WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, November 29, 2012

Safari Ya Mwisho Ya Sharo Milionea



                                                                
MAELFU ya waombolezaji jana walijitokeza kushiriki mazishi ya msanii Hussein Ramadhan maarufu kwa jina la Sharo Milionea, huku mamia wakizirai baada ya kushindwa kujizuia wakati mwili wake unawekwa kaburini.


Mwili wa msanii huyo ulizikwa jana kijijini kwake Lusanga wilayani Muheza saa 7 mchana, katika tukio lililomshirikisha Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ambaye alimwakilisha mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.


Waombolezaji walianza kumiminika kijijini Lusanga tangu juzi jioni na idadi yao iliongezeka zaidi jana asubuhi. Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi.Sala ya mazishi iliongozwa na Sheikh Twaha Juma ambaye baadaye aliamuru jeneza hilo kupelekwa makaburini, ambako waombolezaji kadhaa walipoteza fahamu.

20 wapelekwa hospitali
Miongoni mwa matukio yaliyojitokeza katika msiba huo ni baadhi ya waombolezaji kupoteza fahamu msibani.Matukio tofauti ya watu kuzirai yalitokea wakati mwili wa msanii huyo ulipokuwa unapelekwa nyumbani kwao kijijini Lusanga ukitokea Hospitali Teule ya Wilaya ambako ulihifadhiwa tangu alipopata ajali Jumatatu usiku na wakati wa mazishi.

Miongoni mwa waliopoteza fahamu katika msiba huo ni wasanii na waigizaji wa filamu waliokuwa wakiigiza na Sharo Milionea wakati akiwa katika kundi la AL Riyam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na MC wa shughuli hiyo, Steve Nyerere, zaidi ya watu 20 walipoteza fahamu katika msiba huo na kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Muheza.


DC Mgalu aliwaomba waombolezaji kutokuwa na shaka juu ya waliopoteza fahamu kwa kuwa madaktari maalumu walikuwa wameandaliwa hospitalini hapo kwa ajili ya kuwapa huduma.
Mwananchi lilifika katika hospitali Teule na kukuta waliokuwa wamepoteza fahamu, wengi wao wakiwa ni wasichana, wakipata huduma huku wengine wakiomba kupewa ruhusa ili wakahudhurie maziko.

JK atuma rambirambi
Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara kutokana na vifo vya wasanii watatu vilivyotokea hivi karibuni, kikiwamo cha Sharo Milionea.


Taarifa iliyotolewa jana Dar es Salaam na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ilisema kuwa Rais Kikwete ameshtushwa na vifo hivyo vya ghafla.
Wasanii hao ambao walifariki dunia katika mazingira tofauti ni Mwigizaji wa Kundi la Kaole, Khalid Mohamed ‘Mlopelo’ aliyefariki dunia hivi karibuni kutokana na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua kwa muda mrefu

Soma zaidi:  http://www.mwananchi.co.tz/habari



Mkuu Wa Wilaya Na Nape Wamzika Sharobaro

  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (Watatu kulia, waliobeba jeneza) akishiriki kubeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi, kwenye mazishi ya msanii huyo, leo kwenye Kijiji cha  Lusanga, Muheza Tanga.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa pole za Chama Cha Mapinduzi (CCM) alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea,leo kwenye Kijiji cha  Lusanga, Muheza Tanga
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nauye, akitupa mchanga kaburini, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea,leo kwenye Kijiji cha  Lusanga, Muheza Tanga.
 Mkuu wa wilaya ya Muheza, Subra Mgalu akisoma salam za Shirika la Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) la Mama  Anna Mkapa, kwenye msiba huo. Pamoja naye ni Nape

 (Picha na Bashir Nkoromo).


No comments:

Post a Comment