WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, November 30, 2012

Maalim Seif aongoza mamia kumzika mke wa Hamad Dar



Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza la marehemu Kissa Gwalugano Mohamed,ambaye ni mke wa Mbunge wa Wawi,Zanzibar Bw.Hamad Rashid Mohamed,kwenda msikitini na mazishi kufanyika jana jioni katika makaburi ya Kisutu,Dar es salaam.


Na Goodluck Hongo

MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, jana aliongoza mamio ya waombelezaji katika mazishi 
ya Kissa Gwalugano Mohamed ambaye ni mke wa Mbunge wa 
Wazi, Zanzibar Bw. Hamad Rashid Mohamed.

Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni Pamoja na Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Bw. Wiliam Lukuvi, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Ludovick Utouh.


Wengine ni Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda, Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba, Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa UDP, Bw. John Cheyo, viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa pamoja na wabunge.

Katika msiba huo, viongozi wa kisiasa waliweka pembeni tofauti zao na kumfariji Bw. Mohamed ambaye chama hicho kiliwahi kumfukuza uanachama.

Mazishi hayo yalifanyika Dar es Salaam jana katika makaburi ya Kisutu, saa kumi jioni.

Akizungumza kwa niaba ya familia, Profesa William Matuja aliwashukuru viongozi wote walioshiriki mazishi hayo kwani wamefarijika sana ingawa wamepata pigo kwa kifo hicho.

Marehemu alizaliwa Oktoba 20,1955 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, alisoma katika Shule ya Msingi Azimio, baadaye Sekondari ya Zanaki jijini Dar es Salaam.

Alisema baadaye alijiunga na masomo ya kompyuta na kuajira THB (iliyokuwa Benki ya Nyumba nchini), lakini alichana kazi na kuamua kujiajiri mwenyewe hadi mauti ilipomkuta.

Alifunga ndoa na Bw. Mohamed mwaka 1984 na walibahatika kupata watoto kati ya hao mmoja wa kiume. Marehemu alikuwa akilalamika kusumbuliwa na mgongo na baada ya kupimwa 
iligundulika kuwa na ugonjwa wa mifupa.

Marehemu alilazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Novemba 27 mwaka huu, baada ya kuzidiwa na kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi na kufariki saa tatu usiku.

Majira


1 comment:

  1. Jamani kuna ugonjwa wa mifupa ndiyo nini?? Arthritis?? OMG pole Uncle kwa msiba huu mkubwa jamani, she is too young to die. Yale yale ya seriously viongozi wetu mnahitaji kureview the health system in Tanzania. Just this week nimesoma habari za kusikitisha kuhusu vifo vya vijana ambao na uhakika vimesababishwa na UZEMBE WA MADAKTARI FOR NOT GIVING PROPER DIAGNOSIS OR PROPER TREATMENT.




    Viongozi washiriki mazishi ya mke wa mbunge wa jimbo la wawi , Hamad Rashid

     Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akimfariji Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF) Mhe. Hamad Rashid Mohd nyumbani kwa Mbunge huyo Mikocheni jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mke wake bibi Kisa Mohd.
     Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akimfariji Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF) Mhe. Hamad Rashid Mohd nyumbani kwa Mbunge huyo Mikocheni jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mke wake bibi Kisa Mohd.
     Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akimfariji Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF) Mhe. Hamad Rashid Mohd nyumbani kwa Mbunge huyo Mikocheni jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mke wake bibi Kisa Mohd. Kushoto ni Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba.
     Sheikh Abdallah Issa (kushoto), akiongoza dua ya kumuombea marehemu bibi Kisa Mohd nyumbani kwake Mikocheni Dar es Salaam.
     Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa na serikali katika Makaburi ya Kisutu aliposhiriki mazishi ya bibi Kisa Mohd, mke wa Mbunge wa Wawi (CUF) Mhe. Hamad Rashid Mohd.
     Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiweka mchanga katika kaburi la marehemu bibi Kisa Mohd, mke wa Mbunge wa Wawi (CUF) Mhe. Hamad Rashid Mohd aliyezikwa katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam. (Picha na Salmin Said, OMKR)
    Na Hasssan Hamad OMKR

    Viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa na serikali wameshiriki katika mazishi ya bibi Kisa Mohd ambaye ni mke wa Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF) Mhe. Hamad Rashid Mohd.
     Mazishi hayo yaliyofanyika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam na kuzikwa katika makaburi ya kisutu, yaliongozwa na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.

    Viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa UDP John Cheyo, Mwenyekiti wa ADC bw. Said Miraji na Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda.
    Mwili wa marehemu huyo ulisaliwa katika msikiti Maamur ulioko maeneo ya Upanga na baadaye kupelekwa katika makaburi ya Kisutu kwa ajili ya mazishi.

    Marehemu bibi Kisa Mohd alifariki Jumanne iliyopita baada ya kusumbuliwa na matatizo ya Presha kwa muda mrefu, na kuzikwa Alkhamis tarehe 29/11/2012.

    Akizungumza katika mazishi hayo, msemaji wa familia hiyo amewashukuru viongozi na wananchi waliojitokeza kushirikiana nao katika msiba huo, na kwamba familia imepoteza mtu muhimu ambaye pengo lake haliwezi kuzibika kwa kipindi kifupi.

    Imewekwa na MAPARA

No comments:

Post a Comment