WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, October 11, 2012

YANGA WAISHUTUMU SIMBA KWA KUTIA MKONO MECHI ZAO




Na Mahmoud Zubeiry

MWENYEKITI wa Yanga, Yussuf Mehboob Manji anakwenda Mwanza kuongeza morali ya wachezaji kwa ajili ya mechi ya kesho ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, dhidi ya wenyeji Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kesho.
Habari kutoka ndani ya Yanga, ambazo BIN ZUBEIRY imezipata zimesema kwamba Manji ameamua kwenda mwenyewe Mwanza, kufuatia timu kupoteza mechi ya Bukoba juzi mbele ya wenyeji Kagera Sugar kwa kufungwa 1-0.
“Mwenyekiti anakwenda Mwanza, ili kwenda kuongeza morali ya wachezaji, timu iweze kushinda mechi ya kesho,”kimesema chanzo chetu kutoka Yanga ‘mida hii’.
Baada ya kufungwa na Kagera, Yanga wamedai wamegundua Simba SC ‘wanatia mkono’ kwenye mechi zao na ndio maana zinakuwa ngumu, ila kuanzia sasa na wao wanaanza ‘fitina’.
“Simba ilituma watu Bukoba watie mkono mechi yetu, sisi tuliwashitukia hao watu baadaye sana, lakini tunashangaa kwa nini wanafanya hivi, wakati sisi tulizungumza nao tukakubaliana haya mambo tuyaache, tucheze mpira, sasa wao wanatuzunguka wanaendeleza mchezo mchafu,”alisema kiongozi Mjumbe mmoja wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, ambaye hakutaka kutajwa jina.
Mjumbe huyo alisema kwamba wao walijua baada ya makubaliano na Simba kutofanyiana fitina, waliamini mambo hayo hayatakuwapo, lakini baada ya kugundua wenzao wamewageuka sasa na wao wanaanza ‘mchezo huo’.
“Na sisi sasa tunaanza kuzicheza mechi zao, wakumbuke tu wao ndio walichokoza nyuki, sasa subirini kuanzia mechi yao na Coastal, wakishinda wao wanaume, na pamoja na kuzicheza mechi zao, tunajizatiti katika mechi zetu. Uzuri watu wote wanaowatumia tumekwishawajua, ni wale wale waliokuja Morogoro, na wale wale waliokuja Bukoba. Tumekwishawajua,”alisema Mjumbe huyo.
Bao pekee la Themi Felix katika dakika ya 67, juzi liliwapa Kagera Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga SC, kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Felix aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mnigeria, Enyinna Darlington kwa kumtungua bao hilo, kipa Mghana wa Yanga, Yaw Berko, ameendeleza rekodi yake kuvifunga vigogo, Simba na Yanga katika Uwanja huo.
Hiyo inakuwa mechi ya pili Yanga kufungwa ndani ya mechi sita walizocheza hadi sasa na mbili wametoka sare- maana yake inabaki na pointi zake nane na kuzidi kujipunguzia matumaini ya ubingwa msimu huu, ikiwa sasa inazidiwa pointi nane na vinara wa ligi hiyo Simba SC.
Aidha, hiyo ilikuwa ni mechi ya pili Yanga inacheza chini ya kocha wake mpya, Mholanzi Ernie Blandts aliyerithi mikoba ya Mbelgiji, Tom Saintfiet na katika mechi hizo mbili ameambulia pointi moja kutokana na sare dhidi ya Simba Jumatano.
Kwa ujumla Yanga haijashinda hata mechi moja ya ugenini kati ya tatu ilizocheza hadi sasa, ilitoka 0-0 na Prisons, ikafungwa 3-0 na Mtibwa na jana imechapwa 1-0 na Kagera Sugar, wakati Alhamisi itacheza na Toto African mjini Mwanza.
Katika mechi hiyo ya juzi, Yanga ilipata pigo dakika ya 23 baada ya mshambuliaji wake mahiri na tegemeo, Said Bahanuzi ‘Spider Man’ kuchanika nyama za paja dakika ya 23, baada ya kugongana na beki Benjamin Effe wa Kagera Sugar na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Jerry Tegete.
Tangu ajiunge na Yanga akitokea Mtibwa Sugar msimu huu, leo Bahanuzi amecheza mechi ya 13 kwa dakika hizo 23 na ameifungia timu hiyo jumla ya mabao 12, matatu kati ya hayo kwa penalti.

No comments:

Post a Comment