WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, October 2, 2012

Watu 65 wamenusurika kufa Segera baada ya basi la Dar Express likitokea Arusha-Dar kuteketea kwa Moto.



Basi la abiria la kampuni ya Dar Express limepata ajali ya kuungua na kuteketea kwa moto leo asubuhi katika eneo la Segera kwenye njia panda ya Dar es Salaam-Arusha-Tanga.

Basi hilo lilikuwa likitokea Arusha kuelekea Dar es Salaam likiwa na abiria sitini na tano.

Imeripotiwa kuwa hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa au kupoteza uhai katika ajali hiyo isipokuwa mizigo yote ambayo iliteketea.

Basi hilo lilikuwa na wanafunzi. Askari usalama wa barabarani aliyekuwa zamu katika eneo hilo aliona moshi ukitoka na mara moja akawaamuru abiria wote kushuka. Muda mfupi baadaye gari hilo lilishika moto. Gari la zimamoto kutoka Korogwe lilikuwa likitarajiwa kufika katika eneo hilo kutoa msaada wa kudhibiti moto huo.

---
Picha na maelezo: Samweli Mikuza via blogu ya HabariMseto na tweet ya ITV Tanzania
Picture
Picture
Picture


Source: http://www.wavuti.com

No comments:

Post a Comment