WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, November 27, 2012

Kikwete amzibia ‘masikio’ Lissu


RAIS Jakaya Kikwete ameendelea kuteua majaji wapya licha ya madai kwamba baadhi ya majaji wanaowateua, hawana sifa.
Hivi karibuni, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, alitishia kumpeleka mahakamani Rais Kikweke, kwa madai kuwa amekuwa akiteua majaji wasiokuwa na sifa.
Jana kiongozi huyo wa nchi, aliwaapisha majaji wapya wa Mahakama ya Rufaa ambao ni Jaji Profesa Ibrahimu Juma na Jaji Bethewel Mmilla.

Kabla ya uteuzi huo Jaji Mmilla (56) alikuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, wakati Jaji Juma (54) alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Rais Kikwete pia aliwaapisha Jaji mstaafu John Mkwawa kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Winfrida Korosso kuwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria.
Akizungumza baada ya kuapishwa, Jaji Profesa Juma, aliwaasa wananchi kuwa na tabia ya kupenda kusoma hukumu na kupitia mwenendo wa kesi, ili wasipotoshwe.
Alisema upungufu wa majaji na mahakimu, unatokana na mfumo mzima wa sekta hiyo na kwamba jukumu la mahakama walilojiwekea kesi zote ziwe zimeisha ndani ya miaka miwili.
Naye Jaji Mkwawa, alisema watajitahidi katika uchaguzi mkuu ujao ili kuhakikisha kwamba matokeo yanatolewa kwa wakati.
Mwananchi

No comments:

Post a Comment