WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, October 28, 2011

JE UVUMILIVU NI KARAMA AU MAZOEA


UVUMILIVU HUJENGWA NA MISINGI GANI?



Naanza kwa kujiuliza kuwa “tulichonacho sisi wananchi je ni subira?; na baadhi ya viongozi wetu je wanao uvumilivu?  

Kwa haraka haraka tu Uvumilivu ni uwezo wa, au ni mazoezi ya, kutambua na kuheshimu imani au matendo ya wengine; uvumilivu uko katika kila nyanya ya maisha yetu, kuanzia maisha yetu ya kila siku;TATIZO katika maisha ya kawaida sana, swala la uvumilivu halizungumzwi sana, kwani uvumilivu unahusishwa na familia au kikundi kidogo cha watu; katika level hii uvumilivu huzungumzwa sana katika kuimarisha  maisha ya ndoa;


Uvumilivu huongelewa sana kwa mapana hasa katika maswala ya uongozi, uongozi ni hali ya kuongoza nchi katika mwelekeo wa kuleta maendeleo na ni ukweli kama mwandishi mmoja alipowahi sema kuwa “ KUONGOZA watu na hasa wa watu wazima ni kazi nzito inayohitaji mtu anayepewa jukumu hilo kuwa makini, vinginevyo mambo yanaweza kuwa magumu na hatimaye kuangukia katika mtego wa udikteta.  Hii inatokana na kukosekana mambo makubwa matatu ambayo ni ufahamu au maarifa, hekima na  hasa uvumilivu. Kiongozi asiye mvumilivu anaweza kujikuta anatumia mabavu kutawala ili watu wajue kuwa yupo, ana nguvu na ana mamlaka”.


Ni ukweli ulio wazi kuwa  kiongozi anatakiwa kuwa, mtulivu, mvumilivu na anayetumia zaidi hekima kuliko mabavu”, kiongozi anatakiwa Kuwa na  msimamo wa uvumilivu ni moja ya kazi ngumu zaidi miongoni mwa viongozi dhidi ya wananchi katika jamii. Ni ukweli ambao haufichiki kuwa  viongozi hawakuzaliwa wakiwa wavumilivu, lakini lazima tujifunze kuwa wavumilivu. Katika siasa uvumilivu wa kisiasa unakuza  utamaduni wa utawala bora na ukomavu wa demokrasia; na Kwa demokrasia kufanya kazi vizuri, wananchi lazima kuwa tayari kuvumilia na kuvumiliana.



Dhana ya uvumilivu ni ya msingi sana kwa maendeleo kwani inaruhusu mawazo mapya ndani ya jamii; kupitia dhana hii ya uvumilivu, kiongozi anakuwa  tayari kukubali  na kuheshimu  maoni na mawazo ya watu wengine na haki zao kwa uwazi na uhuru. Katika hali hii,uvumilivu huruhusu kuwepo kwa vyombo  huru vya habari kutumika kama chombo muhimu kuwahabarisha wananchi na kuwasilisha madai yao kwa viongozi wao. Demokrasia inahitaji vyombo vya habari amabvyo hugeuka kuwa daraja la mawazo kati ya viongozi na waongozwa. Vyombo huru vya habari husaidia   wananchi kuelewa taratibu ambazo zinaimarisha demokrasia.uvumilivu wa viongozi huru utasaidia kueneza demokrasia  na uwajibikaji kwani wananchi wataweza kukosoa serikali na ujumbe kufikishwa serikalini bila kuogopa.


ni ukweli kuwa Falsafa ya Uvumilivu hufunza na kuwakumbusha viongozi wanatakiwa kuishi kulingana na fikira njema. Mwenye kuifuata falsafa ya uvumilivu hayuko tayari kuamsha fikra mbaya za udikteta bali daima atajitaidi kuziepusha kwa kuendeleza uamuzi  wa uwazi na kwa kutumia njia  ya utulivu wa hekima kupitia uzoefu makini wa kimantiki: Kiongozi mwenye uvumilivu daima hutafakari, na kuziweka fikira mahali pamoja kabla ya kufanya uamauzi.Msingi wa kimaadili wa falsafa ya uvumilivu  kama mtaalam mmoja alivyo wahi kusema kuwa "zuri liko katika hali ya nafsi, yenyewe, inaonyeshwa katika hekima na kujidhibiti, hivyo kuboresha ustawi wa kiroho: Fadhila inatokana na nia ambayo inawiana na Maumbile. Kanuni inatumika katika uhusiano wa kibinafsi, yaani: kuwa huru kutokana na hasira, na wivu"

kwa ufupi tunaweza kusema kuwa uvumilivu umesheheni nini?
·        Tendo lililojaa subira kubwa,
·        Tendo ambalo kama linafanywa na kiongozi wa nchi basi anatoa uhuru mkubwa kufanya mambo bila kuingiliwa na nguvu za Ikulu,
·        Tendo lililojaa utu,
·        Tendo kwa serikali kuwa tayari kukosolewa na watu binafsi au vyombo vya habari.
·        Tendo ambalo linaashiria uwajibikaji wa serikali na utumishi wenye tija katika kwa taifa na wananchi wake katika kukuza demokrasia

Ni ukweli ambao haufichiki kuwa viongozi wetu wakiwa wavumulivu katika uwajibikaji wao mara moja  hurudisha imani ya wananchi dhidi ya serikali yake, upendo na matumaini katik ya viongozi na wananchi huongezeka pia: Tukumbukwe kuwa Ingawa watu wengi kufikiria uvumilivu ni upole  na kuto wajibika la hasha uvumilivu ni uwajibikaji ulio jaa busara na subira;


Swali lakujiuliza tunavyoelekea kusherekea miaka 50 ya uhuru wa Taifa letu je viongozi wetu katika awamu zote katika serikali yetu ya Muungano waliutumiaje uvumilivu katika kutekeleza majukumu yao?

Je uvumilivu wa kipindi cha mapambano ya uhuru wa taifa letu Bara  na visiwani katika miaka hiyo ni sawa na uvumilivu wa leo?

Je uvumilivu baiana ya vyama vya kisiasa ukoje? Ni kweli kuwa wanavumiliana katika kuchangia hoja katika mambo mbali mbali yanayohusu maendeleo ya Taifa letu?


Je hali ya viongozi wetu na vyama vyao wakati wa chaguzi mbalimbali uvumilivu hutawala kampeni zao?

Kuna maswali mengi sana ya kujiuliza hasa katika kipindi hiki cha kuelekea miaka 50 ya uhuru wa taifa letu na nini kifanyike baadaya ya sherehe hizo kwa manufaa ya taifa letu la Tanzania

MUNGU IBARIKI TANZANIA KUELEKEA MIAKA 50 YA UHURU

No comments:

Post a Comment