WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, November 27, 2012

SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA KWA AJALI


 


MSANII nyota wa vichekesho na muziki wa kizazi kipya nchini, Hussein Ramadhani, maarufu kwa jina la Sharo Milionea amefariki dunia.
Sharo alifariki dunia kwa ajali ya gari jana saa mbili usiku katika barabara ya
Segera-Muheza wakati alipokuwa akitoka Dar es Salaam kwenda Muheza.
Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga, Constantine Massawe amesema kwa njia ya simu kuwa, Sharo alipata ajali katika eneo la Maguzonizoga wilayani Muheza baada ya gari alilokuwa akiendesha kuanja barabara na kupinduka mara kadhaa.
Kwa mujibu wa Kamanda Massawe, marehemu Sharo alikuwa akiendesha gari aina yaToyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR na kwamba alikuwa peke yake kwenye gari.
Kamanda alisema hakukuwa na kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea na kwamba gari hilo limehifadhiwa mahali salama kwa sababu halitembei.
Kamanda Massawe alisema mwili wa marehemu Sharo umehifadhiwa katika hospitali teule ya wilaya ya Muheza.
Marehemu Sharo alianza kujipatia umaarufu baada ya kushiriki kwenye filamu za vichekesho zilizokuwa zikitayarishwa na msanii mkongwe wa fani hiyo, Amri Athumani maarufu kwa jina la King Majuto.
Baadaye alijitosa kwenye fani ya muziki wa kizazi kipya, ambapo alifanikiwa kuteka soko la muziki huo baada ya kuibuka na kibao cha Chuki za nini.
Hivi karibuni, Sharo alijiongezea umaarufu zaidi baada ya kushiriki kutengeneza matangazo ya Kampuni ya Simu ya Airtel akiwa na King Majuto.
Blogu ya liwazozito inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Sharo.


AJALI YA SHARO MILIONEA PICHANI





HIVI ndivyo gari alilokuwa akiendesha msanii Sharo Milionea lilivyopata ajali katika barabara ya Segera-Muheza mjini Tanga jana saa mbili usiku. (Picha kwa hisani ya gazeti la Uhuru)





SWAHIBA wa aliyekuwa msanii nyota wa vichekesho na muziki wa kizazi kipya nchini, Hussein Ramadhani, maarufu kwa jina la Sharo Milionea, amesema marehemu alikuwa na sh. milioni sita kabla ya ajali.

Akihojiwa na kituo cha redio cha Clouds FM leo usiku, swahia huyo wa Sharo Milionea, Mussa Yussuf maarufu kwa jina la Kitale amesema alizungumza kwa simu na rafiki yake huyo na kumueleza kwamba alikuwa safari kwenda Tanga kumpelekea mama yake sh. milioni sita.

Kwa mujibu wa Kitale, alipata nafasi ya kuzungumza na Sharo Milionea muda mfupi kabla ya ajali hiyo na kupanga kwenda naye katika mazishi ya msanii mwenzao wa filamu, marehemu John Maganga aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita na kuzikwa jana.

Kitale alisema alifanya mazungumzo hayo na Sharo Milionea wakati alipokuwa safarini akirejea Dar es Salaam kutoka Iringa, ambako alikwenda kushiriki kwenye tamasha la Asante Tanzania, lililoandaliwa na msanii Sajuki na mkewe Stara.

Lakini wakati akikaribia kufika Dar es Salaam, Kitale alisema alishangaa alipompigia simu Sharo Milionea na kumueleza kwamba alikuwa safarini kwenda Tanga kumtembelea mama yake.
"Aliniambia hataweza kwenda kwenye mazishi ya Maganga kwa sababu alikuwa na mzigo muhimu aliokuwa akimpelekea mama yake Tanga. Aliniambia alikuwa akimpelekea mama yake shilingi milioni sita kwa ajili ya kazi muhimu,"alisema.

Kabla ya tukio hilo, Kitale alisema marehemu Sharo Milionea alimkaribisha katika nyumba mpya aliyopanga katika maeneo ya Magomeni, Dar es Salaam, ambapo alikuwa akilipa kodi ya shilingi laki mbili kwa mwezi.

Kitale alisema Sharo aliamua kuhamia kwenye nyumba hiyo mpya kwa lengo la kubadili hali ya maisha kwa vile mambo yalishaanza kumuendea vizuri, tofauti na alivyokuwa akiishi miaka ya nyuma.
Swahiba huyo wa Sharo Milionea alieleza kusikitishwa kwake na kitendo cha watu wa kwanza waliofika katika eneo la ajali kumvua marehemu nguo zote alizokuwa amezivaa na kumuacha akiwa na nguo ya ndani.

"Kwa kweli hawa watu wamefanya kitendi kibaya sana," alisema Kitale kwa sauti iliyojaa majonzi makubwa kutokana na msiba huo mzito wa swahiba wake.

Akizungumzia jinsi alivyopata taarifa hizo, Kitale alisema alipigiwa simu na mmoja wa rafiki zake na alishindwa kuziamini hadi alipowasiliana na King Majuto, hali iliyosababisha aishiwe nguvu.
Kitale alisema amempoteza mtu muhimu katika maisha yake na hajui ataendeleaje kushiriki katika fani ya vichekesho na muziki wa kizazi kipya bila ya Kitale

Source: Habari na Picha Liwazo Zito Blog 

2 comments:

  1. R.I.P SHARO MILIONEA MUNGU AKULAZE MAHALI PEMA PEPONI AMINH. TUNASHUKURU KWA MAZURI ULIYOYATENDA ANSANTE

    ReplyDelete
  2. TUNAMUOMBEA KWA MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA HLF JAMANI TUJIFUNZE KUWA SAFARI NDEFU TUWE TUNASHIRIKIANA TUSIPENDE KWENDA WENYEWE

    ReplyDelete