UONGOZI USIO NA TIJA
HUZORETESHA ELIMU BORA YA URAIA MIONGONI MWA WAPIGA KURA WAISHIO VIJIJINI
Kipimo cha uongozi bora ambao hutokana na uongozi
uliotukuka ni pale tu wapiga kura wanapoufurahia
uwajibikaji wa viongozi walioko madarakani kwa kuwatatulia kero
ambazo zinahitaji nguvu ya serikali kama huduma bora za jamii kwa maendeleo yao.
Lakini katika nchi
zinazoendelea, bado zinabaki kuwa wahanga wa migogoro ya kiuchumi na kisiasa.
sababu kubwa ya migogoro hii ni uongozi mbaya katika nchi husika.
Tanzania kama nchi
nyingine za kiafrika bado tunakabiliwa na hali mbaya inayotokana na ubadhirifu
wa fedha na utumiaji mbaya wa madaraka ambayo baada ya kumsaidia Mwananchi
kumkwamua kiuchumi na kijamii bado mwananchi wanaendelee kukabiliwa na tatizo
la umasikini.
Uchambuzi
wa maswala ya kiuchumi unatukumbusha kuwa nchi ikifikia katika hali hii inatuonyesha
kuwa kuna tatizo la utawala bora, kuna tatizo la uzalendo kuna tatizo la balance of power;Je serikali
inasimama upande upi? Kumsaidia wananchi wa kawaida au kuwatajirisha mtu mtu
mmoja mmoja au kikundi cha watu wachache kwa masilahi binafsi?
Je ni
nani waliowaweka viongozi madarakami ni wananchi wanyonge walio wengi au ni
kikundi kidogo cha watu wenye pesa?
Kama ni
wananchi ambao ndio waliowachagua viongozi kwa kura zao; kwa maoni yangu kama wananchi kuendelea
kuishi katika lindi la umasikini katika nchi yenye rasilimali nyingi ambazo nchi
inamiliki ni ukiukaji wa haki za binadamu.
Hivi sasa kama Taifa tunahitaji viongozi ambao wataweza kuwatetea na kuwaletea wananchi wao maendeleo;
Tunahitaji viongozi waaminifu na wasafi; hili ni jambo la muhimu sana kwa
maendeleo ya taifa tukuangalia sana viongozi wetu wanakosa sana sifa hizi mbili
kuu muhimu; viongozi wengi wa Afrika wamechagua kutekeleza sera maovu(ufisadi) badala ya upendo mkubwa kwa taifa(
utawala Bora) husika.
Nafikiri
itakuwa ni jambo la busara kama viongozi wetu watakubali kusimamia elimu ya
uraia kwa wananchi wa vijijini ili kusaidia katika mageuzi ya kuboresha utawala
na kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi, na utulivu wa kisiasa ambao ni sehemu ya utawala bora na
utekelezaji wa kidemokrasia wanayohubiri.
Tatizo
la viongozi wetu wanashindwa kuja na vision nzuri ambayo kweli itasaidia maendeleo na kuondoa kero ambazo
wananchi wanakabiliwa nazo kila siku;
Hali
hii tata kushindwa kutatua malalamiko ya wananchi kwa miaka mingi ilimpelekea Robert Wheelen wa Taasisi ya
Uchumi. Katika jarida la taasisi ya mwezi Septemba 1996 kuuliza’ kwa nini nchi ya
afrika isibinafsishwe kwa nchi tajiri ili kuwasaidia kutatua kero
zinazowakabili na kuwasaidia katika kusimamia katika kutoa huduma bora na
kuleta ufanisi na nidhamu wa ukusanyaji kodi kwa maendeleo
ya nchi zao’
Kauli hii wakati mwingine
inaingia akilini pengine kuna kweli kama viongozi wetu wanaelekea kushindwa
kutatua kweli za wananchi wao pengine swala hili la ubinafsishaji linaweza kuwa
ni suluhisho la maendeleo kwa wote;
Maswali ninayojiuliza kutoka na
kauli hii;
· Je Serikali yetu ya Tanzania
imefanikiwa kwa kiasi gani katika ukusanyaji wa kodi hali ambayo imefikiwa sasa
tunaweza kujisifu tumepiga hatua au bado juhudi zinahitajika katika kuendelea
kufanikisha hili?
· Je Serikali yetu inasimamiaje shughuli zake za
kuendesha serikali kwa faida ya wote, je utawala bora unatekelezwa au bado tuna usugu wa usimamizi mbovu chini
na ukosefu wa uwezo wa utawala bora?.
· Je Serikali yetu imeandaaje
miundo na mageuzi ambayo yataimarisha utawala wa sheria, kusaidia kukuza
demokrasia na uwajibikaji na uwazi.
· Je kwa nini wazee wetu kama
Mandela, Nkrumah na Nyerere wameendelea kuwa viongozi bora na wa kuheshimika
ndani ya nchi na nje ya nchi zao?
· Je viongozi bora wanatakiwa
wawe na sifa gani?
kwa matazamo wangu:
- anayeweza
kuwasiliana na
kuwasilisha hoja kwa ufasaha,
- mwenye
uwazi na mawazo mapya,
- uwezo
wa kusikiliza pande zote za mipango endelevu,
- mwenye
hekima na akili ya kawaida,
- uwezo
wa kusimama na
kuongoza wakati political or economic crises ,
- kujua
ukweli kabla ya kufanya maamuzi,
- Kiongozi bora lazima awe mchapa kazi na mwajibikaji
Tunamkumbuka Mwalimu
Nyerere alipoamua kwa hiari yake kuachia madaraka na kutengeneza platform kwa
kiongozi wa kuchukua madaraka ya urais kwa kupitia vikao halali ndani ya chama
chake na nje ya chama chake.
Kwa msingi huu Viongozi bora kuandaa watu wao wa kuendeleza
safari ya uongozi wa nchi bila woga wa kushitakiwa wakiwa nje ya madaraka;
viongozi wetu lazima wajifunze kuwa mabadiliko ya uongozi ni muhimu kwa ajili ya kuanzisha
tawala mpya. Hapa ndipo
tunapoona umuhimu wa elimu bora ya Uraia.
Utawala
bora ni utekelezaji wa uwezo na mamlaka na serikali kwa njia ya kuwa watumishi
bora wanaoweza kuboresha ubora wa maisha ya wananchi wake. Hii itasaidia
kujenga jamii bora na yenye uwezo wa kujikwamua na kupambana na changamoto
zinapojitokeza
Na hitimisha kwa kusema
kuwa Kuwa kiongozi bora si kazi rahisi wakati mwingine inahitaji mtu kuwa na maono ya
mabadiliko, elimu ya utambuzi, mawasiliano ya wazi bila woga, na kuwa tayari
kufanya maamuzi magumu. Tunahitaji viongozi ambao ni wawajibikaji wa maendeleo yetu; ambao watusaidia sisi kukimbia wakati wenzetu wanatembea katika kuyatafuta maisha bora. Tunawaombea viongozi wetu waweze
kuwa charisma na maono ya kujenga upya taifa letu kisiasa na kiuchumi kwa
maendeleo ya wananchi wao bila kusahau elimu bora ya uraia.
No comments:
Post a Comment