WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, September 25, 2011

IGUNGA INATUPELEKA WAPI KAMA TAIFA


Igunga imegeuka fitina ugomvi na mbaya zaidi sio ugomvi wa hoja ni ugomvi wa misuri ambao hauna tija kwa Taifa letu.

Tunaendelea kujiuliza kwa nini wakati kampeni za hicho kiti kimoja tu zikiwa zinakaribia kufikia ukingoni  tunaendelea kushuhudia matukio yanayotishia uvunjaji wa amani, yanazidi kuongezeka.
Kama vile, Kudhalilishwa kwa watendaji serikali na vyama na serikali




Kujihami kwa baadhi ya viongozi hadharani, kama ndugu yetu Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM), akiwa na bastola kiunoni akiwa akihutubia katika mkutano wa kampeni. Kama magazeti mengi  yalivyoonyesha kuwa” Bastola ya Rage ilionekana wakati mbunge huyo akijiandaa kupanda jukwaani kwa ajili ya kumnadi mgombea ubunge wa CCM kwenye moja ya mikutano ya kampeni jimboni humo”.





Kama Mwandishi  wa makala hiyo alipouliza”Kwa sababu hiyo, tunajiuliza, Rage alikuwa akikabiliwa na hatari gani hadi kulazimika kupanda jukwaani ni bastola? Hivi kila mwenye silaha ya moto Igunga akisema atembee na silaha yake hali itakuwaje?Na kwa wasio na silaha za moto, wakiamua kutoka na silaha za jadi kama mishale, visu, mapanga na zinginezo, Igunga patakalika? Sisi hatuungi mkono kitendo hicho na tunalitaka jeshi la Polisi kuchukua hatua ili kuhakikisha kampeni za uchaguzi Igunga na hatimaye uchaguzi wake, unafanyika katika mazingira ya utulivu na amani.”


Nakubaliana kabisa na mwandishi wa makala hii kuwa huu ni udhaifu mkubwa kabisa kwa wasimamizi wetu wa maswala ya amani na utulivu; Mheshimiwa Mbunge hakuwa na sababu yeyote ile ya kuja kwenye kampeni na silaha, kama alikuwa na uhakika kuwa usalama wake ulikuwa mashakani kulikuwa hakuna sababu yeyote kwa yeye kujumuika katika kampeni  kwa siku na wakati kama huo.



Tunafahamu kuwa vikosi vyetu vya ulinzi na usalama jamani viko na vinaendelea kuwa makini katika kulinda amani ya wakaazi wa Igunga na taifa kwa ujumla katika wakati huu wote wa kampeni;



Tukio nyingine ambalo nalo limepigiwa sana kelele ni kitendo alichofanyiwa DC; kwa wahusika wote wale katika sakata hili la kumdhalilisha Mama huyu; kumekuwa na matumizi ya nguvu zaidi kuliko busara;hata kama wahusika wanakana na kuona waliyofanya ni sawa, ukweli ni kuwa kosa lilifanyika watake wasitake; Busara busara jamani tunahitaji sasa kuliko wakati mwingine wowote huko nyuma.


Bado ni ukweli ambao haufichiki kuwa Heshima kwa viongozi wetu  na hata kwa mtanzania yeyote na  mtu yeyote ni muhimu. Nafikiri tulitakiwa kuangalia sheria na hatua zake na sio kumdhalisha kama alivyofanyiwa huko igunga katika eneo lake la kazi. Ni busara kujaribu kuepuka kujichukulia sheria mkononi;

Tukikumbuka sana wosia wa  Baba wa Taifa kuwa watanzania wote ni ndugu. Ni vema basi sote kama taifa tukafuata sheria tulizojiwekea bila kujali itikadi za vyama; na wabunge wetu wakawa mstari wa mbele katika kuishi kwa matendo yale wanayoyapitisha bungeni na sio kuwa vinara wa kuongoza fujo na uvunjaji wa sheria hizo. Sisi kama taifa tujitahidi kwa pamoja kudumisha amani! “Inawezekana timiza wajibu wako”

Hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa mawazo, ni umaskini mbaya  sana'  Mwalimu J. K. Nyerere,

Mtu mwenye akili akikuambia neno la kipumbavu -ukalikubali, anakudharau!'  Mwalimu Nyerere


Kama  Taifa tusimame imara katika kupigania "umoja, amani na upendo miongoni mwetu" hii ni kati ya zawadi kubwa sana ambayo  waasisi wa taifa letu Mwalimu Nyeyere na Mzee Abeid Karume walituachia

Tuache kuburuzwa na upepo wa siasa na wanasiasa; ambao wanapigania zaidi masilahi binafsi  na sio masilahi ya taifa, tufunguke sasa.

Nawatakieni Kampeni za mwisho mwisho zenye amani  na nguvu ya Hoja na sio matumizi ya Misuri

No comments:

Post a Comment