WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, October 6, 2012

Maalim hamad asema hakuna atakayevuna kwa vurugu




Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar   Maalim Seif Sharif Hamad amewataka wananchi kuacha tabia ya kufanya vurugu kwa lengo la kuvunja amani na utilivu  Zanzibar.

Amesema bado liko kundi la watu ambao wanazembea hatua ya  amani na utulivu
uliopo Zanzibar na kujaribu kutaka kuleta machafuko katika nchi. Maalim Seif ameyaeleza hayo huko Hoteli ya Grand Palace ilioko Malindi mjini Zanzibar wakati akizungumza na Waandishi wa Habari. Amesema,Serikali iliopo sio kama haiwezi kuchukuwa  hatua kali bali inafanyakazi kwa utaratibu maalum ili kuepuka utumiaji wa nguvu.

Ameongeza  pindi Serikali ikichukuwa hatuwa kali watu wataanza kupiga
kelele na kusema kuwa  wanaonewa na zinakiukwa haki za kibinaadamu.

Hivyo aliwaonya wenye tabia hio kuacha mara moja tabia hiyo ya kuleta
vurugu na fujo kwani hali ikiwa mbaya hakuna mtu atakaefaidika na kitu.

Maalim Seif ambae ni Makamo wa Rais wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar alisema wapo baadhi  ya watu ambao hudhani pakiwa na
fujo na ghasia wanafaidika jambo hilo sio kweli kwani kukitokea vurugu na
Serikali kuchukuwa hatua kali hakuna atakaefaidika bali itakuwa hasara kwa
Wananchi.

Hivyo  aliwasihi Wananchi kuacha  na kuendelea kudumisha Amani na Utulivu
ambao ni jambo la kujivunia.

Makamo  wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar alitowa Mfano wa nchi zenye mizozo na
kusema hakuna maendeleo yanayopatikana na watu wanaishi katika hofu na
wasiwasi.

Akizungumzia suala la Uchumi wa Zanzibar,MaalimSeif amesema Uchumi wa
Zanzibar unakuwa kwa kiasi ,kwani mwaka 2011 ukuwaji wa Uchumi ni 6.8 na
unatarajia kuongezeka mwaka 2012/2013 na unatarajia kufikia  asilimia 7.5
wakati pato la Mzanzibari linakuwa kutoka TSHS  782,000 kwa mwaka hadi
kufikia TSHS 960,000 ambazo ni sawa na Dolla za Kimarekani 615 kutoka 560
mwaka 2010.

Ameongeza kuwa lengo la Serikaliya Mapinduzi Zanzibar ni kufikia lengo la
Melenium ambapo nchi zote zinatakiwa ifikapo mwaka 2015 pato la Wananchi
wake liwe TSHS 884,000 sambamba na kuonekana fedha  mifukoni na sio kwenye
makaratasi.

Kuhusu matumizi ya fedha za Serikali, Maalim Seif alisema bado Serikali
inakabiliana na changamoto kubwa juu ya matumizi ovyo ya fedha za Serikali.

Amesema Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za  Serikali ya mwaka
2010/2011 imeonyesha bado wako baadhi ya Watendaji hujinufaisha kupitia
fedha za Serikali jambo ambalo sio zuri na halikubaliki.

Amesema ,tatizo la matumizi yasiofuata taratibu linaendelea kujitokeza. Pia
udhaifu wa kukosekana baadhi ya vielelezo muhimu katika ukusanyaji na
matumizi ya Mapato limeonekana kujitokeza katika Taasisi mbali mbali za
Serikali , kutokana na uchunguzi uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Aidha Maalim Seif alisema kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar amebaini kuwa kuna matatizo kwa baadhi ya
Taasisi za Serikali kutokusanya mapato ipasavyo pamoja na kutumia fedha
bila kufuata taratibu za Kisheria za fedha na malengo waliojipangia wenyewe
Taasisi hizo.

Amesema kuwa ipo Miradi mingi imepewa fedha nyingi katika utekelezeaji wake
lakini kazi iliotendeka hailingani na fedha zilizotolewa.

Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema kuwa, Serikali haitovumilia
kuona baadhi ya Watendaji wanaendelea kukiuka sheria ziliopo za fedha na
kuchukuwa fedha za Wananchi kujinufaisha binafsi.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment