WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, October 24, 2012


Serikali Ya Zanzibar Kuchunguza Kutekwa Kwa Kiongozi Wa Uamusho 

  
Na Habari Maelezo Zanzibar 24/10/2012


            SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR IMEVITAKA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA  NCHINI KUFANYA UCHUNGUZI WA KINA ILI  KUBAINI  KIINI  CHA KUTOWEKA   SHEIKH FARID HADI  AHMED NA CHANZO CHA VURUGU ZILIZOTOKEA NCHINI WIKI ILIYOPITA..

KWA MUJIBU WA TAARIFA  ILIOTOLEWA NA WAZIRI WA NCHI AFISI YA MAKAMO WA PILI WA RAIS  ZANZIBAR MH. MOHAMMED ABOUD AMESEMA
KUTOWEKA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA  KWA SHEIKH FARID KULIPELEKEA KUZUKA KWA MACHAFUKO KATIKA MAENEO KADHAA YA MJI WA ZANZIBAR AMBAPO MALI ZA WATU ZILIPORWA NA KUHARIBU MIUNDO MBINU YA BARABARA NA KUCHOMA MOTO MASKANI ZA CCM..

HIVYO ILITAKA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUFANYA TATHMINI ILI KUJUA KIWANGO CHA HASARA KILICHOTOKANA NA VURUGU HIZO NA  KUWACHUKULIA HATUA  ZA KISHERIA WALE WOTE WATAKAOBAINIKA KUHUSIKA NA KADHIA NZIMA YA SHEIKH FARID,VURUGU NA MAUAJI YA ASKARI KOPLO SAID ABRAHMANI HUKO  BUBUBU WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA.

AIDHA VYOMBO HIVYO VIMETAKIWA KUENDELEA NAKUDHIBITI  HALI YA USALAMA WA NCHI KWA WAKATI WOTE KWA VILE VITENDO HIVYO
VIMEKUWA VIKIJITOKEZA MARA KWA MARA NA KUHAKIKISHA KWAMBA HAVIREJEI TENA.

TAARIFA HIYO ILIENDELEA KUSISITIZA WANANCHI KUACHA VITENDO VYENYE KUHATARISHA AMANI NA UTULIVU ULIOPO NCHINI KWA VILE CHUKI NA FUJO SIKU ZOTE KAZI YAKE NI KUBOMOA NA SIO KUJENGA.

MH. ABOUD ALIENDELEA KUSEMA KUWA  WALE WOTE WENYE DHAMIRA YA KUGOMBANISHA  WANANACHI NA SERIKALI YAO  NI VYEMA WAACHE KUFANYA HIVYO BALI JAMBO LA MSINGI  NI KUDUMISHA MASHIRIKIANO  ILI KUJENGA NCHI YETU KWA MASLAHI YA TAIFA NA VIZAZI VIJAVYO.
AMESEMA KUWA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR INAWASHUKURU WANANCHI WOTE KWA USTAHAMILIVU WAO NA PIA KUVISHUKURU VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KWA KAZI NZURI WALIOIFANYA  KUTULIZA FUJO NA VURUGU AMBAPO HIVI SASA HALI IMEREJEA KUWA  YA UTULIVU.
 ALIONGEZA KUWA HIVI SASA  VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VINAENDELEA KUDHIBITI HALI HIYO NA KUWAOMBA WANANCHI WAENDELEE NA SHUGHULI ZAO ZA KAWAIDA BILA YA WASIWASI.

KUHUSU UCHUMI WANCHI, ALISEMA KUWA ADUI MKUBWA WA UCHUMI  NI KWA NCHI KUINGIA KATIKA VURUGU NA MACHAFUKO KUNAKOPELEKEA KUVUNJIKA KWA AMANI NA UTULIVU  AMBAPO ZANZIBAR UCHUMI WAKE MKUBWA NI KUTOKANA NA SEKATA MAMA YA UTALII AMBAO HUATHIRIKA SANA KUKIKWA HAKUNA AMANI NA UTULIVU NA KUREJESHA NYUMA MAENDELEO NA KUZIDISHA HALI YA UMASIKINI JAMBO AMBALO HUONGEZA UPUNGUFU WA AJIRA KWA VIJANA WETU

WAZIRI HUYO  AMEWASIHI WANANCHI WA ZANZIBAR HASA VIJANA KULINDA AMANI YA NCHI AMBAYO NDIO RASILMALI KUU YA TAIFA.

ALISEMA KUWA PANAPOTOKEA TATIZO AU CHANGAMOTO YA AINA YOYOTE KWA MUJIBU WA MISINGI YA UTAWALA BORA NA WAKIDEMOKRASIA  NI BUSARA KUFANYIKA KWA MAZUNGUMZO MIOUNGONI MWA WADAU WAHUSIKA.

TAARIFA HIYO IMEONGEZA KUWA  WAZANZIBARI WOTE NI NDUGU, NI WATU WAMOJA  HAKUNA BUDI KUPENDANA, KUAMINIANA, NA KUSAIDIANA KWA HIVYO VIACHWE VITENDO VYENYE KUHATARISHA AMANI NA UTULIVU ULIOPO CHUKI NA FUJO HAZINA NAFASI KATIA ULIMWENGU HUU, KWANI VITU HIVYO KAZI YAKE NI KUBOMOA  NA SI KUJENGA

I SHEIKH FARID NA WENZAKE WANATARAJIWA KUFIKISHWA TENAKATIKA MAHKAMA YA MWANAKWEREKWE  HAPO KESHO .

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR. 24/10/2012

No comments:

Post a Comment