
Picture
picha @akhtarissak
Taarifa via RemmyMwema blog:  Taarifa kutoka kwa watu waliopo Zanzibar zinasemakuwa zimezuka vurugu kiasi cha kusababisha barabara za eneo la Darajani mjini Unguja, kufungwa.

Vurugu hizo inasemekana zimetokana na baadhi ya watu kuamini kuwa askari wamemtia nguvuni kiongozi wa kikundi cha “Uamsho” kinachoendesha mihadhara ya dini ya Kiislam, Sheikh Farid jana usiku na hivyo kushinikiza Jeshi la Polisi limwachie huru.

Habari zilizogaaa kila kona sasa hivi mjini Unguja ni kuwa Sheikh Farid alitekwa na watu wasiojulikana na hadi sasa haijulikani aliko.

Katibu wa Uamsho, Abdallah Said Ally, amesema Sheikh Farid alikuwa na dereva wake maeneo ya Michenzani akitokea nyumbani kwake Mbuyuni, ndipo akakutana na gari moja ambalo dereva halifahamu na akashuka mwenyewe kwenye gari lake na kuingia katika hilo gari na kuanzia hapo hadi sasa hajulikani alipo.

Katibu huyo na wenzake wamekuwa katika juhudi za kutuliza jazba za wafuasi wao na kuwasiliana na polisi kujua alipo kiongozi wao.

Sheikh Farid 'amepotea' muda ule ule ambao inadaiwa mwenzake (Sheikh Ponda) alikamatwa (saa 4 usiku wa kuamkia leo jijini  Dar).

Hata hivyo, wananchi wa  Zanzibar wanasema polisi, Uamsho na Serikali wangesubiri wanafunzi wamalize mitihani ya Form 4 kabla ya wao kuanza malumbano yao!

Kutokana na Vurugu hizo Sehemu ya ofisi ya Chama Cha Mapinduzi imechowa moto na kwa kiasi kikubwa imeungua na hakuna aliyeripotiwa kuumia wala kupoteza maisha katika vurugu zinazoendelea sahivi huko zanzibar.
Picture
picha: @akhtarissak
Picture
picha @akhtarissak
Picture
picha @akhtarissak
Picture
picha @nazaninemoshiri
Picture
Moshi ukifuka kwa mbali nyuma ya majengo (picha @nazaninemoshiri)

Source: http://www.wavuti.com

No comments:

Post a Comment