NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
6/10/2012
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema kuwa Tanzania itaendelea kutafuta msuluhishi wa mgogoro wa mpaka kati ya Malawi na Tanzania kuhusu ziwa Nyasa iwapo nchi hiyo haitaweza kuja kwenye meza ya mazungumzo juu ya suala hilo kwa kuchukua hatua mbalimbali.
Mazungumzo ya mgogoro huo ambayo yangetarajiwa kuanzia Oktoba 7 hadi 10, mwaka huu, kinachotarajiwa kufanyika jijini Dares Salaam.
Aidha Waziri Membe alitoa pendekezo kwa serikali ya Malawi kwa kuiomba kuwa ikubali timu mbili zilizokuwa katika mazungumzo hayo zikaendelea kukutana ili kuweza kupendekeza msuluhishi wa tatizo hilo kwa pamoja.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri huyo katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya ziara kurejea nchini hapa kutoka Canada alipokuwa akihudhuria mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa usiku wa kuamkia leo kuhusu hatua ya serikali ya Malawi kuandika barua mbili kwa serikali ya Tanzania mwishoni mwa mwezi uliopita.
Ambapo alisema wamesitushwa na uamuzi huo ,kabla ya kujibu barua hizo.
“Ikiwa Malawi hawatakuja katika meza ya mazungumzo tutaendelea kutafuta msuluhishi juu ya tatizo hili. Tumeamua kulimaliza suala hili chini ya uongozi wa Rais wa Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete kwa kutumia timu za wataalamu tatu, ambazo ni wakumbukumbu ambao wataishia kuchukuia kumbukumbu za maisha ya ziwa hili kabla na baada ya mwaka 1890 nchini Uingereza, pia kukupitia nyaraka mbalimbali itakazozitumia ”alisema . Waziri Membe.
Waziri Membe alitaja timu nyingine kuwa ni za wanasheria ambapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali atahusishwa ili kuangalia namna ya kutoa tamko katika Mahakama ya Kimataifa ya Utatuzi wa Migogoro(ICJ) kuitambua na timu yake ya washauri yenye ujumbe wa watu 14.
Aliongeza kuwa tatizo hilo pia linaweza kushughulikiwa na marais wastaafu wa Nchi zilizo katika Jumuia ya Maendeleo ya Uchumi ya Kusini mwa Afrika (SADC), kupendekeza mtu wa kusuluhisha mgogoro huo kwa kupendekeza majina matatu na kutumia kitengo cha usuluhushi wa migogoro chini ya Umoja wa nchi za Afrika wanaweza kuja kusuluhisha.
Hata hivyo alisema kuwa Malawi haiwezi kuipeleka Tanzania ICJ kwa kuwa nchi yetu bado haijatoa tamko la kuikubali ICJ ingawa wao weshaikubali tangu mwaka 1969.
“Malawi haiwezi kutupeleka sisi ICJ mpaka tukae katika meza moja tukubaliane nao kuwa twende ICJ,” alisisitiza huku akisema wakifanya hivyo watarudishwa mpaka wakubaliane na Tanzania. Ila sisi tunaweza kuikubali ICJ hata leo na kwenda kuwashtaki Malawi,” alisisitiza.
Akifafanua kuhusu barua hizo, alisema ya kwanza ilikuwa ililalamika juu ya boti Tanzania kupeleka boti katika ziwa hilo na kutaka iondolewe.
Alisema barua ya pili ni kutoka nchini humo inahusu kitendo cha serikali ya Tanzania kuchapisha ramani mpya ambayo inaonesha mpaka wa ziwa hilo kwa Tanzania kuwa upo katikati na kusema kuwa kinaonekana kuwa ni cha kichochezi.
Waziri Membe alifafanua malalamiko hayo alisema boti hiyo ni timu ya utalii na mifugo na uvuvi ambao wanafanya doria kama kawaida na wanasaka wavuvi haramu, hivyo madai hayo si ya kweli boti namna hiyo ipo pia katika ziwa Tanganyika na Viktoria kwa ajili ya kulinda usalama maeneo ya majini.
Aidha alisema lalamiko la pili kuhusu ramani mpya alisema imechapishwa kwa ajili ya kuonesha mipaka ya mikoa minne na wilaya 19 ili viongozi wa maeneo husika watambue mipaka yao na imeonesha mpaka wa ziwa hilo baina ya Malawi na Tanzania uko katikati kama ilivyo katika mkataba wa Heligoland wa mwaka 1890 ,hivyo usingewezwa kuonesha uko kwenye fukwe kama wanavyodai Malawi.
No comments:
Post a Comment