WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, March 9, 2016

MIEZI MINNE YA DR. JOHN POMBE MAGUFULI NA TANZANIA MPYA:-

 

JE FALSAFA YA MHESHIMIWA MAGUFULI YA HAPA NI KAZI TU NI SAWA NA  SEMI HIZI?

Kumpa mtu samaki utakuwa umemlisha katika siku ya leo; ukiweza  Kumfundisha mtu  namna ya kuvua samaki  utakuwa umeweza kumsaidia kumlisha katika maisha yake yote.

Ukiweza kumfundisha mtu namna ya kutengeneza na kusafirisha na kuweza kuuza samaki katika masoko ya nje; utakuwa umefanikiwa kuchochea maendeleo ya kiuchumi

Raisi Magufuli toka aliposhika nafasi ya kuliongoza Taifa la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ameendelea kuwa gumzo la utendaji uliotukuka hasa akipigania maendeleo ya wananchi Masikini. Amekuwa na maono ya  uzalendo wake kwa kujitoa kwa kusimamia vizuri rasilimalia za taifa letu. Ameweza kuonyesha umahili katika kusimamia nidhamu ya utendaji katika Wizara na idara zote za serikali, huku akibana matumizi ili kuelekeza nguvu zaidi katika miradi ya maendeleo ambayo inawagusa wananchi moja kwa moja.

Raisi magufuli katika kipindi hiki kifupi amweza kujijengea sifa ya kuwa "unforgettable" miongoni mwa viongozi wa juu wa Tanzania na amekuwa kipenzi cha wanyonge ambao wanamwona kama mkombozi wao katika shida na umasikini wao. Mfano maauzi yake ya haraka ya kuwanusuru wagonjwa waliokuwa wanalala chini katika hospitali zetu; vitendo kama hivyo wananchi wananwmona Dr. Magufuli kama Kiongozi mwenye  maono ya   maendeleo ya nchi yake:

Katika kipindi hiki kifupi ameweza kusimamia ukusanyaji wa mapato ya serikali ambayo yameongezeka sana na kusaidia katika kupunguza utengemezi hasa katika bajeti ya maendeleo ambayo tulikuwa tunategemea sana ufadhili na kukwamisha shughuli za msingi za maendeleo ya Taifa letu. Amekuwa kiongozi ambaye ameonyesha uwezo wa Kujenga na kuboresha uchumi, wetu katika siku zijazo mbele; Ameweza pia kukuza mifumo ya kiutawala na sera zinazolenga zaidi katika kusimamia maisha na ukuaji wa uchumi wa nchi ili tuweze kuondokana na tatizo kubwa la umasikini wa Taifa letu.

Nimejaribu kueleza hayo yote ili kuonyesha kuwa bila kuwa na uongozi wenye maono usiotafuta faida yake wenyewe, usiokuwa tayari kuwawajibisha watendaji wabovu na wanaokiuka maadili na uvunja sheria  hatuwezi kutoka hapa tulipo, tutaendelea kufurahia kauli mbiu ambazo hazina maana wala msingi mkubwa kwa maendeleo ya Taifa.

Kwa sasa Taifa linamwitaji kiongozi mwadilifu, mkweli ambaye anaweza kupambana na matatizo ya rushwa na ufisadi bila kuyaonea aibu. Ili kulivusha Taifa la Tanzania katika mabadiliko ya maendeleo ambayo kama taifa tunayahitaji kwa sasa; tunahitaji Kiongozi ambaye anauchungu sana na nchi yake hasa katika kuwasaidia wananchi ambao ni wanyonge ambao wanahitaji mkate wao wa kila siku na watoto wao waweze kwenda shule; Tumeliona hili kwa Raisi wetu Dr. Magufuli amekuwa msimamizi wa khali ya juu wa utekelezaji wa mpango wa mabadiliko ambayo kama taifa tunayahitaji kwa sasa; katika kampeni alituhahidi kuwa  hana mchezo hata kidogo katika hili  na hatakuwa na msamaha kwa wale wote ambao hawatafikia malengo ambayo serikali yake imeainisha kutekeleza.

Ameshatoa onyo kwa viongozi na wafanyakazi kuwa hayuko tayari kuona kuwa rasilimali ya taifa zinachezewa na wajanja wachache, ikibainika serikali yake itawafukuza kazi bila huruma;  Kwa Dr, Magufuli  ufanisi utakuwa unapimwa kwa uwajibikaji na uadilifu na sio propaganda za kisiasa.

Mheshimiwa Magufuli amepania kurudisha kwenye kamusi maneno uwajibikaji na uwajibishaji kwa watendaji wa serikali katika taasisi zake na idara zake,  na ameamua kuondoa kabisa kwenye kamusi maneno kama utashi wa kisiasa urafiki na undugu na michakato katika kutekeleza wajibu katika majukumu yako ya kikazi.

Mheshimiwa Magufuli anaamini kuwa  hakuna maendeleo ya kweli kama tutaendelea kuendekeza utashi wa kisiasa; ni dhahiri kuwa tuwe tayari kuhesabu kuwa hakuna maendeleo ya haraka yatapatika katika nchi yetu bado tukiwa tunatawala na michezo michafu ya siasa; tukumbuke kuwa majukumu  ya kiserikali yanatakiwa kuzingatia zaidi, misingi yake ya utendaji, na utaalamu, nidhamu na ukweli na sio kuendekeza  urafiki na undugu. 

Mheshimiwa Magufuli amethubutu na amejitangazia wazi kuwa yeye ni sadaka ya watanzania katika kupambana na ufisadi na yuko tayari kujitoa Muhanga ili tu watanznaia wanyonge waweze kunufaika na rasilimali za taifa lao.

Mheshimiwa Magufuli utendaji wake unaongozwa na kauli mbiu ya sitawaangusha: Hapa Ni Kazi Tu; katika imani kuwa ameona umasikini na tabu ya Taifa letu hivyo kama watanznia walivyojenga imani kwake hivyo naye ameweka juhudi zote katika kusimamia kwa dhati kabisa rasilimali za Taifa ili kurudisha matumaini makubwa kwa serikali yake anayoiongoza kwa wananchi kwa maendeleo yao.

Binafsi kama mtanzania na mfuatiliaaji wa utendaji wa kazi  Dr. John Pombe   Magufuri,   pamoja  na  mapungufu yake kama binadamu amekuwa miongoni mwa viongozi wachache ;   kama  kiongozi wa juu kabisa hataki kuona watendaji ambao wako chini yake wanatenda kazi kwa mazoea; daima ameonyesha kuthubutu katika kutekeleza sheria na kuwashugulikia watendaji wabovu  huku akiwa tayari kufuata sheria na kujielimisha ili aweze kuzielewa zaidi sheria  za nchi na wizara husika;  

kwa keli ni ni msimamiaji mzuri  wa sheria katika utendaji hata  kama  wakati  mwingine  maamuzi yake yanakuwa kero kwa kwa watendaji wenzake wanaomzunguka lakini bado yanafaida kubwa kwa jamii ya Kitanzania. Kimsingi    kama  nilivyoainisha  hapo  juu  inawezekana  magufuli  akawa  na  madhaifu  yake  lakini  huwezi  kuondoa ukweli kuwa katika kipindi hiki kifupi cha uongozi wake amekuwa kiongozi mzuri wa Juu aliyeweza kufanya  vizuri katika kazi ya kusimamia hata kuchukua hatua kali kwa wakati dhidi ya wale wote ambao wamekuwa na hawafuati maadili ya kazi na vinara wote wa Rushwa na Ufisadi. Hilo  hata     wananchi   wa  kawaida  wameliona hilo nao wamempa tano.

Ni ukweli  ni wazi  kuwa  Magufuli ni kiongozi mchapakazi  na msimamizi mzuri  “Mnyonge mnyongeni  lakini  haki yake mpeni, wengi tunamtambua Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya, tunakuomba uendelee kufanya hivyo hivyo na  Serikali yake ya awamu ya tano iendelee kujiepusha kufanya kazi na watendaji wabovu:  

Watanzania wamemchagua mheshimiwa Magufuli kwa sababu utendaji wake kazi mzuri na kuwa kiongozi ambaye ameonyesha kiwango cha juu cha maadili; na ameonyesha katika kampeni zake kuwa yuko tayari kuwavusha wananchi  kuelekea katika bandari ya salama na yenye amani na maisha bora.

Magufuli ameonyesha upendo wa juu kabisa sio tu kwa watanzania wote bila kujali itikadi zao au dini zao au makabila yao. Ni kiongozi ambaye anaonyesha  upendo kwa wananchi wote; kwake uongozi ni kwa ajili ya wote na sio watu wachahce tu.

Tukumbuke kuwa kuwa uongozi ni dhana nzito ya kuaminiwa ambayo unakabiziwa na watu; lakini na kwa  kuwa uongozi wa kweli ni matokeo ya kuwa na maadili mazuri. Tukumbuke kuwa kuweza kutekeleza majukumu yako vizuri, Lazima kuwe na uhuisano wa karibu kati ya uongozi na mwongozo.
 
Mheshimiwa Magufuli tunaweza sema kuwa  amejitambua mwenyewe kuwa kazi moja ambayo anakabiliwa nayo ni kuwaletea mabadiliko wananchi wa Tanzania hivyo amejiaamini YeYe mwenywe kuwa anaweza kufanya hivyo hivyo anayo mizizi ya huruma na uvumilivu ndani  na ni mtu ambaye haogopi kushindwa

Kiongozi bora atahangaika kuhakikisha kuwa maisha ya wananchi wake yanasonga mbele na kuwa na misha bora. Ukiwa mnyonyaji wewe ni kiongozi mbovu; viongozi ni viashiria vya mabadiliko katika jamii, na kuendeleza mafanikio tukumbuke kuwa sio vigumu kumtawala mtu ila jukumu ni kumwendeleza mtu.

Viongozi wanaishi kwa kuelewa mazingira na tabia za watu; kiongozi lazima awe tayari kuyapokea mabadiliko kila kitu kinaendelea kubadilika; kiongozi lazima ajue kuwa haitakiwi kuogopa awe tayari kujifunza na kamwe ahitimu shule ya mabadiliko, kiongozi lazima awe tayari kuishi na mabadiliko ya tamaduni. kiongozi mzuri anajua mapungufu ya watu wake, mapungufu yetu yanakamilishwa na wengine ambao wanautaalamu zaidi.

uvumilivu ni nguzo muhimu kwa viongozi wazuri ( role model). kiongozi mzuri lazima ajue kuwa kushindwa ni sehemu ya uongozi bora kwani inakupa nguvu ya kuanza upya, unawapenda watu wako kama huwapendi basi usiwe kiongozi hata kama watu hawakupendi bali kama kiongozi bado unatakiwa kuwajali.

kiongozi lazima ujifunze kutokuona wivu wa mafanikio ya watu wengine sio kukosoa kila kitu hata kama mwenzako amefanya vitu vizuri tabia ya kupongezana ni nzuri sana kwa kiongozi mwenzake. viongozi ni wabunifu ambao wanatakiwa kuleta mabadiliko na kuleta utamaduni wa kazi na kudumisha utamaduni wa mafanikio ni wajibu wa kiongozi mzuri, kwa hiyo viongozi wanatakiwa kuwa viashiria wa mabadiliko ya kweli kwa taifa.

 
kiongozi wanatakiwa kuwa na mawazo mazuri ya kimaendeleo na kujua namna ya kuyatumia kwa ajili ya maendeleo ya watu wao na kwa faida ya watu wao, mgonagano wa mawazo ni sehemu tu ya uongozai mzuri. kiongozi hatakiwi kuhangaika wakati kunatokea matatizo ndani ya uongozi kila kitu kipo kwenye mpito. kiongozi lazima uelewe kuwa yale uliyojifunza shuleni wakati mwingine hayafnayi kazi wakati wote na tayari kufahamu kuwa kufanyia utafiti mabadiliko ya tamaduni za uongozi wako.

VIVA MAGUFULI TUNAKUJUA WEWE NI:

Ni Jembe:
Ni Tingatinga
Ni Mtumishi wa watanzania wote
Unayajua mapungufu yako.
Unaongoza kwa usemi wa sisi sisi.
Ni Mnyenyekevu na mtumishi wa watu wote.
Ni mwadilifu
Mtu wa watu hasa wanyonge
Ni Mwogopa Mungu

VIVA MHESHIMIWA  JOHN POMBE MAGUFULI RAISI WA AWAMU YA TANO MWENYEZI MUNGU AKUPE NGUVU YA KULIVUSHA SALAMA TAIFA LA TANZANIA KATIKA MIAKA HII MITANO KATIKA MAENDELEO AMBAYO  SISI WATANZANIA TUMEYASUBIRI KWA MIAKA MINGI SANA;

UKADIRIFU INAKUTAKIA UONGOZI BORA MIEZI HII MINNE YA UONGOZI WAKO KAMA RAISI WA AWAMU YA TANO