WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, November 22, 2012

TETESI: MMOJA WAO NDIYE ATAKAYESIMAMA KAMA MGOMBEA KWA TIKETI YA CCM MWAKA 2015




Hivi karibuni Chama Cha Mapinduzi(CCM) kupitia Mkutano wake Mkuu uliofanyikia mjini Dodoma, kimefanya mabadiliko katika safu yake ya juu ya uongozi. Na kama ambavyo ungetarajia,mkutano wa namna ile, ni sehemu muhimu ya kila aina ya hulka za kisiasa. Kuna kujitambulisha na kutambulishwa(networking). Kuna kuanzisha kampeni za chaguzi kubwa kubwa kama ile ya Urais mwaka 2015.

Miongoni mwa yale yaliyotokana na mkutano wa Dodoma wa #CCM, ni pamoja na tetesi.Kubwa zaidi ambayo nimeisikia mara kadhaa mtaani(na wanaopigia upatu tetesi hizo wanasema wanatizama vitendo zaidi ya maneno) ni kwamba miongoni mwa majina ambayo yanatajwa sana linapokuja suala la mgombea wa Urais kupitia #CCM ni yale ya Mh.Membe na Mh.Lowassa.

Kuna ukweli? Ikiwa kweli Je?Wanazo sifa?Wanao Uwezo?Maswali mengi,majibu haba.Tusubiri tuone!

source; Read more: BongoCelebrity 

No comments:

Post a Comment