“HONORIS CAUSA”
Kama ilivyoelezwa na wataalum wa vyuo vikuu
ambavyo ndio watoaji wa Shahada ya Heshima “ Honoris Causa” kuwa;
shahada
ya heshima ni ile itolewayo kwa mtu mwenye vigezo stahiki na aliyetoa mchango
mkubwa wa maarifa, elimu au ujuzi katika eneo fulani la kitaaluma.
Kwa
kawaida shahada hizi hutolewa kama njia ya kuheshimu na kutambua michango ya
watu hao katika maarifa, ujuzi au eneo la kitaaluma kwa mfano, afya, uchumi,
mazingira, sayansi au fasihi,
mtunukiwa wa shahada
hiyo hapasi kuwa na uhusiano wa awali na taasisi inayompa heshima hiyo.
Mtu
anayependekezwa kupewa shahada katika chuo chetu ni yule aliyetoa mchango
mkubwa kwa umma au kwa taifa na sio lazima mchango katika taaluma bali ni kazi
ya ziada yenye manufaa kwa umma nje ya wajibu wake wa kazi.
Mheshimiwa Dr.
Jakaya Mrisho Kikwete toka alipochagualiwa kuwa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania amekuwa kiongozi ambaye amepata shahada zaidi ya moja nje ya nchi na
ndani ya nchi;
Kwa maneno
mengine ni kuwa Dr. Kikwete amekuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya jamii
katika mfumo wa moja kwa moja (direct) na kwa kupitia viongozi wengine ( in
direct) katika kuonyesha njia na kutekeleza majukumu amabayo amekabidhiwa kwa
kulingana na katiba yetu;
Shahada hizi
zote ambazo amepata zinahusiana na utendaji wa kazi ambao unampa sifa yeye
kufikia kilele hiki na utekelezaji wa majukumu.
Kwa wale wote ambao wanakaa darasani na kufanaya utafiti na hatimaye kufanikiwa
kutunikiwa shahada mbalimbali lengo kubwa na la msingi wake ni kuwawezesha kuelewa na mambo mbali mbali kupita uchambuzi
wa vitabu na utafiti na kutumia elimu hiyo katika kutatua matatizo ya jamii
inayowazunguka;
Lakini kwa
upande mwingine viongozi mbali mbali ambao hawana shahada ya juu wanaweza kwa
namna moja au nyingine wakawa ni wasomi wakubwa sana ambao wanaweza kutatua
matatizo ya jamii kuliko hata kama wengekuwa wamesomea kozi husika. Tuchukue
utambuzi ambao Kenya waliona na kuamua kumtunukia Mheshimiwa Kikwete shahada ya
heshima kupitia chuo kikuu cha kenyatta,”
kwa ujasiri wake wa kusuluhisha ugonvi wa kibaki na oginga 2008; suluhu hii ya
ugomvi ilikuwa na maana kubwa sana katika nchi ya Kenya baada ya vifo vya
wenyewe kwa wenyewe;
Je unafikiri
kuwa “baadhi ya maelezo” ya hapo chini
yana mpa sifa
Dr. Kikwete
kutunukiwa shahada hizo zote za heshima?
Dr. Kikwete kama
kiongozi wa chama na serikali ametumia muda wake mwingi kukemea Ufisadi unaofanywa
ndani ya chama twawala na , serikali yake
Dr. Kikwete
amekuwa mbele katika kuimarisha utawala
bora miongoni mwa jamii;
Dr.Kikwete
ariruhusu kuundwa kwa tume huru ya
kuchunguza mikataba mibovu katka sekta mbalimbali zenye kulalamikiwa na wananchi
Kuhusu
demokrasia, Kikwete amepiga hatua kwa kuruhusu kwa wazi mijadala mbalimbali.
Vyombo vya habari na wananchi wamekuwa huru kuibua hoja mbalimbali zikiwamo
hata zile zinazodhalilisha serikali pamoja na kuagizi kuandikwa upya kwa
katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania iweze kuendana na miaka hamsini ya
uhuru
Rais
Kikwete ameendelea kuwa msikivu na kupokea hoja zilizotolewa na makundi
mbalimbali ya Watanzania na kuzitafutia majibu kulingana na mipaka yake na bila
kuingilia chombo kingine cha maamuzi.
Dr. Kikwete ameweza
kuiagiza chombo kinachuhusika kutenda haki kwa watuhumiwa wa fedha za Akaunti
ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) na wale
wote waliotumia madaraka yao vibaya; uamuzi huu wa busara unatoa matumaini kwamba rais kweli amedhamiria
kupambana na ufisadi ambao unatishia uhai wa uchumi wa nchi yetu,
Kikwete kwa kiasi
kikubwa kaonyesha kutoingilia Bunge wala Mahakama katika utendaji, ndiyo maana
baadhi ya mambo yamefanikiwa.
Dr. Kikwete amesaidia
kuleta suluhu Kenya na Zimbabwe na kuuweka uongozi wa umma Comoro, baada ya
kutuma vikosi vyetu huko.
Amesimamia muafaka
kati ya CCM na CUF mpaka serikali ya
umoja wa kitaifa imepatika na inafanya kazi kwa kushirikiana vizuri sana.
Lakini ikumbukwe kuwa
hata wasomi ambao wanakaa darasani katiki kusomea shahada kama aliyopewa
mheshimiwa Kikwete wanakabilia na “ challenges”; na kwa msingi huu Si rahisi
kwa binadamu akawa na mazuri matupu; hakuna aliye mkamilifu kwani sisi si
malaika na Mheshimiwa Kikwete kadhalika,kama binadamu anayomapungufu yake;
Rais Kikwete kwa
mazuri aliyofanya anastahili heshima hiyo kwa pamoja na mapungufu yake na kama kiongozi bado
ana muda wa kurekebisha kasoro zilizojitokeza katika uongozi wake kwa kuendelea
kuwabana watendaji wake walio chini yake; lakini tusisahau kuwa nasi
tunamchango wa kufanikisha maendeleo yetu tukishirikiana na Mheshimiwa Rais
wetu.
HONGERA SANA
MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA KUTUNIKIWA SHAHADA ZA JUU ZA HESHIMA
NJE NA NDANI YA NCHI
Karibu
tujadili kwa maendeleo ya Taifa letu
Nilihudhuria siku ambapo JK alipata digirii ya heshima ya udaktari katika Chuo Kikuu cha St. Thomas hapa Minneapolis. Habari za tukio hilo ni hizi hapa.
ReplyDelete