WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, October 10, 2012

Wazanzibar Kuondokana Na Tatizo La Mgao Wa Umeme


 


Na: Ali Issa Maelzo Zanzibar 
 
 Rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar DR Ali Muhamed Sheni amesema kukamilika kwa jitihada zakulaza waya mpya wa umeme kutoka Fumba hadi Rasi kilomoni Dar wazanzibari wataondokana na tatizo la umeme wa mgao linalo endelea hivisasa. Hayo ameyasema leo huko Fumba wakati wauzinduzi wa laini mpya ya umeme unao tarajiwa kumalizika disemba mwakahuu na kutoa huduma kwa wananchi wa Zanzibar ambao kwa muda mrefu wanatumia nishati hiyo ya umeme wa mgao . 

 Amesema hali hiyo itamalizika muda mfupi tu kwani umeme umnao lazwa waya wake una megawati 100 ambao utatoshelza mahitaji ya wazanzibari bila ya wasiwasi wowote. Amesema hali hiyo ni ya kufurahisha kwa wazanzibari kwani itaifanya zanzibar kuendeleza shughuli zake za kimaendeleo na kuinua uchumi zaidi bila upungufu wa huduma hiyo .

 “Waya uliopo una megawati 45 ambayo hii ni ndogo kwamatumizi ya wananchi lakini kukamilika kwa waya huu mpya uta tosheleza mahitaji ya watu na katika mazingira ya kawaida sirahisi umeme kukosekana ”ali sema DRsheni . DR sheni ali wasihi wana nchi kuku bali kuupokea na kuitunza huduma hiyo kwa mashirikiano kuazia ngazi ya shehia Wilaya Mikoa na Taifa kwa kuepuka kujenga ,kuchota mchanga na kadhalika karibú na nguzo za umeme .

 Aidha Raisi huyo alishukuru serikali ya marekani kupitia shirikalake la changa moto za milenia (MCA compact) ,seriaki ya japan kampuni ya VISCAS kwamengenezo ya waya huo na kuulaza baharini. Waya huwo umegharimu zaidi ya milioni ishirini 28 za kimarekani wenyeurefu wa kilomita 36.5 una njia za mawasiliano 24 kupitia mshipi teknohama (febre optic),una uwezo wa kuishi miaka 40 ,utalazwa kwa gharama zaidi ya milioni 72 za kimarekani na serikali ya Mapindunzi ya Zanzíbar imechangia 1,465,625.00 za marekani kufidia mali za wananchi zilizo athiriwa katika eneo la utekelezaji . 

 IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR .

No comments:

Post a Comment