WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, November 23, 2012

RAGE: HATUNA MATATIZO NA FRIENDS OF SIMBA, HANSPOPE ATAKA MKUTANO WA DHARULA



 
Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage amesema uongozi wake hauna ugomvi wala matatizo na kundi la wanachama, maarufu kwa jina la Friends of Simba.
Rage amesema wanawaheshimu baadhi ya wanachama wa kundi hilo kwa sababu wamekuwa wakitoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya klabu.
Hata hivyo, Rage amesema wapo baadhi ya wanachama wa kundi hilo, ambao hawautakii mema uongozi wake kwa vile wamekuwa wakishirikiana na makundi ya wanachama kuchochea vurugu.
Alisema kinachosikitisha ni kwamba, wanachama wa kundi hilo wanawafahamu vyema wenzao wachache wenye lengo la kuchochea vurugu, lakini hakuna hatua zozote walizowachukulia.
Rage amesema iwapo hali itaendelea kuwa hivyo, uongozi wake utalazimika kuwataja wanachama hao ili wafahamike na wahukumiwe kutokana na matendo yao.
"Si kweli kabisa kwamba uongozi wa Simba hauelewani na wanachama wa Friends of Simba. Tunawaheshimu sana kwa sababu baadhi yao wamekuwa wakitumia fedha zao nyingi kwa manufaa ya Simba,"alisema Rage.
"Lakini wapo baadhi ya wanachama wa kundi hilo miongoni mwao, ambao wamekuwa mstari wa mbele kuchochea vurugu kupitia katika baadhi ya matawi, lengo lao kubwa likiwa ni kuuondoa uongozi uliopo madarakani ili wakae wao,"aliongeza.
Akizungumzuia ombi la kuitishwa kwa mkutano wa dharula, Rage alisema uongozi wake hauna kinyongo na ombi hilo la wanachama, isipokuwa wanapaswa kufuata taratibu na katiba ya klabu hiyo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hanspope amesema suluhusho pekee la mgogoro uliojitokeza sasa Simba ni kuitishwa kwa mkutano wa dharula wa wanachama ili waweze kujadili matatizo yaliyojitokeza na kuchukua hatua.
Alisema baadhi ya wanachama wa friends of Simba, akiwemo yeye wamekuwa wakiisaidia klabu hiyo kwa mapenzi yao wenyewe na katu hawana malengo ya kutaka uongozi.
Hata hivyo, alisema anashangaa kuona kuwa, wanachama hao hawakusema lolote katika mkutano ulioitishwa na uongozi hivi karibuni, badala yake wanazusha hoja ya kutaka uitishwe mkutano wa dharula hivi sasa



 

KLABU ya Simba imeiunda upya kamati yake ya usajili na kumrejesha mfanyabiashara, Zacharia Hanspope kuwa mwenyekiti.


Kamati hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alipozungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam.

Rage alitangaza kuzivunja kamati zote ndogo za Simba wiki iliyopita kwa madai ya kutokuwa na mchango wowote kwa klabu.

Kuvunjwa kwa kamati hizo kulikwenda sambamba na kufutwa kwa tawi la Mpira Pesa lenye maskani yake Magomeni, Dar es Salaam kwa madai ya kuchochea vurugu klabuni.

Rage alisema ameamua kumrejesha Hanspope katika wadhifa wake huo kutokana na mchango mkubwa alioutoa katika kusajili wachezaji wapya msimu huu kwa kutumia fedha zake.

Aliwataja wajumbe wengine watakaokuwa wakiunda kamati hiyo kuwa ni mfadhili wa zamani wa klabu hiyo, Azim Dewji, mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani, maarufu kwa jina la Maji Marefu, Muhsin Ruhwey na Sued Nkwabi.

Rage alisema anatarajia kutangaza majina ya wajumbe wengine wa kamati hiyo hapo baadaye.

Kamati zingine ndogo za Simba zilizovunjwa ni ya ufundi, iliyokuwa ikiongozwa na Ibrahim Masoud 'Maestro', kamati ya nidhamu iliyokuwa chini ya Jamal Rwambow, kamati ya mashindano iliyokuwa chini ya Joseph Itangare 'Mzee Kinesi' na kamati ya fedha iliyokuwa chini ya makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Geofrey Nyange 'Kaburu'.

Kwa mujibu wa Rage, atatangaza wajumbe wapya wa kamati hizo hivi karibuni baada ya mchakato wa kuwateua kumalizika.

source: Liwazo Zito blog

No comments:

Post a Comment