MAJUKUMU YA VYAMA VYA SIASA NI NINI BAADA YA UCHAGUZI?
Je uchochezi na kuleta vurugu dhidi ya chama kilichoshinda
kuongoza nchi?
Je malumbano baina ya vyama vya upinzania
vyenjewe?
Je vinabaki vyama vya msimu kwa kusubiri
uchaguzi ujao na ruzuku?
Jukumu kubwa la chama chochote
cha upinzani ni kuangalia kwa makini sera za chama tawala, na kuzipinga pale
ipasapo, na kutoa mikakati na sera mbadala na kuwafahamisha wananchi kuhusu
masuala yote ambayo yanahusu uendeshwaji wa serikali.
Kila kimoja kinapokuwa
kwenye upinzani kinakuwa na kazi ya kukikosoa chama kilicho madarakani ili
kukipa changamoto katika kufanya kazi vizuri. Uwajibikaji wao utawapa fursa wapiga
kura kuafanya uamuzi wao kutokana na mafanikio ama kushindwa kwa chama
kilichokuwa madarakani kutimiza yale iliyokusudia kuyafanya.
Je kama vyama vya upinzani vinalumbana vyenyewe kwa
vyenjewe matokeo yake nini?
·
Vinapoteza muda na malengo ya vyama vyao
kwa kuanza kulumbana na wapinzani wenzao. Kwa kufanya hivyo, vinajidhoofisha
vyenyewe.
·
Vinapopambana vyenyewe kwa vyenyewe
vinakipa chama tawala kupata upenyo wa kuendelea kutawala na kupata hoja ya
kuvisema na hata chama tawala kisipotekeleza sera zake kunakuwa hakuna chama
mbadala cha kuwaambia wananchi mapungufu ya chama tawala
Umuhimu wa Elimu ya uraia na mikakati ya vyama kushika dola ya kuongoza
nchi
Ukosefu wa elimu ya uraia
imetufanya wengi wetu kuingia katika malumbano ambayo yanafanya safari ya
kuelekea demokrasia bora kuwa sio nyepesi.
Kuna haja ya kuanziasha makakati wa kitaifa wa
kutoa elimu ya uraia kwa wananchi. Jambo hili litafanyika kama serikali itakuwa
na nia ya kuleta demokrasia ya kweli nchini.
Ulazima wa elimu ya uraia
upo sana kwa mwananchi wa kawaida kuelewa dhana ya mfumo wa vyama vingi na
umuhimu wake katika uendeshaji wa masuala ya kila siku ya serikali na sio ile
maana ambayo ipo kwamba chama cha upinzani ni fujo, kupoteza amani na utulivu
wa nchi, hawana sera au ni wapinzani wa kila kitu kumbe maana haswa sio hiyo
bali ni waangaliaji wa kile kinachofanywa na serikali na penye mapungufu
kukosoa
Ndo maana nasema elimu ya
uraia ni muhimu sana katika kuhakikisha kuwa dhana nzima ya chama tawala na
chama cha upinzani inaeleweka na nini umuhimu wa kuwepo kw achama cha upinzani
katika kuhakikisha kuwa chama tawala kinawajibika kutekeleza sera zake
Kwa nini vituko kati ya
chama Tawala na vyama vya upinzani ni sehemu yapropaganda ya siasa?
Vyama vya upinzani
vinatakiwa viendelee kuwajibika, katika mazingira yeyote yale dhidi ya chama
tawala lakini kwa busara ili kukubalika miongoni mwa wananchi; chama tawala
daima kitakuwa kinajitahidi kuhoofisha upinzani, kufanya uwe dhaifu, na daima ili kuvipunguza kasi vyama vya upinzani na kuvifanya kuwa haviwezi kuwa na majadiliano ya kuijenga nchi;
Demokrasia ni demokrasia na daima inataka Pande
zote mbili kati ya chama tawala na upinzani kwa pamoja kuzingatia sheria za mchezo. Demokrasia
kama msimamiza wa kandanda ya siasa inapinga vikali wachezaji kucheza “ Rafu”
na daima inawategemea wananchi katika kusaidia katika maamuzi ya sahihi na kufanya kandanda ya siasa
kuwa safi; kwa hiyo ni jukumu la wananchi kuelewa sheria na elimu ya mchezo huu. Tusipofanya jitihada
za dhati kabisa katika kulielewa hili Demokrasia
inakuwa fujo.
Ni dhahiri kwamba kama
watu wako makini na wanachuikua taadhari , nguvu zote bila kupita katika mikono
ya wanasiasa wajanja kitaalamu na waaribifu ambao mara chache hujitashidi
kuwarubuni raia ambao hawana elimu ya kutosha na wale ambao wako katika
mazingira magumu katika kutekeleza sera
ambazo kuwasaidia kuendeleza utawala wao.
Vyama vya upinzani wakati wote
vinatakiwa kuwa na uwezo wa hoja ili
kuweza kukuza majadiliano
na mijadala, na kujitahidi kuachana na mayowe, hoja za nguvu ili kuviwezesha
vyama hivyo kubaki katika mijadala ambayo itakuwa na tija kwa
wananchi kama mijadala ya afya , ustawi wa jamii na uwajibishaji wa serikali
iliyoko madarakani; na bila kusahau kuendeleza aina fulani ya "mazungumzo
ya kitaifa" na kushinikiza mjadala wa kidemokrasia kwa kiwango cha juu ya ili
kuleta zaidi ukomavu wa demokrasia nchini;
Ili kujiimarisha zaidi
miongoni mwa wananchama wao na wananchi kwa ujumla nyama vya upinzani
vinatakiwa daima viweze kujisafisha na kuwa na rekodi nzuri ya matumizi ya
fedha. Kukumbuke kuwa uwajibikaji uanza ndani ya chama chenyewe; upinzani ili
kudumisha uwazi, vinatakiwa wakati wa mikutano yao ya ndani itawaliwe na uwazi;
kiwe ni chama cha wote na sio chama cha mtu Fulani au kikundi Fulani cha watu. kuhakikisha
matumizi ya fedha za chama kuwajibika ni zaidi ya uwezekano wa kubeba sifa hizi
ndani ya utawala wake
Vyama vingi vya upinzani
daima vinakabiliwa sana migogoro ya ndani na ukosefu wa Utawala bora ili kujihakikishia ushindi katika
kinyanganyiro cha ushindi wa kuongoza nchi vyama vya upinzani lazima vijenge
jitihada za kichama katika kuimarisha demokrasia mahiri wa ndani ili iweze kusamabaa
baina ya wananchi ambao ndio washika dau wakuu tukumbuke kuwa “ Love starts at home”
kwa kufanya hivyo vyama vya
upinzani vitakuwa vimefanikiwa kutimiza Lengo la kuimarisha demokrasia ndani ya chama kabla
ya kuwa mabingwa wa demokrasia na utawala bora kitaifa. Demokrasia
ya kweli haiwezi kustawi bila upinzani mahiri.
Namaliza kwa kujiuliza je vyama vyetu vya upinzani hapa Tanzania vinafanyaje kazi zake?
vinapingana kwa hoja dhidi ya serikali iliyopo madarakani?
vimeweza kujiimarisha na kutoa elimu ya uraia kwa wananchi waishio vijijini, au vinajikiti katika miji mikuu tu ya wilaya au mikoa?
na wanapotofautia na serikali vinatumia mbinu gani katika kuhakikisha kuwa hoja imefika bila kuvunja amani yetu?
Lakini tusisahau kuwa "Politics is a dirty game. A good person shouldn't be involved in it."
No comments:
Post a Comment