WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, November 19, 2012

Maalim Seif aendelea na Ziara ya kichama Kigoma


 

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikagua ujenzi wa skuli ya sekondari ya Amahoro katika kijiji cha Mgaraganza Wilaya ya Kigoma Vijijini.

 

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mgaraganza Wilaya ya Kigoma Vijijini, kabla ya kukagua ujenzi wa Skuli yao ya Sekondari ya Amahoro.

 

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wafuasi na wapenzi wa Chama hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kigoma mjini

Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Ibrahim Lipumba akizungumza na wafuasi na wapenzi wa Chama hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kigoma mjini.

Na Hassan Hamad , Kigoma

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema skuli nyingi za vijijini bado zinakabiliwa na upungufu wa walimu pamoja na vifaa vya kufundishia.

 Amesema hali hiyo inapelekea kutolewa kwa elimu isiyo bora ambayo husababisha vijana wengi kushindwa kupata ajira baada ya kuhitimu masomo yao.

 Maalim Seif ameeleza hayo katika ziara yake ya kutembelea ujenzi wa skuli ya sekondari ya Amahoro katika kijiji cha Mgaraganza Wilaya ya Kigoma Vijijini.

Amesema ili kuwajenga vijana kitaaluma, ni lazima waandaliwe kwa kupatiwa elimu bora ambayo itaweza kuwasaidia katika maisha yao ya baadae.

 Katika risala yao iliyosomwa na mjumbe wa kijiji hicho bwana Said Seif Wagara, wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuwasaidia ili waweze kukamilisha jengo la utawala, ili hatimaye skuli hiyo iweze kufunguliwa na kuanza kazi.

 Wakati huo huo Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF amehutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho katika viwanja vya Kigoma Mjini, na kuwashauri wale waliokihama chama hicho kurejea ili waweze kuongeza nguvu ya kutetea haki za wananchi.

 Amewaambia wananchi wa Kigoma kuwa Chama cha CUF bado kipo na kinaendelea kuimarika katika maeneo mbali mbali ya Tanzania, hasa baada ya kuzinduliwa kwa operesheni mchakamchaka hadi mwaka 2015.

 Amesema CUF ni chama chenye malengo ya kuwakomboa Watanzania kiuchumi, kisiasa na kijamii na kuwaomba wananchi wa Kigoma kuendelea kukiunga mkono chama hicho ili kiweze kufikia malengo yake.

 Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Ibrahim Lipumba amewataka vijana wa Kigoma kusoma na kuifahamu historia ya nchi yao ili kujua malengo halisi ya kupigania uhuru kutoka kwa wakoloni.

 Amesema Mikoa ya Magharibi ya Tanzania ikiwemo Tabora na Kigomailichukua nafasi kubwa katika kubigania uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, lakini bado imeachwa nyuma kimaendeleo, na kuwataka vijana kuweka mikakati maalum ili waweze kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi katika mikoa hiyo.

 Akizungumzia kuhusu maendeleo ya kiuchumi katika mikoa hiyo ya Magharibi, Prof. Lipumba ameelezea haja ya kuimarishwa kwa miundombinu ya barabara na reli ili kurahisisha shughuli za kilimo na biashara.

Amesema iwapo miundombinu hiyo itakuwa imara, Mkoa wa Kigoma unaweza kuwa kituo kikukuu cha biashara na kuweza kuwaunganisha kibiashara wananchi wa Kigoma na Kongo ya Mashariki yenye idadi ya watu wapatao milioni 30.

 Amefahamisha kuwa Mkoa wa Kigoma una fursa nyingi za kiuchumi ikiwemo jiografia ya mkoa huo, na kwamba iwapo zitatumika vizuri zinaweza kuwanufaisha wananchi wa eneo hilo na kuwezakuondokana na ukosefu wa ajira.

Imewekwa na MAPARA

 

No comments:

Post a Comment