Kwa nini tunaikumbuka Mwalimu Nyerere
siku hii ya leo miaka 12 baada ya kifo chake?
Nyerere alikuwa anawaambia viongozi waliokuwa chini yake kuwa:
·
kama unahitaji heshimna yangu nionyeshe
kuwa unastahili kwa kutimiza wajibu wako
·
Wewe sio mtu mbaya kama umefanya kosa
lakini utakuwa mtu mbaya kwa taifa la Tanzania kama utashindwakujifunza
kutokana na kosa lako.
·
Kimya changu wakati mwingine si kwamba
nimesahau au nimedharau hapana kwani hata mlima unaweza kuwa kimya lakini una volcano ndani yake na siku ikilipuka matokeo yake tunayajua
·
Sio kila jambo mtakalo lifanya litamfurahisha
kila mtu hapana, lakini kuna kitu kimoja
tu kizuri kuhusu kila mtu katika taifa hili ni ustawi wa jamii yetu na amani
yetu
·
Kama kuna viongozi wanasababisha utendaji
ulio mbovu, lazima tuwawajibishe na tusiwaonee huruma hata kidogo
·
Kwa nini tusiwatendee wananchi wetu vile
tunavyotaka sisi kutendewa au vile sisi tunavyojitendea?
·
Nyerere daima macho yake yalikuwa yakiuma
kwa kulilia haki za wanyonge, moyo wake ulikuwa ukiuma kwa kujaribu kuwaletea
maendeleo wanyonge lakini mafanikio yalikuwa madogo kutokana na umasikini wa taifa letu na Roho
yake ulikuwa ikiuma kwa kuwaombea wananchi wake amani na ustawi kitu ambacho alifurahi mpaka kufa kwake kulikuwa na amani na utulivu; kwa kuendelea kukosoana kwa hoja na sio matumizi ya nguvu.
·
Kwa kweli wakati mwingine maisha yanakuwa magumu lakini
mara nyingi sisi viongozi tunayafanya maisha kuwa magumu kwa wananchi wetu kwa
maslahi yetu binafsi; Ugumu wa upatikanaji wa huduma za jamii nani anasababisha ugumu wa mafanikio yake? tatizo la mgao wa umeme linaloendelea hivi sasa nchini nini chanzo chake kikubwa? uzembe uko wapi? nani wa kulaumiwa?
·
Katika maisha yetu ya kila siku ni kweli
kuwa matatizo yanayoikumba taifa letu yataendeleea kuwapo na kamwe
hayataisha mara moja, basi inatupasa kama viongozi kuendelea kuyataua, na kuyakabili bila kuchoka. Je taifa letu limejipanga vipi kuhusu kuhusu ongezeko la watu ukilingananisha na huduma zinazotolewa? je uwiano wa huduma na ukuaji miji yetu na ongezeko la watu ni sawa? nini kifanyike sasa?
No comments:
Post a Comment